Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Ili kusiwepo na shida hizi za mtumba zenye 200W zatakiwa Ohm yake isizidi ngapi?

Mkuu kwanini unataka kutumia hizo za mtumba? Yan lengo lako ni nini ili nikupe mawazo....
Ohms isipungue tatu 3ohms
Zikizidi pia sauti itakua inapungua
Kwamfano ukiweka 8ohms
 
Kwema mkuu....nna home theatre yangu ya sony (code siikumbuki ila ina spika ndefu mbili).....

Kinachotokea ni kwamba ukifungulia mziki max kwa mda mrefu kuna saa inafika bass inajizima......kuwaka mpaka uzime na kuiwasha.....

Imekaaje hiyo wataalam.
 
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza

KaribuView attachment 1559794





Stay here....
More good things are here.....
Welcome......View attachment 1921368
View attachment 1921369
Napenda kujua vifuatavyo
1. Tofauti kati ya operation amplifier na amplifier kikazi.
2. Kwa kuangalia ktk sakiti ya subwoofer utajuaje kwamba hii ni operational amplifier na hii ni amplifier, unazitofautishaje.?
3.Mechanism ya sauti ikoje? ni semiconductors zipi zinahusika katika suala la sauti ikiwemo suala la volume up and volume down?
kelphin kepph
 
Haijarishi mkuu purposely ni kujifunza kutumia, nitainstall home , napenda sana piano , nataka nijifunze ila mashine niwe nayo home

Kama hii hapa nahitaji
View attachment 2075734
View attachment 2075735
Anhaa!! Hiki sijawahi kutumia hii. Nilianza na YAMAHA PSR 170
YAMAHA PSR 450
YAMAHA PSR 550
YAMAHA PSR 1000-2100
YAMAHA PSR S650-S950
Na sasa niko na PSR SX900 (TOUCHSCREEN)
 
Napenda kujua vifuatavyo
1. Tofauti kati ya operation amplifier na amplifier kikazi.
2. Kwa kuangalia ktk sakiti ya subwoofer utajuaje kwamba hii ni operational amplifier na hii ni amplifier, unazitofautishaje.?
3.Mechanism ya sauti ikoje? ni semiconductors zipi zinahusika katika suala la sauti ikiwemo suala la volume up and volume down?
kelphin kepph

Mkuu vuta pumzi kisha soma taratibu....
Ntajibu swali moja baada ya lingine!
1
Operation amplifier au op amp na amplify ni kitu kimoja...zote zinaongeza nguvu ya sauti
Ila zinatofautiana output power
Opamp inapokea signal kutoka kwenye MP3 players,dvd players, au laptop itaongezea nguvu ya signal kabla yakuiingiza kwenye amplify.....
Alafu amplifier itaongeza nguvu ya nguvu ndogo iliyotoka kwenye opamp
Twende kwenye mfano
2.1 multimedia systems ambayo ndio hizi zinafahamika km subwoofer ile speaker ya bass hua inadunda tu alafu zile tweeter zinaimba sauti nyembamba sio!?
Lakini amplifier za ndani zote ni sawa
I mean channel ya bass na ya tweeter zote hutumia ic au transistors sawasawa
Kwahyo ni sawa na kusema amplifier inayosukuma ile bass inaweza sukuma tweeter zile pia
Ki kawaida amplifier yenyewe inakuza nguv ya sauti tu
Ila hizo sauti zinatofautiana frequency (usikivu)
Ile signal inayodunda tunaita low
Ila tweeter tunaita high
Lakini kumbuka kua hiz pc zinatoa stereo
I mean sio low wala high
Zikiingia ndani ndio zinakutana na opamp ambayo itaziongeza nguvu kwanza( kwasababu ni amplifier pia) kisha zitafanyiwa kitu kinaitwa filters Yaan kutengeneza hizo frequency sasa!
Hivyo output signal ya opamp inategemeana na aina ya opamp nikisema aina nnamaanisha inategemeana na filters walivyoitengeneza itoe aina fulani ya mziki
Alafu hizo output signal ndio zitaingia kwenye amplify


Zile power amplifier kubwa mfano wa hi apa chini
IMG_6285.jpg


Unajua kwanin haina vidude vingi vyaku tune saut zaid ya hivyo viwili( hivyo viwili havi tune mziki zaid vinaongeza na kupunguza SAUTI TU!)
Kwasababu hi ni amplifier tu haina opamp yeyote
Zile crossover , equalizer, zote ni opamp kwasababu zina tune signal kusikika tofauti tofauti lakin pia hizo zote zina amplify signal lakin kwa kiwango kidogo sana kias kua ili usikie unahitaj amplifier [emoji28][emoji28] yan sijui umepata picha?
!!!
IMG_6286.jpg

Hi pia ni amplifier vilevile ila hi ina opamp!
Just understand
Angalia ina sehemu ya kuchomeka frash apo
Inamaana hiyo MP3 players ikitoa mzik itapeleka kwenye opamp ampapo utatune sound kama unavyoona hapo Alafu signal ndio zitaenda kweny amplify
Mkuu umepata mwanga?
 
Napenda kujua vifuatavyo
1. Tofauti kati ya operation amplifier na amplifier kikazi.
2. Kwa kuangalia ktk sakiti ya subwoofer utajuaje kwamba hii ni operational amplifier na hii ni amplifier, unazitofautishaje.?
3.Mechanism ya sauti ikoje? ni semiconductors zipi zinahusika katika suala la sauti ikiwemo suala la volume up and volume down?
kelphin kepph

Operation amplifier haiendesh load ( I mean huwez kuunga speaker hapo) bali yenyewe outpt yake itaenda kwenye amplifier ambayo huko ndio utainga speaker
Ndio maana utaona zile 4558 , TL 084 hazina heat sink ila 2050 lazima uweke heat sink
Umeme unaoingia kwenye opamp ni tofauti na amplifier
Mkuu hili ni somo mama kwenye sound system ni ngum kunielewa hapa labda tukizungumza
 
Napenda kujua vifuatavyo
1. Tofauti kati ya operation amplifier na amplifier kikazi.
2. Kwa kuangalia ktk sakiti ya subwoofer utajuaje kwamba hii ni operational amplifier na hii ni amplifier, unazitofautishaje.?
3.Mechanism ya sauti ikoje? ni semiconductors zipi zinahusika katika suala la sauti ikiwemo suala la volume up and volume down?
kelphin kepph

Swal la3 sijalisoma vizuri...unamaana gani? Kipi kinafanya saut ya amplifier (power) kuwa kubwa au ndogo au
Vitu gani vinafanya sauti kua kubwa au kipi mkubwa
 
Kwema mkuu....nna home theatre yangu ya sony (code siikumbuki ila ina spika ndefu mbili).....

Kinachotokea ni kwamba ukifungulia mziki max kwa mda mrefu kuna saa inafika bass inajizima......kuwaka mpaka uzime na kuiwasha.....

Imekaaje hiyo wataalam.

Ikizima haileti endication yeyote
Shida ya HT zinakua processed na computa
Kama shida itakua power system unaweza rekebisha, kama itakua audio processing basi nisikudanganye hadi irudi kwa wahusika
Wakati mwingine hata kama waya hazijakaa sawa inaweza kua sasab mkuu
Kifupi ni hardwares
 
Kuongeza sound na base!!,
Zile 3 za home theater zinabaki, zile mbili ziwe za mtumba!

[mention]devijoy [/mention] mkuu unachokitaka nadhan hakitawezekana
Kwasababu! Ile sauti inayotoka kwenda kwenye ht inakua imeshafanyiwa filters ni output tayari
Kwahyo imeshasetiwa kusikika vile mkuu
 
Back
Top Bottom