Niulize kuhusu biashara ya hardware, nitajibu kwa uwezo wangu

Niulize kuhusu biashara ya hardware, nitajibu kwa uwezo wangu

Mimi nahitaji kufungua hardware hapa dar lakini kila nikifikiria location napata changamoto kusema niweke wapi nlikua naomba mawazo niwapi naweza wela hardware kwa hapa dar mimi kama kijana?!!
 
Maisha ni ujenzi boss, pale unapokaa geto ukitaka kuweka pazia utahitaji screws na fisherplugs na star ya kufungia, hadi mtaani majengo na vitu vinaharibika kila siku, vifaa vya ufundi vya kichina vina haribika mapema,

Miji inakuwa kila siku...

Bidhaa za ujenzi haziozi, so price inabaki pale palle bila kuweweseka

Pia faida ni nzuri katika kila bidhaa
Vitu vipi vya kuzingatia unapotaka kufungua hardware?
 
1. Weka misumari inchi 2.5, 3 na 4 hata mfuko miwili miwili wa kilo 18,20 au 45.

2. Weka misumari ya ceiling hata kilo kama hapo juu.
3. Weka vifaa muhimu vya mafundi ujenzi.
4. Weka vifaa muhimu vya umeme
5. Weka vifaa muhimu vya bomba
6. Weka cement , white cement, chokaa na wall putty hata mifuko 100, 50, 50, 50 mtawalia.
7. weka vifaa vya usafi kama yote.
8. Weka mabomba ya PVC kadhaa Kwa size kadhaa pia(diameter)
9. Weka paints za emulsion, white, cream.
10. Weka nondo za 12mm, 16mm, 8mm hata tani moja kwa jumla.
11. Weka steel conduits/ducts kwa size mbali mbali.
12. Weka plastic conduits kwa ajili ya kuuza na vifaa vya umeme.
13. Weka nyaya maarufu za umeme. Hata roller nne none.
14. Weka Wires kama vile binding wire, kench wire, chicken wire, draft wire.
15. Weka ceiling board , Gypsum boards.
16. Weka red oxide za lita moja, nusu Lita na za Lita 4 kadhaa
(mfumo wako)
17. Weka ceramics kama vile sinks za vyoo, kunawia etc.

(Hapo Duka linakuwa tayari), wewe sasa utaendelea kifuatilia wateja wanataka nini halafu unapeleka nguvu huko kutegemeana na location.
Hii comment nzuri sana
 
Boss cha kwanza hardware ni term pana sanaa..

Ukitaka uwe na hardware ambayo ni:

general hardware (handtools, appliances, power tools, materials za ujenzi, plumbing na sanitary)..yani mtu hakosi kitu..kama unaanza itakubidi uwe na kibubu cha 80million to 150million na zaidi

Plumbing na sanitary system: tenga 25million hadi 30million

Mchanganyiko wa vitu vidogo: Handtools, appliances ndogo(vitasa, komeo,), fixets kama screws, bolts etc, vifaa vya vidogo vya mafundi 25million to 35million,

Yenye Materials za ujenzi tu: kuanzia foundations hadi fiinishing 50 to 100million

Au unaweza kufanya cheat code kwa mtaji mdogo kwa kumix kidogo kidogo hivyo vyote hapo juu kidogo kidogo ila kuna bidhaa utamiss dukani ..35miillion

Kama ni mbao tu 15m to 25m
Nafwatilia huu Uzi kwa ukaribu mkuu.
Zipi changamoto common za hii biashara? vipi kuhusu vitabu vya records Auditing Mara ngap au at the end of the year inatosha?
 
Personally nimefaidika na madini mengi humu JF kwa ajili ya maswala mbali mbali, sio vibaya na mimi kushare info na wana jamii wafaidike pia.

Nimekulia katika familia yenye b'ness ya hardware, then na mimi nikajikita katika b"ness hio hio.

Nitashare kutokana na uzoefu, uwezo na kiwango cha ujuaji wangu.

Karibuni na wengine mtakao kuwa na majibu kwa wengine.
Safi aiseee
 
Hii comment nzuri sana
Ningependa kujua mkuu, je frame ya duka la hardware inatakiw iweje maan naonaga mara nying wenye maduka ya hardware wana frame kuanzia mbili mpaka tatu sehem moja kwa ajil ya store je kam unaanz hii imekaaje
 
Nimeusoma uzi wote, ni mzuri,

Kuna siku na mm nitakuwa na uzoefu wa hii biashara nitakuja na majibu, wacha nipambane na mm niifungue
 
Personally nimefaidika na madini mengi humu JF kwa ajili ya maswala mbali mbali, sio vibaya na mimi kushare info na wana jamii wafaidike pia.

Nimekulia katika familia yenye b'ness ya hardware, then na mimi nikajikita katika b"ness hio hio.

Nitashare kutokana na uzoefu, uwezo na kiwango cha ujuaji wangu.

Karibuni na wengine mtakao kuwa na majibu kwa wengine.
Ningeomba unifafanulie ishu kuhusu TRA, service levy na leseni ya biashara. Naona kama serikali inakwapua faida yote. Nipo napambana kujichanga ili nianzishe hii business

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Uzi mzuri,
Hiv mkuu Forrest Gump, upande wa electricals tu inahitaji mtaji wa sh ngapi hiv ?
 
Back
Top Bottom