Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Kwa taarifa yako hio ya chini ndo nzuri
kwa subwoofer za digital control Sea Piano amefunika wote. ukiizima sauti kama uliicha 25 ukiiwasha utaikuta hivyo hivyo, ukiset subwoofer volume mpaka 30 utaikuta hivyo hivyo, ukiset gain ya tremble level 13 au 10 utaikuta hivyo hivyo,ukiset gain ya bass level 12 or 14 utaikuta hivyo. tofauti na sub nyingine waliposetia sauti from factor manufactururing itaanzia hapo mfano kama waliseti iwe inaanzia vol level 27 itakuwa inaanzia hapo,au kama waliseti sauti ya juu ya mwisho 60 itaanzia hapo ukiwasha, bass level 2 itaanzia hapo mpaka upandishe tena mpaka 6 na trembo hivyo hivyo. kwa hiyo unakuwa na kazi ya kufanya seting kila mara uwashapo subwoofer yako. hakika ni usunbufu
 
Toleo zuri ni yenye volt 14± inatumia tda2050 na mbili Ni UTC 2050
Mzigo ni old model
Unatumia transformer ya 18vac+_
Powered by tda 2050
Two of them for tweeter
Two remained bridged to drive woofer


Moja kati ya matoleo bomba sana sana sanaa


Hi tuipe na Bluetooth mkuu[emoji2][emoji2]
 
Ndiyo mkuu imejilock,inaandika protection,nilienda Sony pale mliman city wakasema mpaka niende Samora tatizo muda ndo umekua kipengele

Pole! Hadi tuiangalie
Huenda kuna components haziko sawa
Nenda ulipoambiwa ikishindikana tuone tufanyaje
 
Tl? Mbon tumeagiza juzi tu
Upo dar?
Mkuu, si mradi TL au TL494, bali pia package yake pia ni muhimu. Hili suala nimeshalieza kwenye post zangu zilizotangulia ila milango ya ufahamu imefungwa watu wasielewe. Ni TL494 ya kubandika, si ya kuchomeka, na upatikanaji ni mgumu baadhi ya maeneo, ndo maana nimeuliza mhitaji mahali alipo, kaziba masikio ipi asisaidiwe. Na-log off.
 
Mkuu, si mradi TL au TL494, bali pia package yake pia ni muhimu. Hili suala nimeshalieza kwenye post zangu zilizotangulia ila milango ya ufahamu imefungwa watu wasielewe. Ni TL494 ya kubandika, si ya kuchomeka, na upatikanaji ni mgumu baadhi ya maeneo, ndo maana nimeuliza mhitaji mahali alipo, kaziba masikio ipi asisaidiwe. Na-log off.

[mention]dyuteromaikota [/mention]
 
Mkuu umejaribu kuhamisha matundu yakuchomekea nyuma?
Ikiwa ukihamisha inaimba basi tatizo lipo ndani kwenye system ya waya au ic inauo drive hyo ic
Ikiwa haitaimba hata ukichomeka kwingine bAsi speaker huenda inashida ndani yenyewe au waya zimekatika
Mkuu subwoofer langu speaker moja ina koroma,nyingine nzima,je kutumia speaker moja kunaweza kuuwa subwoofer??
Pili nikichomoa speaker zote besi inakuwa mbaya kama ina koroma pia.ila ukiweka speakers balaaa jingine,pia switch ya kuzimia na kuwashia imekufa kwani.
Nyongeza,ina miaka 5 sasa haijaah finguliwa na nataka niipeleke kwa fund angalau ikafunguliwe iondolewe vumbi ndani je ni sawa??
Na speaker huwa inauzwa hata moja ni aliang lx 313.
 
Mkuu subwoofer langu speaker moja ina koroma,nyingine nzima,je kutumia speaker moja kunaweza kuuwa subwoofer??
Pili nikichomoa speaker zote besi inakuwa mbaya kama ina koroma pia.ila ukiweka speakers balaaa jingine,pia switch ya kuzimia na kuwashia imekufa kwani.
Nyongeza,ina miaka 5 sasa haijaah finguliwa na nataka niipeleke kwa fund angalau ikafunguliwe iondolewe vumbi ndani je ni sawa??
Na speaker huwa inauzwa hata moja ni aliang lx 313.

Spika kukoloma huenda kuna shida ya speaker au ic yake
Kujua kipi shida chukua ile isiyokoloma hamishia hapo ilipo inayokoloma
Ikiwa itaimba vizuri bas shida n speaker
Ikiww itakoloma pia bas ni tatizo ndani

Hapana hakuuwi subwoofer bal wew hutasikia mziki mzuri

Bass kukoloma ni hitilaf kwenye spika au redio yenyewe
Switch inaweza kubadilishwa tu
Nadra sana subwoofer kuwa na vumbi labda kama inawekwa mazingira yenye vumbi kama sivyo si rahis
 
Back
Top Bottom