Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Habarini wakuu.

Mi nahitaji kusaidiwa vitu vyoote muhimu kafika gari kwa ufupi na kwa uhakika zaidi...
Soma kitabu chake kinaonyesha matunzo yanayotakiwa. Ila matunzo ya jumla ni pamoja na kubadilisha oil (kati ya 5W-30 na 10w-30) na oil filter kila baada km 5000, na vile vile kubadilisha air cleaner kila baada ya kama km 10,000.

Hakikisha umeweka maji yanayotakiwa; kuna magari yanahitaji maji ya kijani, na kuna yanayohitaji maji ya manjano, soma kitabu chake. Vile vile hakikisha una mafuta ya breki ya kutosha; magari mengi hutumia DOT 3 lakini soma kitabu cha gari lako kujua lenyewe linatumia mafuta gani.

Badilisha mafuta ya transmission na filter yake kila baada ya km 50,000. Chagua fundi mzuri wa kuwa anakukagulia gari lako; siyo kila anayevaa overoli na nguo zenye mafutamafuta ni fundi. Sijui kama hayo maelezo yamekusaidia.
 
Mkuu Kichuguu, asante sana kwa somo zuri

Tatizo unatupa ushauri halafu tunakaa kimya bila kuleta mrejesho humu ili iwe msaa da kwa wengine

Please jamani, leteni mrejesho ili itusaidie nasisi wengine pleas!!!
 
Mkuu Kichuguu asante sana kwa uzi huu.

Nina Nissan X-Trail ya mwaka 2002, nliinunua kwa mzee mmoja hivi. Ni namba B ila kiukweli mzee aliitunza vizuri sana. Sasa nlipoichukua nadhani nlii-abuse(maji ya Dawassa n.k), nikaitumia kama miezi mitatu ikaanza kuchemsha, nikaipeleka kwa washkaji wa uchochoroni wakaichokonoa mara kadhaa mpaka nlipojua nimeua injini.

Nikaipaki kama mwezi nikijipanga, baadae nikaenda kwa Wapemba Ilala nikachukua injini used ya Japan. Baada ya kuifunga, silencer iko juu kiasi, yaani haiko sawa. Lakini pia kuna siku ilisumbua kuwaka asubuhi, nlipomwita fundi akanambia kuna shida kwenye throttle. Kuna kitu alifanya ikawaka na tangu hapo haijawahi kusumbua tena. Shida ni hiyo silencer..

Naweza kusaidikaje mkuu??
 
Mkuu Kichuguu asante sana kwa uzi huu.

Nina Nissan X-Trail ya mwaka 2002, nliinunua kwa mzee mmoja hivi. Ni namba B ila kiukweli mzee aliitunza vizuri sana. Sasa nlipoichukua nadhani nlii-abuse(maji ya Dawassa n.k), nikaitumia kama miezi mitatu ikaanza kuchemsha, nikaipeleka kwa washkaji wa uchochoroni wakaichokonoa mara kadhaa mpaka nlipojua nimeua injini...

Tatizo lako huenda ni idle air control valve; inaweza kuwa ina uchafu haijifungi sawasawa au adjustement yake imehama. Hilo ni tatizo dogo kwa fundi kurekebisha. Vinginevyo unaweza ukaweka mpya tu. Hizo zinagharimu kama dola 10 mpaka 20 hivi. Sehemu kubwa huwa zinachafuka na kuwa na masizi yanayofanya zisifunge vizuri, kwa hiyo fundi mzuri anaweza kukusafishia tu.
 
naomba kufaham gari aina ya passo na km yenye pistoni tatu au nne na changamoto zake kwa safari ndefu...

HOT
 
naomba kufaham gari aina ya passo na km yenye pistoni tatu au nne na changamoto zake kwa safari ndefu...

HOT
Ni vigumu kukujibu sawasawa bila kujua ukubwa wa pistoni zako; hata hivyo namba ya pistoni ikiwa namba tasa (ODD) huwa hazina balance nzuri, zinakuwa zinatikisika sana, hizi nyingi siyo kwa ajili ya shughli za muda mrefu, ni kwa mfano mashine za kufyeka nyasi na vitu kama hivyo. Injini nyingi kwenye magari yanyofanya safari ndefu huwa za namba shufwa (EVEN) ya piston
 
sawa mkuu vp kwa matumizi ya safari ndefu, maake naona speed zinasoma 180 na wanasema cc huwa ndogo km 900 ivi kwaiyo passo ni rahisi kuchoka au kuchemsha je ni kweli?

HOT
 
sawa mkuu vp kwa matumizi ya safari ndefu, maake naona speed zinasoma 180 na wanasema cc huwa ndogo km 900 ivi kwaiyo passo ni rahisi kuchoka au kuchemsha je ni kweli?

HOT
Itakwenda tu; hakuna tatizo lolote, ila kwa kiwango kikubwa utakuwa unabadilisha engine mounts mara kwa mara.
 
Tatizo lako huenda ni idle air control valve; inaweza kuwa ina uchafu haijifungi sawasawa au adjustement yake imehama. Hilo ni tatizo dogo kwa fundi kurekebisha. Vinginevyo unaweza ukaweka mpya tu. Hizo zinagharimu kama dola 10 mpaka 20 hivi. Sehemu kubwa huwa zinachafuka na kuwa na masizi yanayofanya zisifunge vizuri, kwa hiyo fundi mzuri anaweza kukusafishia tu.
Asante sana mkuu, je hiyo yaweza kuwa suluhisho la issue zote mbili?. Yaani silencer na hiyo ya throttle.
 
Habari Za kazi kiongozi
Unashauri vipi mtu akitaka kununua bmw min copper ya mwaka 2010 je ni nzuri au mbaya upande wa matengenezo au kuharibika


Sent using Jamii Forums mobile app

Hayo magari siyo maarufu sana hapa nilipo, kwa hiyo sina uzoefu nayo sana. Ila kwa hapa tulipo, matengezo ya magari ya Japan na Ulaya huwa ni ghali kutokana na bei za replacement parts zake. hali inawezekana siyo hivyo sehemu nyingine ya dunia
 
Ni vigumu kukujibu sawasawa bila kujua ukubwa wa pistoni zako; hata hivyo namba ya pistoni ikiwa namba tasa (ODD) huwa hazina balance nzuri, zinakuwa zinatikisika sana, hizi nyingi siyo kwa ajili ya shughli za muda mrefu, ni kwa mfano mashine za kufyeka nyasi na vitu kama hivyo. Injini nyingi kwenye magari yanyofanya safari ndefu huwa za namba shufwa (EVEN) ya piston
Fanya homework yako vizuri!!
Td5 ya landrober Ni 5 cylinders
1PZ ya land cruiser Ni 5 cylinders
OM617 Mercedes Ni 5 cylinders

Zote hizo ni gari heavy duty

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya homework yako vizuri!!
Td5 ya landrober Ni 5 cylinders
1PZ ya land cruiser Ni 5 cylinders
OM617 Mercedes Ni 5 cylinders

Zote hizo ni gari heavy duty

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee mimi nina license ya ufundi wa magari tena level ya Consultant na nimeshafanya ufundi wa magari kwa muda mrefu sana ingawaje kwa part time; usinitume kufanya homework yoyote.

Nilichosema hapo ni kuwa ODD number hazina balance nzuri na huua engine mounts haraka; ukitaka kujua sababu zake hilo ni jambo jingine.

Engine ulizotaja hapo juu most likely zote ni za diesel kwa sababu moja kuwa diesel engine huwa siyo high speed engines na ndizo engine nyingi zenye ODD number of inline cylinders kwa wakati huu.

Injini hizo siyo high speed kama za petroli na hivyo hata level ya vibrations ndani yake siyo ya kuleta madhara sana
 
Engine za magari makubwa tusiulize?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Engine za magari makubwa tusiulize?


Sent from my iPhone using JamiiForums
Probably siyo sana labda ziwe za petroli; niko zaidi kwenye hizi za magari madogomadogo. Kuna vitu naweza kujibu vizuri kwa kulinganisha na uzoefu wangu lakini inawezekana nisijibu kama ingekuwa ni zile injini ambazo huwa naweka mikono yangu mara kwa mara.
 
Chief, nina Noah New Model, juzi nmetoka nayo ilikuwa poa, ila nlipotembea kama 1 km ikawaka taa ya engine njano, alafu ikawa haina nguvu ukikanyaga mafuta, nkaizima nlipowasha taa ya engine iliendelea kuwa on ila ikawa ipo kawaida ukikanyaga mafuta, mpaka mda huu taa bado ya waka, Npatie ushauri Kiongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee mimi nina license ya ufundi wa magari tena level ya Consultant na nimeshafanya ufundi wa magari kwa muda mrefu sana ingawaje kwa part time; usinitume kufanya homework yoyote. Nilichosema hapo ni kuwa ODD number hazina balance nzuri na huua engine mounts haraka; ukitaka kujua sababu zake hilo ni jambo jingine...
Wataalamu wetu mkishaanza kuleta habari za vyeti vingapi mnamiliki sie akina karume kenge inabidi tukae kimya
Ishu sio vyeti ni knowledge tu , nilitegemea ungekuja na sababu za kunipinga kwa engine nilizokutajia hapo juu , ambazonni heavy duty na zina maisha marefu tu.

Ishu ya vibration haipo kwenye engine za odd cylider configuration pekee ipo hata kwenye hizi zenye namba shufwa , vibration ipo kwenye engine yoyote ambayo Ina cylinder chache lakini zilizokuwa enhanced kutoa nguvu nyingi, hii Ni kwa sababu kunakuwa na tofauti kubwa ya time kati ya pigo la cylinder moja na jingine, kwa kulijua Hilo huwa zinawekwa shaft balancers ili kupunguza vibration,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom