Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
- Thread starter
- #521
Tatizo lako ni kwenye transmission tu, siyo tatizo la backlash kabisa; fundi alitakiwa akague hizo engine mounting kabla ya kuzibadilisha. Kwa vile siwezi kuikagua mwenyewe, ngoja nikuorodheshee list ya vitu vingine vinavyoweza kusababisha tatizo hilo.Mkuu leo nimebadili geat mount lkn bado mshindo upo palepale. Mshindo unatokea pale napotoka P kwenda R au R kwenda D au D kurudi R. Ila kutoka D au R kwenda P hakuna mshindo.
Mafundi wote waliopo hapa kila mtu anakisia, hakuna mwenye majibu.
Mwingine anasema nibadiki gear box niweke mpya, mwingine anasema drive shaft, mwingine anasema sijui diff imekufa.
Yani inanichanganya sana
(1) Je walipobadili ATF walipima vizuri bila kuweka zaidi au pungufu? na je walihakikisha kuwa hawaku-empty Torque Converter? Na vile vile je walibadili ile transmission oil filter pia?
(2) Je gari yako ina breki nzuri tu, na unapobadili gia kutoka P huwa umekanyaga breki kikamilifu? Kuna magari ambayo yametengezwa kuwa unapobadili gear kutoka au kuingia P lazima uwe umekamata breki kikamilifu
(3) Je gari ina silence nzuri? kama gari ina silence ya juu sana; zaidi ya 1500 rpm, transmission huhama kwa shida na unaweza kusikia inagonga hivyo
(4) vitu vingine nikikumbuka nitakuletea, lakini hivyo ndivyo vikubwa vinavyokuja haraka haraka kichwani mwangu.