Nimekuwa nafuatilia sana elimu unayotoa mdogo wangu for sure am inspired, mpaka nikajiuliza nilikuwa wapi kusomea mambo kama haya, ukweli you deserve to be a lecturer somewhere, umenitoa mbali kwa elimu ya magari nakufuatilia sana.
Anyway nahitaji elimu zaidi maana ndugu yako namiliki subaru forester, iliwahi kuingia maji nikafanya kosa la kuiwasha niitoe ikashindikana, kilichotokea niliomba breakdown ikaichukua mpaka 0-60 garage magwiji wa subaru wanasema hawatengenezi gari aina nyingine, baada ya kuchunguza mfumo wake ni wa umeme wakabaini control box na stering reck zimeungua, wakabadirisha, lakini haikuisha hata miezi minne kurudi service gari ilikuwa inagonga wakasema stering reck imeharibika na ina gharama nikawastukia kuna mmoja akasema ataifanyia engineering itaendelea kutumika nikaogopa, NIMEPATA MSHAURI HAPA NAKAZIA ILI UNISHAURI POA, ANANIAMBIA MAFUNDI WENGI HUWA HAWAPENDI KUSEMA UKWELI, NI KWAMBA HIZI GARI HUWA ZIKIINGIA ILI ZIDUMU WANABADILISHA STERING RECK NA KUWEKA YA HYDRAURIC NA SIO YA UMEME ILIYOKUWEPO, Nipe weledi ndugu yangu niepukane na vishoka japo wana majina makubwa kwenye garage zao.