Niulize jambo lolote kuhusu mziki wa Mchiriku/Mnanda

Mnanda ulianzia wapi???
Mziki wa mchiriku (mnanda) chimbuko lake ni jijini Dar es Salaam,hususani katika wilaya zote tatu kwa maana ya Temeke,Kinondoni na Ilala pia,kwani katika orodha ya band za mwanzoni kabisa (band waasisi) ukizitaja basi ni lazima uziguse wilaya zote tatu.

Mfano band kama Red Star na Night Star (Ilala),Dar Nyota na Hisani Gari kubwa (Kinondoni),Zipolari,Msasa wa Chuma,Topaz na Urahibu Buti Kubwa(Temeke).
 
Namichiga

Juma mpogo; "Jitume Babaa, jitumee fanya kazi oooh oooh ni Msingi wa Maisha yako... (mlio wa vigoma) Mtaji wa maskinii ni nguvu zake mwenyewe (sauti ya J.Mpogo na Jack Simela)

Sijui kama umeshaufahamu kaka!

Lakini nikiupata huu wimbo Mkuu wangu Namichiga kwakweliii ntafurahi sana sanaaa yaani.
 
Jina rasmi la wimbo la huo wimbo,unaitwa #Nguvu zake mwenyewe,upo kwenye albam no. 9 (Vol.9) ya Seven Survival "Juma Mpogo".Njoo what's up kwa 0713963812 nitakutumia
 
Mkuu Namichiga kuna wimbo nimeusahau Ila unaimbwa hivi "nilipokueleza kuwa nataka kuoa, sura ukakunja utadhani nimekutukana,, sio hivyo mama Sheria ya ndoa naelewa Mungu kapanga watatu kuoa, usinitoshe bwana utakapo kwenda nenda"
Wameimba Nani hiyo nyimbo? Na kama kuna uwezekano naomba unitumie kwenye 0717305301 whatsappp

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Hivi kuna tofauti kati ya chakacha na mchiriku?
Ndio,ipo tofauti kati ya Chakacha na Mchiriku.
Chakacha kiuhasilia ni mziki uliokuwa na mienendo,midundo na tamaduni za kimwambao,ambapo kwenye vifaa vya upigaji wake walichanganya magitaa,pamoja na vinanda vya kuvuta huku wakiwa na madensa (wachezaji) walioitwa mafaruku ambao uchezaji wao ilileta tafsiri ya ubaasha ndani yake.

Jambo hilo la mziki wa Chakacha kuwa na tamaduni za ubaasha ndani yake ndio ilikuwa sababu ya serikali kuupiga marufuku.Hivyo makundi mengi ya mchiriku yalipoanzishwa yalipunguza au kuongeza vitu ili kujiweka tofauti na mziki wa chakacha.

Hivyo basi kiufupi tunasema kwamba Mchiriku ni mziki uliotoka ubavuni mwa Chakacha kwa muundo wa vifaa vya upigaji.
 
Mkuu Namichiga kuna wimbo nimeusahau Ila unaimbwa hivi "nilipokueleza kuwa nataka kuoa, sura ukakunja utadhani nimekutukana,, sio hivyo mama Sheria ya ndoa naelewa Mungu kapanga watatu kuoa, usinitoshe bwana utakapo kwenda nenda"
Wameimba Nani hiyo nyimbo? Na kama kuna uwezekano naomba unitumie kwenye 0717305301 whatsappp

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Mkuu,huo wimbo unaitwa #Mama Tishi.Umeimbwa na band ya Survivor Original kwenye albam yao ya kwanza (Vol.1) mwaka 97.
 
Ndio,ipo tofauti kati ya Chakacha na Mchiriku.
Chakacha kiuhasilia ni mziki uliokuwa na mienendo,midundo na tamaduni za kimwambao,ambapo kwenye vifaa vya upigaji wake walichanganya magitaa,pamoja na vinanda vya kuvuta huku wakiwa na madensa (wachezaji) walioitwa mafaruku ambao uchezaji wao ilileta tafsiri ya ubaasha ndani yake.

Jambo hilo la mziki wa Chakacha kuwa na tamaduni za ubaasha ndani yake ndio ilikuwa sababu ya serikali kuupiga marufuku.Hivyo makundi mengi ya mchiriku yalipoanzishwa yalipunguza au kuongeza vitu ili kujiweka tofauti na mziki wa chakacha.

Hivyo basi kiufupi tunasema kwamba Mchiriku ni mziki uliotoka ubavuni mwa Chakacha kwa muundo wa vifaa vya upigaji.
Asante mkuu. Nilikuwa nimeghafilika kidogo, kumbe chakacha nilikuwa naijua kiundani.
 
kugombana mi siwezi kwa sababu ya mapeenzi hii nyimbo kaimba nani
 
Salamu, Kuna mnanda wa jack simela unaitwa DOLA MIA kama unao nauomba, nimetafuta sana kule mjini YouTube sijauona
 
Back
Top Bottom