Habari zenu wakuu, nina gari yangu Toyota will VS 2ZZ engine type, hii gari bwana nliipaki mwaka wa 3 sasa ikiwa na shida ya Timing chain, Kuzima zima na gearbox, ikifika gear namba 3 inavuma halafu haihami tena, mwezi uliopita nliitengeneza kwa hasira baada ya wezi kuiba kioo changu, fundi aligusa engine tu hakugusa gearbox akanambia gearbox nibadilishe au niende kwa fundi wa gearbox, ile gari baada ya kuitoa pale nikaitembeza inaingia gear zote hadi namba 5, nineshanga mpaka leo shida ya gearbox siipati natumia tu, nkimuuliza fundi anasema hajagusa gearbox kabisa. Sasa swali langu ni kutaka ushauri kutoka kwenu (kwa wataalamu wote) je niipeleke kwa fundi wa gearbox au niiache tu nitumie mpaka itakaponifia tena gearbox?