Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Nini kimefanya ipasua capacitors zote nane? Naomba kujua mkuu maana na mimi natumia mziki huu maskani..

1 umeme kama haujakaa sawa
2 kuweka sauti kubwa kwa mda mrefu nonstop (kuna watu hutumia system hiz sehemu za wazi wanaifoc ifanye kaz kubwa
 
wakuu naomba mnaojua mnisaidie katika hili
nina bajeti ya Tsh 700k ipo limited
Ila nahitaji kitu quality
music clear
Stereo kama yote
yaani kifupi mgeni wangu nae aseme kweli umefunga kitu.
sasa nimepitia hizi sound bars na home theaters
nimeshindwa coz sina maarifa yoyote Juu ya hivi vitu
ubora wake, watts, na hitaji langu
Sony
Hisense
Lg n.k
IMG_3655.jpg

IMG_3656.jpg

IMG_3652.jpg

IMG_3653.jpg

IMG_3657.jpg

IMG_3654.jpg

IMG_3651.jpg
 
wakuu naomba mnaojua mnisaidie katika hili
nina bajeti ya Tsh 700k ipo limited
Ila nahitaji kitu quality
music clear
Stereo kama yote
yaani kifupi mgeni wangu nae aseme kweli umefunga kitu.
sasa nimepitia hizi sound bars na home theaters
nimeshindwa coz sina maarifa yoyote Juu ya hivi vitu
ubora wake, watts, na hitaji langu
Sony
Hisense
Lg n.k
View attachment 2458130
View attachment 2458131
View attachment 2458132
View attachment 2458133
View attachment 2458134
View attachment 2458135
View attachment 2458136

Kaka unajua kumshauli mtu kitu chakukichukua mojakwamoja inaweza kuniwia (kutuwia) vigumu kidogo kutokana na mimi kutokujua mojakwamoja unachokitaka
[emoji1314]Watu wengi hununia kitu kwasababu ya EVIDENCES!

Ni ngumu kidogo mtu kununua kitu tu kwasababu kakiona dukani (labda awe hajui vitu)
Ila kitu namba moja cha kukusaidia kujua power ya amplifier yako ni watts!
Usishangae kwanini nasemea amplifier baada ya home theater
Vyote ni kitu kimoja
Na amplifier ndio ipo ndani ya vitu vyoote
Subwoofer
Home theater
Av receiver
Sound bar
Na hata sim yako
Nk
Vyoote vina amplifier hivyo ile amp yake ina watts ngap (per channel) ndio ukubwa wa mziki wake

Najua hujanielewa nliposema per channel

Home theater (HT)
Zina speaker (spk) 6 jumla
Ni sawa na kusema zina channel 6
Ila je kila channel ina watts ngap? Ndio unapata total watts
Hivyo 1000 watts ukigawa kwa 6 ndio unajua kila channel inakupa watts ngapi
Hivyo kama ni av receiver au ht kuielewa ni kuangalia total watts afu zigawe kwa idadi
Hi itakusaidia
Hua naona watu wakipata shida juu ya hi
Na hata wew nakupa tu kwa faida yako upate uelewa
Ukitaka heavy sound bas lazima pawe na watts nyingi
Watts nyingi itakua na bei juu zaid sababu itakua na power kubwa
Power kubwa ndio ukubwa wa sound system yenyewe
emoji117.png
[emoji2532]Uwezo wa kusikika vizur na good looking na kua na option nyingi mfano Bluetooth ,hdm arc na hdm ni features wanazokuwekea tu ili uwe na uwanja mpana wakufanya kile unachokitaka

Hivyo basi inawezekana ikaniwia vigumu kukutajia modern number mojakwamoja au ku point kua nunua hi sababu sielew unachokitaka
Au pengine

Ila nje ya mada kwa 700000 utapata zenye watts za chini kidogo sidhan kama utaweza pata inayofikia watts 1000
 
View attachment 2450077
Bass speaker ya HOME THEATER YA SONY ililiwa na panya
Hivyo ikabidi tudhibiti kwa kusuka wavu kwenye tundu la hewaView attachment 2450079
Na radio mtumba kenwood na shida na spika maan zilizopo hazitoi mziki vizuri, zinaonekana zilisukwa coil kama sijakosea, pia kama kuna uwezekano wa kufunga bluetooth naomba nisaidie gharama zake, Mi nipo iringa
 
Ameniambia tubadlishe speaker,hv Mkuu speaker yenye 80watts na 2ohms ukilinganisha na speaker yenye 70watts na 8 ohms ipi inapga zaid?
Spika zote Ni almost sawa utofaut mkubwa upo kwenye impedance za spika

Kuhusu kupiga kila spika inapiga vizuri kwenye amplifier sahihi

Eg hio ya 2ohms weka amplifier inayoweza toa 80w at 2ohms

Na ya 70w weka amp inayoweza toa 70w @ 8ohms hizo spika huwezi changanya kwenye amplifier moja kutakuwa na utofauti mkubwa sana
 
Mzigo upo poa sana mkuu, yani ni kati ya manunuzi yangu bora niliyowahi kufanya..

Nilochogundua tofauti kubwa ukiringanisha na izi Chinese HiFis ni sound quality, mzigo ata uwe kwenye sofa, ukiwasha shazam kujua wimbo kitu kina daka, tofauti na Sea piano yangu ukikaa kwenye sofa shazam inagoma, mpaka upereke sim mbele ya speaker ya twita.
Kwamba seapiano inaimbaje Hadi simu isidake?
 
Na radio mtumba kenwood na shida na spika maan zilizopo hazitoi mziki vizuri, zinaonekana zilisukwa coil kama sijakosea, pia kama kuna uwezekano wa kufunga bluetooth naomba nisaidie gharama zake, Mi nipo iringa

Bluetooth ni 15000 kuinunua
Ufundi ni maelewano tu
Speaker inatakiwa zi checkiwe
 
Back
Top Bottom