Niulize chochote kuhusu Nyuki na Asali

Niulize chochote kuhusu Nyuki na Asali

Tunatundika MIZINGA sio MASEGA.
Ukitaka kufuga nyuki lazima uwe na yafuatayo.
1. Eneo la kufugia, maana yake eneo lenye miti inayotoa maua.
2. Liwe linafikika kirahisi.
Liwe na chanzo cha maji si zaidi ya kilometa 5, yakiwa hapo kwenye eneo ni bora zaidi.
3. Uwe na mizinga,
4. Eneo liwe mbali kidogo na makazi ya watu, kwa kuwa nyuki wetu wa Afrika kila mtu anawajua.
5. Upate elimu kidogo ya ufugaji.
Ndio hio Mizinga, neno lilinitoka na nkatumia masega tu 😀

Okay, mfano mimi shamba nnalo, linafikika kirahisi tu na chanzo cha maji kipo chini ya 5KM.

Mimi kinachonitatiza ni hawa nyuki, huwa wanatokea wapi wenyewe ikiwa eneo husika hakujawahi kuwa na nyuki ata mmoja?
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Huo utamu hata hawajui ni kitu gani kwanza.
🤣🤣🤣 Dah! Kweli jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza pole kwao..
 
Kwahiyo nyuki chakula chao ni asali? Au kwanini wanatengeneza asali?

Ni kweli nyuki dume hufa baada ya kujamiiana?

Ni kweli malkia hatokag nje mpaka anakufa?
 
Mi ni mtaalamu katika sekta ya ufugaji nyuki, kama kuna kitu unahitaji kujua kuhusu Nyuki na Asali niulize nitajibu kadri ya uelewa wangu. Karibuni. "Without bees man will have only 4 years to live on earth" Albert Einstein!

Je, mfumo wa Kukojoa na Kunya wa Nyuki ni sawa na wa Viumbe Hai ( Wadudu ) wengine?
 
Kuna uvumi kuwa asali inayovunwa toka maeneo yenye kuendesha kilimo cha tumbaku (mf. Tabora), asali hiyo huwa na contents za nicotine.
Je, unasemaje kuhusu hili?
Hiyo issue hata mimi nilishawahi kuisikia, ninachoweza kusema ni kwamba, composition ya Asali ina uhusiano mkubwa na mimea ambapo wamechukua nectar, so kuwepo nicotine kwenye maeneo yanayolimwa tumbaku ni possibility. Ndio maana Asali inayotokana na miarobaini ina uchungu ndani yake, ya mkonge ina washa kiasi n.k.
Kitaalamu tunashauri Mizinga iwekwe angalau kilometa 7 kutoka mahali ambapo kilimo chenye matumizi ya pestcides kinafanyika, kwa sababu foraging rangi ya nyuki ni 6kms. Maana yake nyuki haendi zaidi ya 6km kutafuta chakula, so kuepuka contamination kwenye Asali ni vema tukafanya beekeeping mbali na mashamba.
 
Nyuki huchukua muda gani kuingia kwenye mzinga mpya
Inategemea na uwepo wa makundi eneo husika. Unaweza kuweka mzinga asubuhi, mchana wakaingia, au unaweza ukaweka mzinga leo wakaingia baada ya miezi miwili.
 
Kwahiyo nyuki chakula chao ni asali? Au kwanini wanatengeneza asali?

Ni kweli nyuki dume hufa baada ya kujamiiana?

Ni kweli malkia hatokag nje mpaka anakufa?
Nyuki chakula chake ni Asali, so huwa anatengeneza kwa wingi na kuhifadhi kwa ajili ya wakati wa ukame ambapo hakutakuwa na maua. Na sisi tunavizia akishaweka tunamuibia.
Ni kweli nyuki dume hufa baada ya mating.
 
Ndio hio Mizinga, neno lilinitoka na nkatumia masega tu 😀

Okay, mfano mimi shamba nnalo, linafikika kirahisi tu na chanzo cha maji kipo chini ya 5KM.

Mimi kinachonitatiza ni hawa nyuki, huwa wanatokea wapi wenyewe ikiwa eneo husika hakujawahi kuwa na nyuki ata mmoja?
Kwa kawaida nyuki wanapokuwa wanaishi mahali say kwenye pango au mzinga, wanazaliana, wanapokuwa wengi na nyumba kuanza kuonekana ndogo wanajigawa, lkn kabla ya kujigawa wanatengeneza Malkia mpya, then nusu wanaondoka, hiyo tunaita Swarming, ndio utakuta wametua kwenye baraza yako au kwenye mti. Then wachache wanatoka (wanaitwa scout bees) kwenda kutafuta nyumba. Sasa akija akakuta mzinga upo free anarudi kuwaeleza wenzake kuwa kuna nyumba mahali, then wote wanaingia. That's how it works
 
Kama nyuki wanaweza kutengeneza asali locally, actually niku_Assemble. Maana nyuki hukusanya necta za maua mbalimbali.
Je sisi binaadamu na teknolojia yetu kuubwa tuliyonayo Je kwanini tusiweze kutengeneza asali yetu??kama vile vile nyuki wafanyavyo.
Kama jibu ni haiwezekan basi ningependa kujua Why?
Na kama jibu ni ndio tunaweza basi ningependa kujua How???
Daah,nimelipenda hili swali.Ngoja nami niingie chimbo nitafute mbinu za kutengeneza asali bila kutegemea nyuki.But I think there are some enzymes secreted from their bodies which are very essential components for honey production.
 
Wanapochukua Nectar wanapoitema kuna ingredients zingine zinatoka mwilini mwao, that's why we can not synthesize honey with similar composition kama natural honey, itaharibika mapema tu!
Kama tunaweza tengeneza vitamin vilivyopo kwenye matunda na mboga mboga ndani ya maabara na vinafanya kazi effectively kama au zaidi ya vitamin halisi kutoka kwenye Matunda. Je kwanini tusitengeneze hizo Unknown Ingredients zinazotoka kwenye nyuki??
 
Artificial hii haitakuwa na asilia
 
Mtaalamu Mimi nauliza kama kuna ukweli kwamba kung'atwa na nyuki ni dawa ya mishipa,pia kwanini wengine waking'atwa huvimba wengine hawavimbi,je malkia ana paa au hubebwa kama nadharia nyingi zinavyosemwa
 
Ukitaka kufuga nyuki lazima uwe na yafuatayo.
1. Eneo la kufugia, maana yake eneo lenye miti inayotoa maua.
4. Eneo liwe mbali kidogo na makazi ya watu, kwa kuwa nyuki wetu wa Afrika kila mtu anawajua.
Ukifuga nyuki karibu na makaazi ya watu, au kwenye makaazi ya watu, haitawezekana kwa nyuki kutengeneza asali hata kama kuna maji na maua ya kutosha?
 
So hao workers wanakuwa hawana jinsia..?
Kama hawana jinsi aisee dunia haipo fair yani wanakosa utamu..au ndio maana utamu wao wanauhamishia kwenye asali..😅😂
Dunia ipo fair kwa kuwa hawawezi kula utamu Mara mbili ndo maana wakipanda wanakufa,wengine wanakula utamu wa asali inatosha,malkia ndo amependelewa kula+kuliwa
 
Back
Top Bottom