Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Wakuu Habari yenu, mm gari yangu inashida ya kuwaka, ukiwasha at the first time inagoma then ukipiga starter second time inakubali, nilisafisha tank lilikuwachafu ila sikubadili pamp pia coolant inaisha haraka, nilibadili top cover lakin naona bado....

Msaada wenu tafadhali natanguliza shukrani
Jaribu kubadili fuel pump pia ili system ya mafuta isiwe na kasoro. Coolant kuisha inatakiwa uangalie kunaeza kua na leakage kwenye radiator au gari ina-heat sana ko kupelekea coolant kuisha. Peleka kwa mafundi wataweza kung'amua tatizo.
 
Wakuu Habari yenu, mm gari yangu inashida ya kuwaka, ukiwasha at the first time inagoma then ukipiga starter second time inakubali, nilisafisha tank lilikuwachafu ila sikubadili pamp pia coolant inaisha haraka, nilibadili top cover lakin naona bado....

Msaada wenu tafadhali natanguliza shukrani
Inatoa moshi?
 
Mkuu kichuguu, naomba kuuliza

Mfano gari iliwekwa engine oil ile namba 40 na imetembea zaid ya km laki 2, je kuna tatizo lolote kwa sasa nikitumia 5W30 ?

Gari husika ni Carina Ti.
Km laki 2 ni nyingi sana ukisema urud kwenye 5w30 naona Kama unaenda kuiua engine angalau angalau tumia 15w40, 10w40 au 5w40
 
Habari zenu wakuu, nina gari yangu Toyota will VS 2ZZ engine type, hii gari bwana nliipaki mwaka wa 3 sasa ikiwa na shida ya Timing chain, Kuzima zima na gearbox, ikifika gear namba 3 inavuma halafu haihami tena, mwezi uliopita nliitengeneza kwa hasira baada ya wezi kuiba kioo changu, fundi aligusa engine tu hakugusa gearbox akanambia gearbox nibadilishe au niende kwa fundi wa gearbox, ile gari baada ya kuitoa pale nikaitembeza inaingia gear zote hadi namba 5, nineshanga mpaka leo shida ya gearbox siipati natumia tu, nkimuuliza fundi anasema hajagusa gearbox kabisa. Sasa swali langu ni kutaka ushauri kutoka kwenu (kwa wataalamu wote) je niipeleke kwa fundi wa gearbox au niiache tu nitumie mpaka itakaponifia tena gearbox?
 
Tumia hiyo gari, ikileta shida utapeleka tena kwa fundi
 
Nina gari aina ya Allion 1.8 inatoa upepo sana (compression) hadi nikifungua mfuniko wa oil au dip stick inakuwa kama inazima.
Nunua injini nyingine... Hiyo inaitwa blow by... Blow by ikisha kua kubwa kama yako maana yake you have excessive compression loss kutia kwenye either valves, piston rings zilizo choka au cylinder walls zilizotanuka so rings are no long covering walls..... Ingawa hii changamoto waweza ongeza thickness ya oil (sae 40) unayotumia ikakusogeza ingawa kwa stage injini yako iliyopo hata oil itakua inakula sana.. waweza fanya overhaul but ni better ukanunua new injini...

Kumbuka unachokipitia ni midhara ya kutofanya oil change kwa wakati na kutumia oil low quality.. pole sana
 
Shukurani sana mkuu kwa maelezo mujarabu nitafanyia kazi ushauri wako. Japo hii engine nimeifunga haina hata miezi mitatu.

Mafundi wa chini ya Miembe ndo walinambia oil niliyokuwa nimeweka sio sahihi (SAE 40) niweke 5W-30 hapo ni baada ya taa ya oil kuwaka.

Nilipoweka na bado tatizo likawa palepale la taa ya oil kuwaka na ikaongezeka ya check engine, wakafungua wakasema mkono umeshika (Piston No. 2) so inabidi shaft ichongwe iwe size 25 na kununua cone na vikolokolo vingine.

Baada ya kufanha yote hayo ndo likaja hili la compression.

Nikinunua mswaki utafaa?
 
Mkuu, taa ya oil ikiwaka maana yake oil pressure kwenye gari yako ni ndogo... Chanzo ni oil pump kua na shida, au oil pick up tube ina shida/imeziba au gari imewekewa oil nzito kiasi kwamba pump inashindwa kuvuta na kuipandisha juu ya injini so oil pressure inakua below standard na kufanya taa ya oil pressure iwake. Kumbuka matumizi ya hizi oil nzito huu gari bila wewe kujua..mfano mono-grade mineral oil ya SAE40, mullti grade oil yenye viscosity ya 20w-50 hizi oil ni nzito so hazifiki kwa wakati sehemu mbalimbali zenye moving parts.so injini inakua mdogomdogo inakufa hasa pale unapoiwasha asubuh.

Kuhusiana na hiyo injini uliofunga watakua wamekuwekea injini mbovu.. yenye compression ndogo ndo maana blow by mi kubwa. (Ukitoa deep stick au oil cap ukaona oil inaruka sana nje wakati mwingine kunakua na ka moshi, injini inakuambia bye bye.... Kwamba compression inakua ndogo.... Na kwakua compression ndo hufanya injini kuwaka so low compression huwafanya gari kuwaka kwa tabu sana hasa injini inapokua ya baridi na hata ikiwaka injini inakua na mis kubwa, but hii misfiring hupotea taratibu injini ikisha fika operating temperature kwakua piston hu expand na kufanya zijae vizuri kwenye cylinder bore.. pia kama umeweka oil thick compression huongezeka na kufanya gari iweze angalau kuwaka japo kwa tabu..

Solution ni nunua injini mswaki nenda kanunue ilala usiende tandare... Wakupatie na warrant ya muda ili ujiridhishe injini ipo sawa haitoi moshi, haili oil, wala head gasket haivujishi maji kwenda kwenye combustion chamber, na ukiweka hiyo injini kama unaweza pima kabisa compression yake..
 
Ahsante kwa mara nyingine mkuu, nilibadilisha hadi oil pump ila bado.

Kwa sababu nimeagiza gari nyinhine inaingia week ijayo, hii Allion nataka niisukume kwa bei yoyote mtu akanunue mswaki tu.
 
Mkuu umemweleza vizuri sana, nakumbuka gari yangu inayotakiwa kutumia 5w30 au 10w30 niliweka 5w40. Aisee, kwanza gari ilianza kuwa nzito kidogo, baadaye kama mwezi mmoja au miwili ikaanza kuwasha taa ya oil kila asubuhi. Nilivobadilisha oil kurudi kwenye 5w30 naona gari ipo poa kabisa,
 
Kiukweli sasa hivi oil zimekua nyingi sana mtaani, na hii yote inasababishwa na soko huru lililopo hapa nchini na uepesi wa kuagiza mzigo nje ya nchi hasa Dubai, na kwa kuzingatia uepesi wa Bei unaopendwa na watumiaji wengi wa magari hapa nchini imesababisha hata waagizaji wa oil nao kununua masokoni kile Cha unafuu kuja kuuza bila kuangalia ubora wa oil iliyotengenezwa, sasa Kama muuzaji wa oil ambae Nina miaka 3 hivi sasa na kwa ushauri wangu, ukiachana na oil zinazotengenezwa na watengenezaji wenyewe wa magari mfano Toyota, Nissan,BMW Benz nk zifuatazo ni kampuni angalau zenye oil nzuri na zilizokidhi ubora wa kimataifa wa kutumika kwenye magari yoyote na usipate shida, nitataja kuanzia ya Kwanza kwa ubora
01 liquil Molly made from German
02 Castrol oil made from United kingdom
03 Mobil 1 oil from American
04Total oil made from France
05puma oil from puma company made in UK
06 Oryx oil from Swiss
07 Atlantic oil from California hivyo ukitaka gari yako ilindwe na angalau ukae nae mda mrefu jaribu kutumia vilainishi kutoka miongoni mwa kampuni zilizopo hapo juu. Tahadhari huo ni ushauri tu na maamuzi ya kuilinda gari au mtambo wako uko mikononi mwako na usisahau kwenye products ukikutana na msemo huu "the higher the price the higher the product". Hizo zote Bei yake imesimama kidogo
Ushauri wa oil sahihi kwa gari yako +255719263074 Mikocheni shoppers dsm
Katika hiyo orodha nimetumia liquimoly, Castro, total na Oryx. Kwa upande wangu kwa hizo tatu Liquimoly ya German is the best na sitaacha kuitumia, japo ni gharama sana lkn gari langu linakuwa very smooth just like new nikiweka Liquimoly.
 
Ahsante kwa mara nyingine mkuu, nilibadilisha hadi oil pump ila bado.

Kwa sababu nimeagiza gari nyinhine inaingia week ijayo, hii Allion nataka niisukume kwa bei yoyote mtu akanunue mswaki tu.

Ukiwa unauza tuonane mkuu
 
Habari zenu wakuu, nina gari yangu Toyota will VS 2ZZ engine type, hii gari bwana nliipaki mwaka wa 3 sasa ikiwa na shida ya Timing chain, Kuzima zima na gearbox, ikifika gear namba 3 inavuma halafu haihami tena, mwezi uliopita nliitengeneza kwa hasira baada ya wezi kuiba kioo changu, fundi aligusa engine tu hakugusa gearbox akanambia gearbox nibadilishe au niende kwa fundi wa gearbox, ile gari baada ya kuitoa pale nikaitembeza inaingia gear zote hadi namba 5, nineshanga mpaka leo shida ya gearbox siipati natumia tu, nkimuuliza fundi anasema hajagusa gearbox kabisa. Sasa swali langu ni kutaka ushauri kutoka kwenu (kwa wataalamu wote) je niipeleke kwa fundi wa gearbox au niiache tu nitumie mpaka itakaponifia tena gearbox?
Hiyo gari ilikuwa na shida ya engine na siyo shida ya Gearbox... Niamini mimi.

Gari nyingi auto Gearbox inaitegemea engine kwenye baadhi ya vitu.

Probably kuna tatizo lilitokea mwanzo ambalo lilipelekea gari yako kutrigger Limp mode, na ndio hicho ulichokuwa unaexperience kwa gari kuishia third gear.
 
Mkuu, taa ya oil ikiwaka maana yake oil pressure kwenye gari yako ni ndogo... Chanzo ni oil pump kua na shida, au oil pick up tube ina shida/imeziba au gari imewekewa oil nzito kiasi kwamba pump inashindwa kuvuta na kuipandisha juu ya injini so oil pressure inakua below standard na kufanya taa ya oil pressure iwake. Kumbuka matumizi ya hizi oil nzito huu gari bila wewe kujua..mfano mono-grade mineral oil ya SAE40, mullti grade oil yenye viscosity ya 20w-50 hizi oil ni nzito so hazifiki kwa wakati sehemu mbalimbali zenye moving parts.so injini inakua mdogomdogo inakufa hasa pale unapoiwasha asubuh.

Kuhusiana na hiyo injini uliofunga watakua wamekuwekea injini mbovu.. yenye compression ndogo ndo maana blow by mi kubwa. (Ukitoa deep stick au oil cap ukaona oil inaruka sana nje wakati mwingine kunakua na ka moshi, injini inakuambia bye bye.... Kwamba compression inakua ndogo.... Na kwakua compression ndo hufanya injini kuwaka so low compression huwafanya gari kuwaka kwa tabu sana hasa injini inapokua ya baridi na hata ikiwaka injini inakua na mis kubwa, but hii misfiring hupotea taratibu injini ikisha fika operating temperature kwakua piston hu expand na kufanya zijae vizuri kwenye cylinder bore.. pia kama umeweka oil thick compression huongezeka na kufanya gari iweze angalau kuwaka japo kwa tabu..

Solution ni nunua injini mswaki nenda kanunue ilala usiende tandare... Wakupatie na warrant ya muda ili ujiridhishe injini ipo sawa haitoi moshi, haili oil, wala head gasket haivujishi maji kwenda kwenye combustion chamber, na ukiweka hiyo injini kama unaweza pima kabisa compression yake..
Hapana; sehemu fulani ya jibu hili siyo sahihi tosha ila kwa kiasi fulani tu. Ni kweli kuwa oil pump ikichoka, oil pressure itapungua pia, ila siyo kawaida ya oil pump kufa kwani nyingi ni za aina ya gear pump ambazo kufa kwake ni labda gasket au oil seal kuchoka tu, ambayo inaweza kubadilishwa, na huwa haitokei kirahisi sana- ni less than 10% chance kupata tatizo kama hili. Taa ya oil pressure mara nyingi huashiria mojawapo kati ya mambo mawili: ama engine haina oil ya kutosha (more than 45% chance) au oil pressure sensor imekufa ( more than 45% chance). Oil pump ikifa, kuna dalili nyingine zitajionyesha zaidi ya taa kuwaka tu; kwa mfano injini itaana kuwa inapiga makelele sana na inakuwa ni ngumu sana kustart. Vile vile inakuwa inachemsha sana hata kama ina maji ya kutosha.
 
Kwa kuongeza.. Kuna baadhi ya gari zina taa rangi mbili tofauti.. Kuna ya njano na nyekundu.. Njano inawaka kama oil pressure ni ndogo..kama uliyosema most likely ni sensor.. Nyekundu kama oil level ipo chini..!
 
Wakuu Habari yenu, mm gari yangu inashida ya kuwaka, ukiwasha at the first time inagoma then ukipiga starter second time inakubali, nilisafisha tank lilikuwachafu ila sikubadili pamp pia coolant inaisha haraka, nilibadili top cover lakin naona bado....

Msaada wenu tafadhali natanguliza shukrani
Hiyo ni dalili ya injini kuchoka.... That engine has low compression ndo maana inashindwa wak vizuri pindi injinii inapokua cold, pia hali hii hata oil itakua inalika sana, itakua ni big blow-by problem.
 
Back
Top Bottom