Niulize chochote kuhusu Kalynda E-commerce

Niulize chochote kuhusu Kalynda E-commerce

Status
Not open for further replies.
Nimeanza na mtaji wa laki 1 lakin hadi sasa nishapata faida ya kutosha!! Sio lazma usichokiamini wewe basi kila mtu asikiamini.... mimi binafsi sipendi siasa lakin kuna watu wamefanikiwa.... Fuata moyo wako na usiforce kulazimisha wengi waone upo sahihi ...
Mkuu mbona hueleweki?,mara ya kwanza umesema ulianza na laki 2 sasa hivi tena unasema umeanza na mtaji wa laki,tushike lipi tuache lipi?
 
Kama nikupigwa ngoja nipigwe tu, leo siku ya 3 nimejiunga kwa 20,000/=.

Ngoja nivute upepo hadi siku 15 au 20 nitoe hiyo commision. Maana kuna jamaa alinishawishi siku nyingi sana nikawa nachomoa. Yeye alishatoa karibia 35K.
 
Mkuu mbona hueleweki?,mara ya kwanza umesema ulianza na laki 2 sasa hivi tena unasema umeanza na mtaji wa laki,tushike lipi tuache lipi?

Soma vizuri thread... afu mimi nikuongopee wewe nakujua au ili nipate faida gani... kama haupo interested unaweza kuacha... Sipo hapa kwa ajili ya kukulazimisha au kumlazimisha yoyote... pesa ni zako na wewe pekee ndo mwenye uchungu nazo!!
 
Mhariri , Moderator na JamiiForums dhibiti Ponzi schemes na Pyramid scheme kama hizi zinazotangazwa humu na kuifanya jF kuwa salama.

Ngoja waje Kudhibiti.... unadhani chuki zako zinaweza kuzaa matunda??!... Mlimpigia kura Diamond asipate BET kisa tu ni kada wa CCM... Roho za watanzania wengi zimejaa chuki na kuona watu wanaothubutu wamefeli!
 
WABONGO BHANA ...MTU ANAKUTUKANA HAPA AFU ANAKUFUATA PM AU WHATSAPP .... NAOMBA KUJUA KUHUSU KALYNDA!! DAH... ILA CUSTOMER CARE NI KAZI SANA!
 
Ni matumaini yangu wote wazima. Mimi ni kijana wa kiume nimesoma diploma ya procurement and logistic management na bachelor degree ya business management, natafuta ajira nipo tayari kufanya kazi mkoa wowote
 
First,you need to register as an intern of Kalynda company, the company will give you 1,000 TZS registration bonus and 50,000 TZS experience bonus that will give you a commission of 1988 within 5 days!
Hii ikoje
 
WATANZANIA wamefika mahali wameshatapeliwa mpaka wakachanganyikiwa, makampuni haya yanakujaga vizuri na documents Safi kabisa Ila Sasa the future is not promising to the extent watu wanahisi serikali inahusika katika hili.
JATU walijisajiri mpaka DSE lakini kinachowakuta watu Leo ni maumivu tu.
Kuna utitiri wa haya makampuni kuanzia DECI,MR KUKU,VANILLA VILLAGE, SUNGURA VILLAGE, NAMAINGO,D9, N.K
 
Watu awaogopi mkuu MTU anaweka laki mbili

Laki mbili mbna pesa ya kawaida sana!!
031c7c16-0727-4257-aac0-5d628b266673.jpg
 
Watu awaogopi mkuu MTU anaweka laki mbili

Wewe una chembechembe za umaskini ... kams unaogopa kuweka laki 2 Kalynda utaweza kula bata la mamilion wewe;; laki 2 ni kitu kidogo sana kwenye uwekezaji;; tena usiongee mbele za watu
 
Pyramid schemes hizi sijui watu watajifunza lini...

Muda si muda hawa nao watakuja kulia kama hawa. It is only a matter of time...

 
Eti Kylanda nini?

Wacha hyo wewe utapigwaaaa!!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kampuni haiuzi cho chote. Ukiuliza mnazalishaje hizo pesa wakati wala hamuwekezi hakuna jibu. Hela zinajizalisha tu kama chuma ulete. Ni typical pure ponzi/pyramid scheme. Wale wa mwanzo mwanzo na chambo wengine wachache ndo wanalambishwa vitone vya asali ili wakawalete makondoo wengine wengi zaidi. Jamaa wakiona mzigo umetosha hao wanasepa.

Na hawa wanalindwa na vigogo maana utapeli ni ule ule lakini Brela bado wanatoa leseni. Ukifuatilia utakuta bosi wa hii ni kibopa huko serikalini au mtoto wa kigogo fulani.
 
Kuna kitu wengine sijui ndo wanaitaga iner voice,jambo lolote lenye kunipa kigugumizi huwa nasikia kabisa ndani ya moyo naambiwa acha au fanya kwakweli huwa sidharau.
kuhusu hiyo Kalynder nafsi yangu imekataa katakata sitojaribu ingawa kaka yangu ni mmoja wapo anafanya hii kitu lakini kwa mimi hapana.acha yeye na wengine wawe mabilionea kirahisi rahisi tu mimi ntakua mfanyakazi wao wa kuosha hayo mavieti watakayonunua.
 
Kuna kitu wengine sijui ndo wanaitaga iner voice,jambo lolote lenye kunipa kigugumizi huwa nasikia kabisa ndani ya moyo naambiwa acha au fanya kwakweli huwa sidharau.
kuhusu hiyo Kalynder nafsi yangu imekataa katakata sitojaribu ingawa kaka yangu ni mmoja wapo anafanya hii kitu lakini kwa mimi hapana.acha yeye na wengine wawe mabilionea kirahisi rahisi tu mimi ntakua mfanyakazi wao wa kuosha hayo mavieti watakayonunua.
Kabsa mkuu
 
Yaani mimi nafsi inakuja halafu inakata nimekuwa hoves sijuwi nifanye nini aisee.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom