Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
hiyo lg nimeisikikiza mkuu,haina kitu, na ni lg mchina,box size ya spika kabana sana,katumi mdf laini sana, kairemba na plastics, bass nyepes, ni redio ya kisasa ila kwa maana ya mziki hamna kitu
Mimi nilisikiliza kidogo dukani,niliona mziki wake ni mzuri.Ni kweli ni LG made in China. Hiyo home theater nyingine ni SONY,ina watts 400 nadhan imetengenezwa dubai lakini sijaijaribu
 
Mimi nilisikiliza kidogo dukani,niliona mziki wake ni mzuri.Ni kweli ni LG made in China. Hiyo home theater nyingine ni SONY,ina watts 400 nadhan imetengenezwa dubai lakini sijaijaribu

Siko saw kwenye output sound
Kwasababu sijaisikiliza maskioni
Ushauri wangu sikiliza zote
 
Kati ya music options ipi ni nzr kuseti home theater?
Na kupata quality nzr ya mziki?
--jazz
--rock
--dance
---stereo
---music
---pop.

Nina Samsung home theater.
 
Siko saw kwenye output sound
Kwasababu sijaisikiliza maskioni
Ushauri wangu sikiliza zote
Sawa boss nitafanya hivyo,lakini SONY ina wired connection...na kwenye installation wanashauri zile speaker ndogo zikae nyuma yako,je huwa zinakuja na nyaya ndefu za kutosha kuweka speaker nyuma ya sebule wakati sub woofer inakuwa mbele yako sebuleni?
 
Ndio zina waya ndefu kidogo
 
Kati ya music options ipi ni nzr kuseti home theater?
Na kupata quality nzr ya mziki?
--jazz
--rock
--dance
---stereo
---music
---pop.

Nina Samsung home theater.

Hizi ni saved equlizer
Wew ndio unaamua tu kutokana na unavyosikia sound yako
Uipendayo wew mwingine hatapenda
 
Naomba kuuliza mara nyingi mziki haswa kwa level ya kinyumbani labda ni watts ngapi ni standard ? Ili uwe unasikika vizuri na je ni ipi Bomba mfano wa soundbar ,HT haswa kama ndo habari ya mjini yaani teknolojia mpya.

320Watts
400watts
500watts
600watts
1000watts

Mziki uwe wa kistaarabu na je Yale maspika ya kusimama kwa soundbar Sion kama ni smart kwa ulimwengu wa sasa zaidi ya kelele bora vile vidogo tena wireless unaweza kuvitega hata kwa nyuma ya sofa ..
 
si
Naomba kuuliza mara nyingi mziki haswa kwa level ya kinyumbani labda ni watts ngapi ni standard ? Ili uwe unasikika vizuri na je ni ipi Bomba mfano wa soundbar ,HT haswa kama ndo habari ya mjini yaani teknolojia mpya.

320Watts
400watts
500watts
600watts
1000watts

Mziki uwe wa kistaarabu na je Yale maspika ya kusimama kwa soundbar Sion kama ni smart kwa ulimwengu wa sasa zaidi ya kelele Bora vile vidogo Tena wireless unaweza kuvitega hata kwa nyuma ya sofa ..

kwa habari ya urefu wa spika hapo unakisea sana, hv mkuu umeshawahi kuona hi end audio speaker system kama utopia,focal,B&W,beo lab etc?
 
Eti "sioni kama ni smart kwa ulimwengu wa sasa". Kuna kitu bado hukijui kuhusu sound systems

Mkuu, inabidi utoke kwanza kwenye hiyo mentality yako unaitaga "mziki wa kistaarabu"...ufunguke uone dunia ya mziki ilivyo.

Unatakiwa uelewe kuwa Hizo wireless soundbars are not the best kwa ajli ya Music.. zimetengenezwa MAHUSUSI kwa ajili ya movies,kwenye mziki, zitakupa mziki wa wastani.

Pili, Unapaswa kuelewa kuwa Hizo speakers za nyuma ya kochi SIO kwa ajili ya Music, ni kwa ajili ya movies.
 
Ndo ninavyotaka sio makelele kama kigodoro ..Unaweza kweli kuweka mziki mkubwa sana sitting room yako kama Kuna kigodoro .Mtasikilizana kweli?

Ushamba mzigo mziki wa kawaida hayo makelele peleka bar
 
si

kwa habari ya urefu wa spika hapo unakisea sana, hv mkuu umeshawahi kuona hi end audio speaker system kama utopia,focal,B&W,beo lab etc?
Izo watts ni nyingi sana hata 400 mziki mkubwa niaje ..uzuri wa speakers zilete muonekano mzuri wa sitting room..kama ndefu fresh basi naona inafaa ila nimeangalia sitting za watu wenye pesa wengi mpaka Wanamuziki sijwai kuona hayo maspiker makubwa zaidi ya studios zao.
 
Ndo ninavyotaka sio makelele kama kigodoro ..Unaweza kweli kuweka mziki mkubwa sana sitting room yako kama Kuna kigodoro .Mtasikilizana kweli?

Ushamba mzigo mziki wa kawaida hayo makelele peleka bar
miziki ya maana ukiachana na hii ya kichina,haina masauti ya makelele. nilikuwa nimepanga somewhere dodoma, siku baba mwenye nyumba alipoingia sebuni kwangu alishangaa sana mziki wangu unavyokitita na una chuja vya kutosha lakini hausiki nje ilihali sebule yangu ilikuwa karibu na sebule yake.

mziki wa maana atlest budget ianzia 1.5
 
Kati ya music options ipi ni nzr kuseti home theater?
Na kupata quality nzr ya mziki?
--jazz
--rock
--dance
---stereo
---music
---pop.

Nina Samsung home theater.
saved equlizer, changamoto yake huwa hazikupi righ music kwa kila wimbo utakaosikiliza,kutokana na ubora wa muziki ulivyorekodiwa, unaweza kusikiliza wimbo mmoja katika seting ya rock ukasikika vyema lakini unafuata ukagoma kusikika vyema kwenye hiyo seting labda uchange to jazz or pop, but ukiwa na graphic eq ya kuset mwenyewe inakuwa inapunguza hayo mambo
 
miziki ya maana ukiachana na hii ya kichina,haina masauti ya makelele. nilikuwa nimepanga somewhere dodoma, siku baba mwenye nyumba alipoingia sebuni kwangu alishangaa sana mziki wangu unavyokitita na una chuja vya kutosha lakini hausiki nje ilihali sebule yangu ilikuwa karibu na sebule yake.

mziki wa maana atlest budget ianzia 1.5
Ndo nataka izo mziki wa kistaarabu sio Yale maspika kama Kuna kigodoro.
 
Ndo ninavyotaka sio makelele kama kigodoro ..Unaweza kweli kuweka mziki mkubwa sana sitting room yako kama Kuna kigodoro .Mtasikilizana kweli?

Ushamba mzigo mziki wa kawaida hayo makelele peleka bar
Mziki wa maana hauna hayo makelele.

Tatizo ni kwamba wewe hujawahi kusikia music system ya maana. Wewe unajua home thearte na soundbars za Sony, lg na Samsung.
 
Ndo nataka izo mziki wa kistaarabu sio Yale maspika kama Kuna kigodoro.
Floor standing speakers (Spika ndefu) za brand zinazoeleweka zinazotengeneza sound system like Klipsch, Polk, Triangle, B&W, Focal na KEF hazina hayo makelele.

Tatizo ni kwamba Hizo brand hujawahi kuzisikia na huzijui, wewe unajua Sony,Samsung na Lg(ambao kwenye Speakers ni kama hawapo)
 
Back
Top Bottom