Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 

Mkuu ...radio kuwa na digital functions kunahusianaje na radio kuwa na mdundo🤔 .. functions ni tofauti na aina ya amp itakuwa imewekwa ndani ..zipo digital , upande wa amp ni class AB amp ndogo tu zingne class D pia upande wa zile analogia ziko hivo hivo tu
 

Subwoofer ni speaker ya bass tu inayoweza cheza extremely low usually 20hz to 150hz...woofer hii ni midrange speaker inaweza perform from 60 or 50hz hadi 2khz zingne Hadi 3khz ....

Hiyo woofer unaeza itumia kama speaker ya bass pia depending na frequency utakazoipa....

Subwoofer unaeza ipata kwenye hizo zetu za kichina ama hizo home theater system ama spika za majukwanii PA ...kwenye zile za magari zenye mabox makubwa kwa ajili ya bass

Woofer ..hii unaeza kuta kwenye HIFI system ...eg zile LG zina spika mbili unakuta ni stereo juu wanaweka vi twita vyake some hifi pia zina subwoofer na woofer ...eg lg hifi ya watts 720 gugo utaona zile mbili spika za duara zenye vitwita ndo woofer na ile moja ni sub

Woofer pia ipo kwenye speaker za magari eg 6*9 speaker or zile components speaker ..kwenye 6*9 lile duara la yai ndo woofer linacheza low na mid vizuri tofaut na subwoofer haiwez cheza mid hata ukiipa frequency za mid itaimba vibaya sana

Woofer haiwezi cheza low sana mfano 50hz kushuka pia haiwezi cheza high sana eg 4khz kupanda kifupi inacheza band bass

Speaker za studio pia pale kuna woofer na twita kale cha juu ..speaker za studio huwa hamna sub
 

Siku hizi kuna ambazo ziko kama hizi kina aboda seapiano zinaitwa svs ni ghali sana sijajua origin yake ni inchi gani ila sio china zinapiga kama za kwenye magari
 

Siku hizi kuna ambazo ziko kama hizi kina aboda seapiano zinaitwa svs ni ghali sana sijajua origin yake ni inchi gani ila sio china zinapiga kama za kwenye magari
 
Kwanini Subwoofer nyingi zinatumia Ic ya 2003/2005/2030/2040/2050 badala ya Transistors?

Hii huwa inategemea na nguvu unayotaka speaker utakazotumia nk...hizo ic ulizotaja pia zina transistor ndani yake...

Mfano unataka sabufa ..complete yani multmedia system ..mfano nahitaji watts 7 to 10 kwa ajili ya twita na bass labda watts 15 ..hapo kutumia transistor haifai au ni process ndefu moja kwa moja nitachagua ic ndogo labda tda7379 inaeza piga twita mbili na bass kwa watts hizo ....

Mfano nahitaji watts 20*2 kwa ajili ya twita na bass labda 40 to 60watts

Moja kwa moja nitachagua nitumie tda2050 nne mbili ziwe bridged kwa ajili ya sub...

Pia kama nataka labda watts 50- 80 kwa ajili ya twita kila channel na bass labda watts 100-200 kuendelea ..nitachagua transistor
 
rising na seapiano na kampuni gani sijui niliona bufa zao zinafanana kila kitu hadi satelite au ndo mambo ya sanlg na haojue na toyo
 
Quality audio by cheap devices. Small power but works fine.
 

Vyema mkuu
 
View attachment 1656307
Siku nikipata uwezo namshusha huyu! Sitaki visubwoofer vya bei rahisi [emoji123][emoji123]
Its a good vendor bt try svs instead..The best way ni kuanza taratibu sio mpaka upate cash ya pamoja...mimi mpaka leo sijaumaliza bt i hope one day ntaimaliza hii project... ukishafika huku siku ukiskia mziki wa kichina utahisi unakupigia makelele.
 
Its a good vendor bt try svs instead..The best way ni kuanza taratibu sio mpaka upate cash ya pamoja...mimi mpaka leo sijaumaliza bt i hope one day ntaimaliza hii project... ukishafika huku siku ukiskia mziki wa kichina utahisi unakupigia makelele.
[emoji106]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…