Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Mkuu kuna nyimbo moja inaimba "wewe dada asha mimi hapa baba yako...yani huyo asha kama anahusiwa jambo flani hivi....vipi unaujua huu Namichiga
 
nyimbo ya "sure" nitaipata wapi kwenye mtandao
 
nyimbo ya "sure" nitaipata wapi kwenye mtandao
"Sure" ipi?,maana kwa haraka haraka inanijia nyimbo ya kifo cha Kassim Sure (Baba Omary),ambayo imeimbwa na band ya Seven Survival kwenye albam no.3 mwaka 98.Sasa tupe ufafanuzi ili nijue namna ya kukusaidia [emoji125][emoji125][emoji125]
 
Mkuu kuna nyimbo moja inaimba "wewe dada asha mimi hapa baba yako...yani huyo asha kama anahusiwa jambo flani hivi....vipi unaujua huu Namichiga
Mkuu hebu jaribu kukumbuka vizuri hiyo mistari,maana kwenye band nyingi za mchiriku jina la Asha limetajwa.Lakini Alipotajwa Asha kama mtoto ni kwenye band ya Atomic kwenye mfululizo wa nyimbo za baba Asha,lakini kwenye band nyingine nyingi Asha katajwa kama mpenzi,mfano Jagwa Music Vol.4 kuna Asha,Seven Survival Vol.3 & 4 kuna Asha,Kombora Music Vol.1 kuna Asha, Atomic Vol.18 kuna Asha.Lakini humo mote anatajwa kama mpenzi,sasa hebu kumbuka vizuri hayo mashairi ya Asha kama mtoto [emoji125][emoji125][emoji125]
 
"Sure" ipi?,maana kwa haraka haraka inanijia nyimbo ya kifo cha Kassim Sure (Baba Omary),ambayo imeimbwa na band ya Seven Survival kwenye albam no.3 mwaka 98.Sasa tupe ufafanuzi ili nijue namna ya kukusaidia [emoji125][emoji125][emoji125]
sure aluka karandinga
 
Mbona mkuu mashairi ya huo wimbo uyaweki sawa?,kwa mfumo huo itakuwa ngumu kupata majibu juu ya swali lako [emoji125][emoji125][emoji125]
iyo nyimbo inahusiana na muhuni anaitwa sure , humo kwenye nyimbo wanamwelezea huyu sure matukio aliyo yafanya, kipindi cha komando yosso

..makaka zangu walikuwa wanapenda kuimba na kuipiga ila mimi siukumbuki vizuri...ninacho kumbuka alifanya tukio siku ya mechi uwanja wa tip uzuri sinza kwenye ligi ya ndondo, kipindi hicho bado nabeba viatu vya mpira vya kaka zangu

Kwa hiyo mkuu nipe connection ya hiyo nyimbo niwakumbuke marehemu kaka zangu
 
Hivi chichi baunsa alikuwa anahusika na nini 7survival kitengo chake

Maskani Yao ilikuwa mtoni au
Tandika ndugu
 
Hivi chichi baunsa alikuwa anahusika na nini 7survival kitengo chake

Maskani Yao ilikuwa mtoni au
Tandika ndugu
Chichi Baunsa alikua ni mpiga ngoma (Sondo) na alijiunga na Seven Survival akitokea band ya Tokyo Ngoma aliyokuwa na maskani yake Tandika.Na kuhusu asili ya makazi yake sina uhakika sana kwani nimemjulia ukubwani na sikuwahi kwenda indeep kuhusu hilo.
 
Hivi chichi baunsa alikuwa anahusika na nini 7survival kitengo chake

Maskani Yao ilikuwa mtoni au
Tandika ndugu
Kama ulikuwa unauliza kuhusu maskani ya band ya Seven Survival,jibu lipo kama ifuatavyo:Band ya Seven Survival wakati inaasisiwa mwaka 97 maskani yake ilikuwa ni Temeke kwa Sokota na jina la band lilikuwa ni Survival Original na mmiliki wa band alikuwa ni kaka mkubwa Masoud Zoba,na wakatoa Vol.1 maarufu iliitwa Champisi.

Baada ya hapo kuna kundi la wasanii likahama kwenda kuanzisha band yao,watu hao ni kama Juma Mpogo,Ramadhani Midoke,Mudy Jongo (Gostino Jala),Said Kitinike,Said Omary Kapenya,Kula Daku na Ramso wa Seven.Baada ya kuhama maskani yao ikawa ni Mtoni Kichangani na jina la band wakajiita #Seven Survival (Zingatia utofauti kati ya Survival Original na Seven Survival) katika mwaka huo huo wa 97,na kutoa albam walianza na Vol.2 kwani walidai hata ile ya mwanzo ni ya kwao kwani wasanii ni wao japo boss alikuwa Masoud Zoba.

Baada ya hapo harakati zikaendelea na wakatoka watu na kuingia watu.Na hatimaye mwanzoni mwa miaka ya 2000 band iliamisha maskani na kuhamia Mbagala kwa kina Nassoro Mwipi (Kepten Cholo Boy) ambae alikuwa kama katibu wa band.
 
Mkuu ngoja nizidi kupekua makablasha yangu kuhusu band za kanda ya Kinondoni,kuanzia Hisani Gari kubwa,Tumaini Jabali,Chaukucha Family,Wanyamwezi, Jagwa na hata Dar Nyota ili nitafute wimbo wenye huo ujumbe wako.Maana ingekuwa rahisi sana ungetaja japo band [emoji125][emoji125]
 
Kuna wimbo wa jagwa wanawapa pole jamaa zao kwa kufiwa na baba yao.
Unaimbwa hivi: ntazidi kuwabembeleza rafiki zangu nyie Juma wa ukae badwela
Najua mna uchungu wa kuondokewa baba yenu mzee....
Punguzeni mawazo fanyeni kazi kwani kifo kimeumbwa na Baba Mwenyezi.
Natanguliza shukrani
 
Unaitwa #Mzee Mgombelwa,muimbaji marehemu Jack Simela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…