mbu wa dengue
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 8,860
- 11,554
Kiwanda ni kitu complicated sana mkuu,unatakiwa kufungua kiwanda baada ya kumiliki biashara kadhaa zikakutajirisha ndio sasa unaamua uadvance na kuanzisha kiwanda wakati huo Akaunti yako inasoma atleast 500m+kwa 20m jamaa anaweza fungua kiwanda kidogo after 5years akawa mbali kuliko kwenye hardware.
Kuanzisha kiwanda kwa mtaji wa 20m ni kujitesa tu maana hiyo watu wa TBS na NEMC wakikutikisa kidogo tu hicho kihela kinapukutika chote unabaki na zero balance,hapo bado hujalipa kodi TRA,bado hujalipa mishahara wafanyakazi,bado hujalipa kodi ya eneo la kiwanda,bado hujalipa bills hapo ni kujikondesha tu.
Biashara ya hardware ni nzuri sana kwa mtu mwenye mtaji wa 20m na bado iko na demand hata kwa Dar es salaam kwa maeneo mapya yanayojengwa kama Goba,Madale,Chanika,Kigamboni,Kibamba,Mpiji,Mbezi msumi.
Ni biashara ambayo hesabu zake ni nyepesi na faida ya bidhaa unaweza kuuza mara mbili ya bei uliyonunulia na bado wateja wananunua hakuna kulialia.
Mbao uliyonunua kwa elfu 8 unaweza ukaiuza kwa elfu 15 na hakuna wa kukuuliza wala kukulaumu kwa sababu hakuna bei maalumu au hakuna bei elekezi ya mbao so kila mmoja anauza kwa bei anayotaka.
Bidhaa yoyote inayohusu mambo ya ujenzi inalipa iwe plumbing materials,electrical materials au building construction materials.
Mimi nakumbuka wakati nataka kufanya wiring kwenye nyumba yangu nilifanya kitu kimoja nilimwambia fundi wangu aniandikie list ya electrical wiring materials yote yanayohitajika kisha nikachukua ile karatasi nikaenda nayo kwenye duka kubwa maarufu la wapemba fulani nje ya mji karibu na ninapoishi nikawaambia wanipigie hesabu gharama ya materials Total ilikuja 2m,nikaondoka na ile karatasi hadi kariakoo kwenye maduka makubwa ya electrical materials nikawapa ile karatasi wanipigie hesabu ya gharama jumla ikaja kwenye 1.2m hapo umegundua nini?
Maana yake wale wenye duka nilipoenda mwanzoni kama ningenunulia pale wangepata faida ya laki 8 kwa mteja mmoja tu sasa jiulize kwa siku wanapata wateja wangapi na wanaingiza faida kiasi gani?