Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

@Kichuguu

Mrejesho wa tatizo nililoomba ushauri

Nilienda kwa mafundi wawili mmoja wa umeme na mwingine makenika na kuwaeleza na kuonyesha nilichoandika ktk uzi huu

Ushauri niliopewa kabla ya kuthibitisha suala la oil seals kwa pamoja waliona ni bora kwanza zisafishwe plugs zote kisha niitumie gari kwa japo siku tatu hk nikichunguza moshi kama utaendelea au laa. Zoezi hilo limefanyika leo, plug zilikuwa chafu sana na pia kua njia ya hewa (siijui vema kama ni sahihi maana nakiri si mtaalam wa mambo ya magari) nayo pia wakaisafisha ilikuwa chafu. Baada ya hapo vikafungwa vema kabisa

Matokeo niliyoyapata
1. Gari imekuwa nyepesi mnooo ktk kuongeza mwendo
2. Sijauona moshi kwa safari nilizofanya leo

Baada ya siku tatu, ntarudi tena kuwapa majibu japo niliambiwa kama tatizo litakuwa limeisha bhasi watafungua na tanki la mafuta walisafishe kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa gari
Kama gari inakula oil na kutoa moshi, usafishaji wa plugs na kusafisha mfumo wa hewa-ie throttle body, MAF sensor, max be airfilter hazitasaidia mkuu... Sanasana hapa kama gari inatumia electronic throttle body itafanya idling iwe juu ukisha safisha but with ECU relearning idle speed itarudi palepale kwenye required rang ya 700rpm na utaanza kuona tena tatizo linarudi.. kumbuka idle speed ikiwa juu inasabanisha injini kuwahi kufika kwenye operating temperature haraka(labda gsri iwe imetolewa thermostat) na hata pia ndo maana gari ikipaki injini ikapoa, ukiwasha lazima silencer iwe juu ili kufika kwenye joto la injini haraka;;so kwakua umesafisha throttle body now engine is revving high and attain operating temperature very fast hivo uwezi ona moshi kwakua piston rings zina expand fast because of heat na ku seal vizuri na kuficha tatizo lako.
 
Ist 4WD ina kipengele kipi?
Ni nzuri.. with 4wd itakua na traction nzuri kwenye barabara haitakua inakusumbua sana hata kwenye terrains za mchanga, tope, un even road surfaces.

Sema mafuta kidogo itakua juu kuliko 2 wheel drive,, pia zingatia kuchange differential oil ambayo usaharika sans
 
Niaje wakubwa.

Nimebadilisha feni inayopoza mashine ya gari... Ist cc 1290

Inafanya kazi vizuri na mashine haipandishi joto.

Wasiwasi wangu ni kuwa tulibahatisha bahatisha saana hadi kufikia kupata suluhu engine iache kuchemsha.. mara motor ndogo, mara panga za feni hazifai, mara feni ilikuwa inapuliza tofaut(iligeuzwa kinyume nyume).

Msaada ninaoomba ni huu.

Kuna utaratibu wowote wa kitaalamu unaoweza kutambua kuwa motor na feni hii ni sahihi kwa engine fulani??

Maaana nisije nikawa najisahau kumbe naua engine kimya kimya... Maana kuna time nikiwasha AC kidogo tu.. mngurumo mkuuubwa afu unakata.

Msaada bandugu
 
Then.... Kwenye suala la oil za gari zenye mileage 50,000 to laki. Ukiacha hizi 5 au 10. W 30. Kuna kingine cha kuzingatia kwenye aina ya kampuni za oil maana zimekuwa nyingi saana na bei tofaut ila zoote number sawa tu.

Nisaidieni kampuni bora angalau... Ukiachana na ile ya toyota yenyewe...ya kopo la bati.!?
 
Pia... Nlikuwa naomba ushauri wenu nyie wataalamu mnaotusaidia humu ndani kwenye masuala ya magari.

Ni gereji gani hapa bongo ina weledi wa utendaji wa hizi kazi, maana madini yenu tunaishia kuyasoma tukienda practical tunafanyiwa vitu vya kijinga kwenye magari na kuingizwa gharama zisizo za msingi!

Tupeni connection hata angalau tu wapi tunaweza tukafanya service bora kwa gharamu nafuu
 
Nimeamua nipost picha kwanza.
Mwaka jana nilienda kuiosha gari pamoja na engine.bahati nzuri ilikuwa siku ya mvua kunyesha kufunga vioo na kuwasha AC ikawa naona gari haina raha niliyoizoea.
Kesho yake asubuhi nikaenda nayo umbali wa km 2.gari ikaheat balaa kuangalia maji yameisha.nikaongeza.oil ikawa inepungua imebaki kama lt 1 tu.nikafanya service kabla ya wakati.
Baada ya hapo gari ikawa bado haieleweki eleweki,nikampa fundi akadai feni ipo sawa,kwa vile nikiendesha baada ya muda naona joto linapanda na maji yanapungua.
Fundi mwengine aliiona kile kibomba akaunga direct yaani maji yanazunguka yenyewe yennyewe bila kurudishwa kwenye rejeta lakini thermostart aliitoa.kipindi hiki akanielewesha kuwa sitopata AC ya ubaridi.tukaenda mjini kuvitafuta na kuchongewa vya shaba.kwa kipindi hiko nilihangaika na engine kila siku na ukiiwasha dk chache mafundi husema ipo sawa kumbe zikizidi dk 10 ndio unaona maruwe ruwe.nashukuru Mungu nilikuwa na masafa mafupi fupi.hivyo nikawa naona kama kuna ushirikina hivi.nalalamika gari haipo sawa mafundi wakiona maji ya rejeta yanapungua baada ya muda wakawa hajui yanatokea wapi.na gari ilikuwa mpya wakawa wanasema ipo sawa.
Mwisho hata baada ya kubadilisha hicho kichuma niliona bado haipo sawa kwa vile ile overheat ilikuwa ni oil imekauka na maji hakuna hivyo nilifanya hiyo engine ovalhall.bado siifurahii engine mpaka leo.naona wengi mnashauri engine kununua na nikitafakari naona ni bora kununua kuliko kubuni kutafuta tatizo.
IMG_20201231_184456_825.jpg
 
Kwa nn usifanye car dignosis kubaini tatizo ,achana na mambo ya ramli mbona life is easy kaka matafute mwamba anaitwa@jitu la miraba minne

sent from HUAWEI
 
Usishangae kuhusu utambulisho huu. Mimi sasa ni ASE Certified Service Consultant wa magari madogo yanayotumia petroli hasa ya Ford, GM, na Chrysler.

Nimepata license yangu hivi majuzi tu mwaka huu baada ya kuitafuta kwa muda kidogo through part-time activities kwani hiyo siyo kazi yangu kuu.

Certification hiyo inahitaji siyo tu kufaulu mtihani wake, lakini pia uwe na uzoefu wa kutosha kwenye auto-repair shop.

Nimekamilisha experience hiyo inayotakiwa mwaka huu na kupata license yangu.

Kwa vile injini nyingi za petroli zinafanana katika utendaji, jisikie free kuniuliza swali lolote kuhusu matatizo ya injini ya gari yako model yoyote inayotumia mafuta ya petroli.

Siahidi kuwa majibu yangu yote yatakuwa ni sahihi, lakini sehemu kubwa itakuwa ni sahihi, na hata yale ambayo hayatakuwa sahihi yanaweza kukusadia kujua wapi pa kuanzia.
Nina maswali mawili kuhusu Gari aina ya Grande Mark 2 (GX110)
1- Naomba kujua kiwango sahihi cha Engine Oil na Gearbox Oil kinachotakiwa.
2- Kwenye Dashboard hasa gari ikitembea muda mrefu na ikipata joto sana inaonyesha taa ya Check Engine hata kwa nusu saa na kuna muda itazima, kuna fundi nilishawahi mpk anipimie akasema ni VVT-i Sensor, akaitoa akaisafisha lakini tatizo lipo pale pale sikutaka kuhangaika tena.
 
Kama injini yako ni 1G - fe cc1988 kiwango chake ni 3.8 lita.

Gearbox ni 6.9 kama utaitoa yote na inatumia type four.

Pia kuhusu hiyo taa ya check injin ilishawahibnisumbua sana nilikuwa na gx 100 cresta ila nikaja kugundua baadae boya la umeme ndo lilikuwa halikai vizur, ila kwa ww kama boya lipo vizuri kanunue VVT- I SENSOR nyingine uweke, hyo sensor ikiwa haifanyi kazi vizuri ulaji wa mafuta huwa unaongezeka sana tu, utaichukia gari bure tu.
 
Sawa Mkuu nimekupata vizuri ngoja nifanyie kazi, ila kwenye Gearbox kumbe mimi huwa nakosea ninaponunua lile kopo la lita4 tu linalouzwa 120,000 huwa naishia hapo tu kumbe inatakiwa atleast ninunue makopo mawili!? Kisha nibakishe lita1 tu eti!?
 
Boya la kwenye Tank la mafuta au!? Na kuna muda inatembea ikiwa smooth halafu muda mwingine inakuwa kama inazuiwa hivi halafu inakuwa laini tena sijui nini kinazuiaga, mwanzo nilijua labda fuel pump ni mbovu lkn hata nilipobadilisha bado tatizo lipo pale pale inakuwa laini halafu kuna muda inakuwa kama inazuiwa flani
 
Kama utaitoa yote kabisa kwenye gear box, ila kama utamwaga tu kwa kufungua kawaida tu inayotoka huwa ni 60% na 40% huwa inabaki kwenye gear box, hapo unaweza kuweka lita 3.5 au 4
 
Boya la kwenye Tank la mafuta au!? Na kuna muda inatembea ikiwa smooth halafu muda mwingine inakuwa kama inazuiwa hivi halafu inakuwa laini tena sijui nini kinazuiaga, mwanzo nilijua labda fuel pump ni mbovu lkn hata nilipobadilisha bado tatizo lipo pale pale inakuwa laini halafu kuna muda inakuwa kama inazuiwa flani
Kwa hapo naomba ukaipime ndo utapata ufumbuzi rahisi na wa uhakika bila kuingia gharama za kununua spare zisizo na ulazima
 
Nina maswali mawili kuhusu Gari aina ya Grande Mark 2 (GX110)
1- Naomba kujua kiwango sahihi cha Engine Oil na Gearbox Oil kinachotakiwa.
2- Kwenye Dashboard hasa gari ikitembea muda mrefu na ikipata joto sana inaonyesha taa ya Check Engine hata kwa nusu saa na kuna muda itazima, kuna fundi nilishawahi mpk anipimie akasema ni VVT-i Sensor, akaitoa akaisafisha lakini tatizo lipo pale pale sikutaka kuhangaika tena.
Engine oil ni lazima iwe 10-W30; gearbox ni mannual au atomatic? Kuhuzu taa kuwaka, mpaka tupime gari tuone ni tatizo gani, lakini kwa magari ya zamani kidogo unaweza kukuta ni catalytic converter ndiyo imeanza kuchoka, kwa hiyo ikipata joto inashindwa kufanya kazi sawasawa. hata hivyo ni lazima gari ipimwe kwenye computer ndipo jibu sahihi lipatikane.
 
Automatic Mkuu
 
Automatic Mkuu
Kama ni Automatic, ukivuta ile dipstick ya oil yake, utakuta imeandikwa aina ya oil ya kutumia. Toyota nyingi huyumia Type T lakini soma iliyondikwa kwenye dipstick yako.
 
Back
Top Bottom