Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli


Engine ina nguvu kama kawida na je inawezekana ikaleta shida kwenye engine???
 
Engine ina nguvu kama kawida na je inawezekana ikaleta shida kwenye engine???
Haina madhara immediately, ila in the long run inaweza kuharibu brake booster yako ukakosa brake, na vile vile inaweza kuvunja pistor rings. Unaweza kuendesha na hilo leak kwa muda hata miezi sita au zaidi bila matatizo yoyote lakini siku moja utapata madhara kama hayo niliyokutajia.
 

Noted mkuu
 
Boss nina runx tangu cc1500 ukiiwasha wakati imepoa kuna mliounatoka wa kugongq kwenye engines na oili ikishapanda ukazima gar na kuwasha tena huo.mlio unakua haupo sasa kunafund kaniambia engine imechoka kwahyo nibadil kununua ingine lakin mwingine anasema nibadili slepper,timing chain na timing chain tensioner naomben msaada nifanyaje
 
Nina gari yangu aina ya passo 990 cc 3 piston, bado mpya ina 40000km. Nikikata kona kali wkt narudi rivas, mfano nimekata kulia kwa rivas then nikitaka kwenda mbele kwa kona kali pia kuelekea kushota gari inazima na redio equalizer inareset. Hali hii imewahi kunitokea mambili hivi nikampelekea fundi wa umeme akasema siku ikitokea nimuite ili aweke mashine kuangalia tatizo inaelekea kuna short circuit sehem. Tatizo hapa ni nini mkuu.maana muda sasa hii hali sijaiona tena.

Pia hii ni passo ya 2 kudrive ya kwanza nliuza ndo nikanunua hii. So naomba kuelewenshwa pia kwa experience yangu kudrive passo nikifunga breki za gjafla ni kama chuma na chuma kinasuguana kwenye breki nakihisi mguuni, nlibadili shoe mpya ila inapotokea mfano kuna yale matuta ya kushtukiza maana huwa nasafiri nacho umbali mrefu mara kwa mara
 
Usishangae kuhusu utambulisho huu. Mimi sasa ni ASE Certified Service Consultant wa magari madogo yanayotumia petroli hasa ya Ford, GM, na Chrysler....

Nimekuwa nafuatilia sana elimu unayotoa mdogo wangu for sure am inspired, mpaka nikajiuliza nilikuwa wapi kusomea mambo kama haya, ukweli you deserve to be a lecturer somewhere, umenitoa mbali kwa elimu ya magari nakufuatilia sana.

Anyway nahitaji elimu zaidi maana ndugu yako namiliki subaru forester, iliwahi kuingia maji nikafanya kosa la kuiwasha niitoe ikashindikana, kilichotokea niliomba breakdown ikaichukua mpaka 0-60 garage magwiji wa subaru wanasema hawatengenezi gari aina nyingine, baada ya kuchunguza mfumo wake ni wa umeme wakabaini control box na stering reck zimeungua, wakabadirisha, lakini haikuisha hata miezi minne kurudi service gari ilikuwa inagonga wakasema stering reck imeharibika na ina gharama nikawastukia kuna mmoja akasema ataifanyia engineering itaendelea kutumika nikaogopa, NIMEPATA MSHAURI HAPA NAKAZIA ILI UNISHAURI POA, ANANIAMBIA MAFUNDI WENGI HUWA HAWAPENDI KUSEMA UKWELI, NI KWAMBA HIZI GARI HUWA ZIKIINGIA ILI ZIDUMU WANABADILISHA STERING RECK NA KUWEKA YA HYDRAURIC NA SIO YA UMEME ILIYOKUWEPO, Nipe weledi ndugu yangu niepukane na vishoka japo wana majina makubwa kwenye garage zao.
 

Habari mkuu! Naomba kujua ni Engine oil yenye grade gani inafaa kwenye Toyota harrier ya mwaka 2003 Engine 2AZ-FE 2400cc inayotumia petrol na inatumika hapa dar es salaam,maana nimeona mkanganyiko sana wengine wanasema 10W40 wengine 5W30 wengine 20W50,tupe muongozo wako kitaalam.Natanguliza shukrani
 
Ina kilometa ngapi. kwani kuanzia mwaka 2003 sasa hivi ina umri wa miaka 17, lakini zaidi inategemea imeshetembea umbali gani. Kama bado iko chini ya KM 250,000 utatakiwa utumie 10W-30 tu, ila kama imeshazidi hapo basi unaweza kutumia 10W-40 au SAE40. Usitumie 20W-50 au SAE50 kwenye gari hilo kwa namna yoyote ile iwayo.
 
Swali lako sikulielewa vizrui, tafadhari tumia PM kusudi tuweze kueleweshana tatizo lenyewe kabla ya kutafuta ufumbuzi wake.
 

Imetembea kM 140000
 
Habari mkuu Kichuguu m nna ist c.c 1490 ni ya mwaka 2004 kuna kipindi nilifanya service nkaweka oil ya liquilmoly 5w-30 nkaenda moshi-dar kurudi oil ikawa imepungua sana yaan iko chini ya nusu baada ya kwenda kwa fundi akasema gari ina kilometer nyingi akabadil oil akaweka castorl 20w-50 then nkaenda dom-dar kurudi tatizo limejirudia tena oil imepungua sana shida inaweza kuwa nn??

Na je oil niliyitumia ni sahihi?? Nilimuuliza je shida inaweza kuwa piston ring akasema ingekua inatoa moshi na kupoteza nguvu....msaada hapo mkuu
 
Sio mara zote piston ring husababisha gari kukosanguvu katika piston ringi kuna kama shanga za aina tatu kuna moja inahusika na oil amachokwambia fundi kinaweza kuwa na ukweli
 
Oil ya mwanzo ya liquimoly ndio iliyokua sahihi hiyo ya 20w50 sio sahihi kwa gari hiyo na hapo kutakuana tatizo kubwa la kiufundi pengine Kuna leakage sehemu ambayo inapitisha oil, kwa gari hiyo oil inayoshauriwa kutumiwa ni 5w30, 10w30 na sio 20w50 hii ni oil nzito Sana
 
Salama Mdau. ndugu nijuze kwa kawaida gari ianatakiwa kufikisha KM ngapi mshale wa joto la njini kuwa kaiwada? maana gari yangu km 3 joto linafika kati kati kwa maana la kaiwada
 
Naomba kufahamu, ukiingiza used car kutoka japan, ni muhimu kufanya service zp? Na je unaweza kutumia oil ya gear box uliyoikuta na ukabadili ya engine tu?
 
Salama Mdau. ndugu nijuze kwa kawaida gari ianatakiwa kufikisha KM ngapi mshale wa joto la njini kuwa kaiwada? maana gari yangu km 3 joto linafika kati kati kwa maana la kaiwada
Mshale wa joto unategemea na aina ya maji unayotumia kama coolant na joto la nje la sehemu ulipo. Tumia coolant ambayo iko recommended (ya kijani au ya machungwa) na usijali umetembea umbali gani kabla mshale haujafika katikaki. Tatizo ni pale tu ambapo joto linapozidi kiwango hicho. Kwa mfano ukiwasha gari ukaliacha kwenye silence kwa muda kabla hujaanza safari unaweza kuanza safari yako wakati joto limeshapanda, lakini hiyo haimaaninishi tatizo lolote kwenye injini yako.
 
Naomba kufahamu, ukiingiza used car kutoka japan, ni muhimu kufanya service zp? Na je unaweza kutumia oil ya gear box uliyoikuta na ukabadili ya engine tu?
Unaponunua gari used, sheria kuu ni kufanya service zote kikamilifu. badilisha oil zote, yaani kwenye injini, gearbox an kwenye diff. Halafu badilisha coolant yote. Ila kama gari hiyo inatumia autotransimission unaweza kubadili ATF yote, lakini hapa inahitaji kuwa na mtu anayejua kufanya hivyo kwani ukikosea kubadili ATF basi utapeleka gari hilo kwenye jalala
 
asanre sana mkuu wa uzi mzuri
hakika una tusaidia sana.


mkuu naomba kuuliza.

gari yangu ni IST
kila nikiwasha kuna kama mswaki wa bluu unatokeza kwenye dash board na kujifuta baada kama ya dakika 3 hivi



hii alama ina maana gani ?





pili naweza aje kugundua kupitia dash board kua engine oil imepungua sana ili nibadilishe ?


asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…