Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Hi swali nilshalijibu huko nyuma; kuna mambo mengi yanayoweza kusababisha hali hiyo. soma post hii
Ashante Mr.Kichuguu,,,nimeiona na nimeelewa ,,, na vp kuhusu swala kwenye mafuta ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ashante Mr.Kichuguu,,,nimeiona na nimeelewa ,,, na vp kuhusu swala kwenye mafuta ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inakula sana mafuta kwa sababu kila mara unakuwa umekanyaga accelerator kupeleka mafuta ambayo mengine hayatumiki ndani ya injini bali yanapotea tu ili kuzuaia injini isizimike.
 
Sawa Mr. lakini swala la mafuta ilikuwa kabla ya ishu hiyo ya silence kiongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujatoa maelezo ya kutosha kwa mtu kuweza kukupa ushauri bila kukagua gari lako. Matatizo uliyoeleza kwenye post yako kuu yanashirikiana na yanakwenda pamoja; inawezekana dalili zilianzia kwenye ulaji wa mafuta kabla hazijafikia kufanya injini iwe inazimika. Ukifix sababu za injini kuzimika, utakuwa umetatua kwa kiasi kikubwa tatizo la ulaji wa mafuta pia.

Mambo mengine madogo madogo yanayoweza kusababisha gari kula mafuta sana ni pamoja na kutumia oil nzito sana kwa mfano SAE40 au SAE50; kuwa na breki zinazobana, injector zisizofanya vizuri, Kuwa na oxygen sensor zisizofanya vizuri, kuwa na fuel pressure regulatroisyofanya vizuri, kuwa spark plugs zisizofanya vizuri, na hata kuwa na matairi yasiyokuwa na upepo wa kutosha. Huwezi kuamini kuwa upepo wa matairi unachangia ulaji wa mafuta. Ukipata fundi akakagua hayo yote ataweza kukuambia ni kipi chenye matatizo.
 
Mkuu kuna gari nimepaki kwa miaka 2.Nataka kuifufua je ni mambo gani ya kuzingatia katika zoezi la kuifufua?
 
Mkuu Kichuguu gari yangu inachemsha ninapotembea kuanzia km tano,pili ninapowasha mshale wa RPM unaanzia kwenye 2000.Pia nahisi gari kukosa nguvu Hapa tatizo linaweza kuwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Kichuguu gari yangu haikamati hand brake..shida inaweza kuwa ni nini?
Ama hand brake shoes zimekwisha, hii hutokea hasa kama mara nyingi hujisahahuna kuendesha wakati hand brake ziko ON, au brake cable imekatika, au hand brake shoes zinahitaji adjustment tena.
 
Mkuu kuna gari nimepaki kwa miaka 2.Nataka kuifufua je ni mambo gani ya kuzingatia katika zoezi la kuifufua?
Kuna sehemu za bopdi zinaweza kuwa na kutu sasa, hayo unaweza kuyaona kwa macho tu.

Baada ya kukaa idle kwa muda mrefu, unapenda kukagua na kusafisha tanki la mafuta pamoja na njia yote ya mafuta, halafu mwaga oil yote usafishe lubrication system, nwaga coolant yote yote na kusafisha cooling system. Njia nzuri ya kusafisha kubrication system ni kuweka oili mpya nyepesi kidogo kama 5W-20 halafu uendeshe injini kwa kama saa tatu au nne hivi, kisha uimwage ndipo uweke oil stahiki, ambayo ni ama 5W-30 au 10W-30.
 
Natumia gari aina ya Vitz old model gari hii inatabia ya kuwasha taa nyekundu kuashiria kuwa tempreture ya gari iko juu pindi jua linapokuwa kari sana na hali hii inapelekea gari kukosa nguvu ama kuzima kabisa.

Ila pindi inapowasha taa ya kuashiria kuwa gari inachemsha huwa naangalia kama maji kwenye gari yapo na nakuta maji yapo na wala ule mvuke wa kuashiria gari inachemsha huwa haupo.

Na pindi taa ya kuashiria kuwa gari inachemsha ikiwa inawaka nikizima AC baada ya muda gari inatulia naombeni msaada juu ya hili maana nishaangaika sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina tatizo la kupasua radiator tank.

Ninanunua, linapasuka baada ya muda mfupi.

Nikaazimia niweke la aluminium.

Kuna jamaa wanauza radiators za aluminium, wanasema zinadumu sana.

Kwa utaalamu wako, unaonaje hilo wazo.

Nibadili hilo tank la plastic iweke la aluminium au niache hilo hilo?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Kichuguu gari yangu inachemsha ninapotembea kuanzia km tano,pili ninapowasha mshale wa RPM unaanzia kwenye 2000.Pia nahisi gari kukosa nguvu Hapa tatizo linaweza kuwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Injini nyingi zinaanza na RPM ya juu kama 2500 hivi halafu inatelemka kuwa kati ya 600 mpaka 1500 kulingana na gari lenyewe. Je hiyo 2000 ndiyo RPM ya silence au ndiyo ya kuanzia?

Kama gari inachemsha, ni lazima itakosa nguvu kwa sababu injini ikipata joto la kupita kiasi huwa inashindwa kuchoma mafuta kiasi kinachotakiwa.

Mwisho gari kuchemsha maana yake ni kuwa injini haipati maji ya kutosha kuipooza. Ama mfereji wa maji ya kupoozea una kutu na umeanza kuziba (kama huwa unaweka maji ya bomba), au water pump yako imekufa haizungushi maji kwenye injini, au radiator yenyewe imeziba haipitishi maji na kuyapoza. Mwambie fundi wako akukagulie Cooling system yote.

Halafu injini iki-overhaeat kwa muda mrefu huharibu vitu vingine vingi, hasa seals na gaskets
 
[QUOTE="Bavaria,

Sababu kubwa sana inayosababisha radiator kupasuka ni kuwa na pressure kubwa sana kuliko uwezo wake wa kuhimili. Sasa cooling system ya kawaida huwa haijengi pressure kiasi hicho, kwa hiyo pressure hiyo lazima itakuwa inatoka kwenye cylinders za injini yako, yaani ama kuna ufa kwenye clinder head unapopitisha pressure kutoka kwenye pistoni cylnders na kuipeleka kwenye cooling system, au cylinder head gasket imechoka inaruhusu pressure kutoka kwenye clinder kuingia kwenye cooling system.

Kwa hali hiyo pia utakuwa unapoteza maji sana kwenye cooling system yako, na vile vile engine oil itakuwa inaharibika mapema sana kwa kuchanganyika na maji. Mwisho zaidi ni kuwa injini itakuwa haina nguvu ya kutosha. Mwambie fundi wako akukagulia cylinder head na cylinder gasket vizuri.
 
Back
Top Bottom