new generation
JF-Expert Member
- Mar 14, 2012
- 817
- 1,687
Kama gari inakula oil na kutoa moshi, usafishaji wa plugs na kusafisha mfumo wa hewa-ie throttle body, MAF sensor, max be airfilter hazitasaidia mkuu... Sanasana hapa kama gari inatumia electronic throttle body itafanya idling iwe juu ukisha safisha but with ECU relearning idle speed itarudi palepale kwenye required rang ya 700rpm na utaanza kuona tena tatizo linarudi.. kumbuka idle speed ikiwa juu inasabanisha injini kuwahi kufika kwenye operating temperature haraka(labda gsri iwe imetolewa thermostat) na hata pia ndo maana gari ikipaki injini ikapoa, ukiwasha lazima silencer iwe juu ili kufika kwenye joto la injini haraka;;so kwakua umesafisha throttle body now engine is revving high and attain operating temperature very fast hivo uwezi ona moshi kwakua piston rings zina expand fast because of heat na ku seal vizuri na kuficha tatizo lako.@Kichuguu
Mrejesho wa tatizo nililoomba ushauri
Nilienda kwa mafundi wawili mmoja wa umeme na mwingine makenika na kuwaeleza na kuonyesha nilichoandika ktk uzi huu
Ushauri niliopewa kabla ya kuthibitisha suala la oil seals kwa pamoja waliona ni bora kwanza zisafishwe plugs zote kisha niitumie gari kwa japo siku tatu hk nikichunguza moshi kama utaendelea au laa. Zoezi hilo limefanyika leo, plug zilikuwa chafu sana na pia kua njia ya hewa (siijui vema kama ni sahihi maana nakiri si mtaalam wa mambo ya magari) nayo pia wakaisafisha ilikuwa chafu. Baada ya hapo vikafungwa vema kabisa
Matokeo niliyoyapata
1. Gari imekuwa nyepesi mnooo ktk kuongeza mwendo
2. Sijauona moshi kwa safari nilizofanya leo
Baada ya siku tatu, ntarudi tena kuwapa majibu japo niliambiwa kama tatizo litakuwa limeisha bhasi watafungua na tanki la mafuta walisafishe kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa gari