Oil mbaya hiyo kwa gari ndogo kama yako; unatakiwa utumie 10W30.
Ushauri mdogo kama unaweza kagua cylinder head gasket. Washa injini kwa muda ipate joto halafu fungua mfuniko wa oil; ukiwa na maziwamaziwa, basi suspect wako anakuwa ni cylinder head gasket. Ukishaona hivyo, chomoa waya zote za spark plugs, halafu fungua mfuniko wa radiator uache wazi mwambie mtu aingine kwenye kiti cha dereva apige ufunguo. Ukiona radiator inatoa mapovu, basi ujue Cylinder head gasket imeshaharabika, na hiyo inaweza kuwa ndiyo inasababisha matatizo yako yote. Usifungue radiator wakati injini ingali ya moto; maji yatakurukia usoni na kukuchoma. Inabidi uache injini ipoe kwanza kabla ya kuanza steji hii ya pili.
Jambo la pili, je huwa unatumia coolant au maji. Kama unatumia maji, huwa yanakwisha haraka sana na yanaweza kuweka kutu ndani ya injini ambayo itasababisha injini injini hiyo kuanza kuvuja.
Tatu: Angalia water pump; kama haisukumi maji kwenye mzunguko, maji hayo huweza kuchemka kupita kiasi na kuevaporate. Hali hiyo husababisha pia injini kuoverheat.
Ulaji wa oil unaosema ni wa kawaida kwa gari ya umri huo.