Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
- Thread starter
- #681
Umeniambia nifanye research-yaani maana yake ni kwamba sijui ninalozungumza, hukuja na comment wala kuuliza swali; halafu jibu langu hapo siyo kukuonyesha vyeti vya shule yangu bali nimesema nina leseni, yaani nimeidhinishwa na mamlaka za kiserikali kuwa nina ujuzi na uzoefu wa kutengeza magari ya watu binafsi. Sikuzungumzia utaalamu kutokana na "vyeti" ninavyomiliki, digrii nilizo nazo hazina uhusiano kabisa na magari kwa taarifa yako, na wala katika thread yote hii sijaingiza swala la taaluma yangu bali ninaongelea uzoefu wangu wa kutengeza magari tu. Kwa hiyo usijaribu kubadilisha topic kuwa ya taalumaWataalamu wetu mkishaanza kuleta habari za vyeti vingapi mnamiliki sie akina karume kenge inabidi tukae kimya.
Ishu sio vyeti ni knowledge tu , nilitegemea ungekuja na sababu za kunipinga kwa engine nilizokutajia hapo juu , ambazonni heavy duty na zina maisha marefu tu...
Nikirudi nyuma, katika introduction yangu nilieleza kuwa kuwa niulize chochote kuhusu injini za magari ya petroli; sikusema injini za dizeli au za umeme. Kila swali ninalijibu hapa nikijua linahusu injini za petroli; watu wote walioniuliza maswali yanayohusu injini za dizeli nimewajibu kuwa sina uzoefu nazo, ingawa ninaweza kuwa najua mambo kadhaa kuhusu injini hizo lakini sina uzoefu nazo na hivyo siwezi kutoa authoritative answer.
Usingenifundisha kufanya research, wewe ukauliza tu kuwa mbona kuna injini hizi zina ODD number ya cylinder, ningekujibu kabisa kuwa huenda hizo ni za dizeli au ni chache sana tena huenda ziko designed ama kwa ajili ya matumizi ya safari fupi fupi kama taxi. Nimeshashughulika na magari ya petroli kwa takribani miaka kumi na sita sasa na wala sijawahi ona gari ndogo yenye odd number ya cylinder; zilijaribiwa zamani lakini zikasitishwa.
Ziliopo chache ni mahsusi kwa magari maalum yasiyotegemewa kufanya safari ndefu za spidi kubwa kama zile zinazotengezwa maalumu kwa makampuni ya taxi. Hiyo ya huyo aliyeuliza swali hilo huenda ilikuwa kwa ajili ya taxi za Japan.