Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Yan nyiny hamjajua shida ulipo.. Kwa uzoefu wangu wa 10 yrs .. Kwanza hakuna MTU anapenda kuumiza kichwa.. pili mafund mbao wengi sio wabunifu vitu vingi wanafanya ni vile vile Kwa kutumia kanuni zile zile. Sasa ukimleta kwenye secta ya spika unamwambia spika tunahitaji itumie gundi nyingi kusiwe na leakage yy anatumia uzoefu WA kwenye kutengeneza milango anaweka gundi kidg spika inakuwa na leakage... Shida inaanzia hapo
 
mbina carpenter bongo wako vyema sana mkuu. kwa huku nilipo lkn.
Ujue kutengeneza spika sio kutengeneza kitanda boss, mm nipo ktk iyo field najua .. Kwa fund wa electronics anaetaka kutengeneza spika na akiwa hajui kanuni na taratib za spika alimpa fund selemara Yan atafanya madudu tu.. kwaiyo sisi wenyewe ndo tuwafundishe maselemala spika huwa zinakuwaje ktk kuunda sio unafanya Tu kama kiti au meza
 
Kaz unayo brother
 
Nafikiri kama ulivyosema basi ipo haja ya kufanya hvyo.
 
Kudos, nilisoma historia ya mwanzilishi wa kampuni ya JBL ilinihuzunisha sana maana jamaa alikuwa na vision kubwa tatizo likawa mtaji na vifaa, mpaka aliamua kujinyonga sababu ya madeni. keep on struggle blaza utatoboa tu
 
Kudos, nilisoma historia ya mwanzilishi wa kampuni ya JBL ilinihuzunisha sana maana jamaa alikuwa na vision kubwa tatizo likawa mtaji na vifaa, mpaka aliamua kujinyonga sababu ya madeni. keep on struggle blaza utatoboa tu

waanzilishi wa kampuni kubwa zote leo hii waliishakutana na bankrupt kipindi fulani.

inahitaji passion imara kweli kweli,jobs mwenyewe ilibidi auze hisa zote mpaka kuajiriwa kama meneja tu katika kampuni aliyoianzisha.
 
Kudos, nilisoma historia ya mwanzilishi wa kampuni ya JBL ilinihuzunisha sana maana jamaa alikuwa na vision kubwa tatizo likawa mtaji na vifaa, mpaka aliamua kujinyonga sababu ya madeni. keep on struggle blaza utatoboa tu
yote kwa yote tupo kwenye zama ambazo teknolojia imekuwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…