Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
- Thread starter
- #661
Soma kitabu chake kinaonyesha matunzo yanayotakiwa. Ila matunzo ya jumla ni pamoja na kubadilisha oil (kati ya 5W-30 na 10w-30) na oil filter kila baada km 5000, na vile vile kubadilisha air cleaner kila baada ya kama km 10,000.Habarini wakuu.
Mi nahitaji kusaidiwa vitu vyoote muhimu kafika gari kwa ufupi na kwa uhakika zaidi...
Hakikisha umeweka maji yanayotakiwa; kuna magari yanahitaji maji ya kijani, na kuna yanayohitaji maji ya manjano, soma kitabu chake. Vile vile hakikisha una mafuta ya breki ya kutosha; magari mengi hutumia DOT 3 lakini soma kitabu cha gari lako kujua lenyewe linatumia mafuta gani.
Badilisha mafuta ya transmission na filter yake kila baada ya km 50,000. Chagua fundi mzuri wa kuwa anakukagulia gari lako; siyo kila anayevaa overoli na nguo zenye mafutamafuta ni fundi. Sijui kama hayo maelezo yamekusaidia.