Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Jbl 12” 😁😁🙌🏻🙌🏻 Nmelala nna vibrate kwa heavy sound😌😅😅
 

Attachments

  • C55A716E-F754-4DD6-955D-8361BD9ABFF4.MOV
    14.2 MB
Jbl 12” 😁😁🙌🏻🙌🏻 Nmelala nna vibrate kwa heavy sound😌😅😅
Kubadili mp3?
sijakusoma...

project bado center na surround speaker tu. kila kitu kipo ndani (driver na crossover) bado mdf tu na finishing materials.
 
Ndio maana nikasema hio kodtec 5.1 ya kiwaki. Ile 2.1 ndio nyokow na muamuzi wa mwisho ni sikio lako mzee. Waliosikiliza wanaelewa zaidi nini namaanisha.
Mkuu kwa heshima niliyo nayo kwako naomba useme neno na Hilo neno ndilo nitakalolifuata.
Bajeti yangu ni kununua mchina na Nina machaguo mawili nayo ni Koditec yenye chanel 5.1 na Koditec yenye chanel 2.1. naomba ushauri wako kwa uzoefu wako na ulivyozisikiliza vizuri Kati ya hizo mbili ni ipi itanifaa kupata mziki mzuri boss?
Nashukuru [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mziki mzuri ni pesa mzee!
Yan pata picha bass speaker nzuri inaanzia 100000! Hadi 150
Hujaja kwenye box design
Bado rangi ya kuipulizia hiyo box
Njoo mashine
Njoo speaker za midbass nzuri
Yan sound nayoitaka mim nkikaa nianze kuitengeneza ntatumia 80000+
Sababu
Nataka midbass zipige full
Ziwe 5!
Na bass ziwe2 kila moja ya nch12!
So definitely ni 5.2
Afu kuna button utabonyeza itazifanya hizo midbass 4 zipige tweeter afu moja itapiga midbass kama kawaida...
Hi inamaana kama sitak kuweka bass nzito hiyo midbass itanipa low frequency kidogo

Ila nkiwa na ham na bass naongeza tu saut yake...[emoji16]
Coz huwez kusikiliza low bass kwa mda mrefu
Hiyo budget yake ni sh ngapi???
 
Mkuu kwa heshima niliyo nayo kwako naomba useme neno na Hilo neno ndilo nitakalolifuata.
Bajeti yangu ni kununua mchina na Nina machaguo mawili nayo ni Koditec yenye chanel 5.1 na Koditec yenye chanel 2.1. naomba ushauri wako kwa uzoefu wako na ulivyozisikiliza vizuri Kati ya hizo mbili ni ipi itanifaa kupata mziki mzuri boss?
Nashukuru [emoji120][emoji120][emoji120]
2.1 ni balaa zito mkuu
 
Back
Top Bottom