Sigara Kali
JF-Expert Member
- May 28, 2017
- 3,727
- 8,785
Uliza chochote kuhusu ugonjwa sugu wa Figo na matibabu ya dialysis nipo hapa kukujibu
Visababishi vikuu vya kufeli kwa Figo ni presha ya juu isiyodhibitiwa pamoja na kisukariNi vitu gani vinachangia au kusababisha mtu kupata ugonjwa sugu wa figo mkuu!
Dodoma pale BMH,Bugando,Muhimbili,KCMCFistula dialysis inafanyika wapi hapa bongo
Nina maswali kadhaa ya kuuliza;Visababishi vikuu vya kufeli kwa Figo ni presha ya juu isiyodhibitiwa pamoja na kisukari
Unasema? 🤔Dodoma pale BMH,Bugando,Muhimbili,KCMC
Yes mkuuUnasema? 🤔
1. Ugonjwa wa figo mara nyingi unakuja kimya kimya hadi kuja kugundulika tayari Figo zimefikia hatuna mbaya ya kushindwa kufanya kazi mara nyingi stage 4 mpaka 5Nina maswali kadhaa ya kuuliza;
1. Hua inachukua muda gani kwa mgonjwa kubainika kwamba figo zake hazifai tena kwa hio inabidi apate figo zingine?
2. Matibabu ya figo huchukua muda gani mpaka mgonjwa kupona kabisa?
3. Je! Mgonjwa wa figo ambae amepata matibabu na kuweza kupona kabisa yupo hatarini kiasi gani kuugua tena ugonjwa wa figo?
4. Imekua ikisemekana kwamba uvutaji wa Sigara ndio kitu kwa asilimia kubwa kinachochangia kwa kiasi kikubwa ugonjwa wa figo pamoja na saratari, je! kuna ukweli kiasi gani kuhusu hilo? Ni kweli Sigara zinaua figo?
5. Je! Nikibainika kwamba ninaugua ugonjwa wa figo ni kitu gani natakiwa kukifanya mwanzoni ili kuweza kufanya figo zisiangamie zaidi na kutoweza kufanya kazi kaabisa?
Mtu anaweza kufanyia Dialysis na maisha yake yakaendelea vizuri kama kawaida kama wengine ambao hawaumwi figo ?
Je wanaruhusiwa kunywa maji ? Au kula vyakula vyenye maji ?
1. Ugonjwa wa figo mara nyingi unakuja kimya kimya hadi kuja kugundulika tayari Figo zimefikia hatuna mbaya ya kushindwa kufanya kazi mara nyingi stage 4 mpaka 5
2. Figo zikifeli Tiba zake kuu ni 2 tu dialysis ambayo hii inasogeza maisha mbele na si kuponesha Figo, Tiba ya kudumu ni kupandikiza Figo nyingine yenye afya, mara nyingi ukiwa kwenye CKD stage 4 au 5 huponi zaidi ya kufanya dialysis au transplant. Kidney failure unayoweza kupona ni Ile Acute kidney Injure zinafeli kwa muda the ulifanya dialysis mara kadhaa zinarudi Tena kuendelea kufanya kazi
3. Ni wagonjwa wachache sana ambao walikua na CKD wakapona maana wengi wanahisi wamepona ila baada ya mwaka 1 au 2 hali inarudi Tena ,so kwa ufupi mgonjwa wa CKD ambaye amefika hatua ya kufanya dialysis wengi hawaponi wanaendelea na dialysis maisha yao yote. Wale wanaopona ni waliopatwa na AKI( Acute Kidney Injury)
4. Chanzo kikuu Cha kufeli kwa Figo High blood pressure isiyodhibitiwa kwa muda mrefu pamoja na kisukari. Uvutaji wa sigara unachochea uwepo wa hayo magonjwa Yani kisukari na High blood pressure so uvutaji wa sigara hausababishi kufeli kwa Figo Moja kwa moja Bali kunachochea chanzo Cha kufeli kwa Figo ambako ni BP na kisukari
5. Ukigundulika una shida ya Figo inategemea na stage uliyogunduliwa nayo maana kuna stage 1-5 ambako hii ya 1-3 ni ngumu sana kujua dalili zake labda tu kama utakua mtu wa kupenda kupima pima. Mara nyingi watu wengi wanagundulika wakiwa stage ya 4 au 5 ambazo zonaonesha dalili mbaya so hapo unachotakiwa kufanya ni kuanza dialysis na kutumia dawa either za presha au sukari maana inategemea kisababishi kikuu ni nini na suluhisho la kudumu ukigundulika na ugonjwa wa kufeli kwa Figo stage 4 au 5 ni kupandikiza Figo nyingine. Na hata ukianza dialysis Ile kazi kidogo ya Figo lliyobaki nayo inaisha kadri miaka ya kufanya dialysis inavyoendelea
Mgonjwa wa figo anayefanyiwa Dialyisis anaweza "Kupiga Mashine" kama kawaida?Ndio mkuu Mfano mzuri ni Mimi mwenyewe nipo kwenye dialysis mwaka wa 3 naendelea na maisha yangu kama kawaida na shughuli zangu za Kila siku.
Kuhusu maji wanaruhusiwa kunywa ila inategemea na kiasi Cha mkojo unachotoa. Kwa kawaida
wale wagonjwa ambao hawakojoi kabisa wanashauriwa watumie vimiminika vyote kwa siku isizidi 500mL hapa inamaanisha maji,chai,juice na vimiminika vingine
At least Kila baada ya miezi mitatu au sifa inafaa kupima hali ya mwiliJe ni vizuri kupima kila baada ya muda, hata kama huumwi ila ile kupima figo tu kama zipo salama au lah
Ndio anapiga mashine kama kawaida ila kadri siku zinavyokwenda hamu inaisha maana unakua unakabiriwa na stress nyingi na changamoto za hapa na pale za ugonjwaMgonjwa wa figo anayefanyiwa Dialyisis anaweza "Kupiga Mashine" kama kawaida?
Okay mkuu.Ndio anapiga mashine kama kawaida ila kadri siku zinavyokwenda hamu inaisha maana unakua unakabiriwa na stress nyingi na changamoto za hapa na pale za ugonjwa
Ni vizuri mkuu kupima afya yako angalau mara moja kwa mwaka na sio kuhusu figo tu bali na magonjwa mengine eg presha,kisukari, meno uchunguzi wa saratani etc. Mojawapo ya sababu kwanini Afrika tunakufa mapema ni kukosa utamaduni wa kucheki afya wakati mwili ukiwa haujaonesha dalili za kuumwa tofauti na nchi nyingine ambapo ni utamaduni mtu kupima afya yake angalau mara moja kila mwaka. Mfano mzuri Papa Leo XIV,amepona saratani ya pafu kwa sababu iligunduliwa akiwa mzima haumwi chochote na hata matibabu yake yalikuwa rahisi, ingekuwa hapa Bongo angeenda hospital kansa ikiwa ishakuwa kubwa na kifuatacho baada ya hapo ni kifo. Ila Papa Leo XIV sasahivi anadunda kama sio yeye aliyekuwa mgonjwa wa saratani wiki chache zilizopita.Je ni vizuri kupima kila baada ya muda, hata kama huumwi ila ile kupima figo tu kama zipo salama au lah