Niulize kuhusu ugonjwa sugu wa Figo(CKD) na dialysis

Niulize kuhusu ugonjwa sugu wa Figo(CKD) na dialysis

Una ushauri gani unaosaidia figo kuendelea kuwa kwenye hali nzuri na kuepusha uwezekano wa kupunguza ufanisi wake na mwisho kushindwa kabisa kufanya kazi?
1. Dhibiti presha na kisukari maana ndo vinaongoza kwa kuua figo.
2. Cheki afya ya figo kila mwaka ili kama zina shida igunduliwe mapema kabla ya kufikia stage mbaya. Figo huwa zinapata shida polepole huku mtu hajijui,siku akianza kuonesha dalili tayari hali ishakuwa mbaya.
3. Usitumie dawa hovyo hovyo haijalishi ni za hospital au za kienyeji.
 
Ni vizuri mkuu kupima afya yako angalau mara moja kwa mwaka na sio kuhusu figo tu bali na magonjwa mengine eg presha,kisukari, meno uchunguzi wa saratani etc. Mojawapo ya sababu kwanini Afrika tunakufa mapema ni kukosa utamaduni wa kucheki afya wakati mwili ukiwa haujaonesha dalili za kuumwa tofauti na nchi nyingine ambapo ni utamaduni mtu kupima afya yake angalau mara moja kila mwaka. Mfano mzuri Papa Leo XIV,amepona saratani ya pafu kwa sababu iligunduliwa akiwa mzima haumwi chochote na hata matibabu yake yalikuwa rahisi, ingekuwa hapa Bongo angeenda hospital kansa ikiwa ishakuwa kubwa na kifuatacho baada ya hapo ni kifo. Ila Papa Leo XIV sasahivi anadunda kama sio yeye aliyekuwa mgonjwa wa saratani wiki chache zilizopita.

Mimi huwa napima magonjwa madogo madogo tu, itabidi kweli nianzishe huo utamaduni
 
Mtindo wa maisha, ulaji na ufanyaji mazoezi. Linganisha walivyokuwa wanakula kizazi cha 80 kurudi nyuma na sisi tunavyokula sasahivi utaelewa kwanini presha na kisukari vimekuwa majanga kwetu.

Kama mtu ana presha ya juu tayari na huwa anasema anabanwa kifuani lakini hospitali amepewa dawa nyingi sana na kila siku anapaswa kunywa dawa zaidi ya tatu je ndo anazidisha hayo magonjwa?
 
1. Dhibiti presha na kisukari maana ndo vinaongoza kwa kuua figo.
2. Cheki afya ya figo kila mwaka ili kama zina shida igunduliwe mapema kabla ya kufikia stage mbaya. Figo huwa zinapata shida polepole huku mtu hajijui,siku akianza kuonesha dalili tayari hali ishakuwa mbaya.
3. Usitumie dawa hovyo hovyo haijalishi ni za hospital au za kienyeji.
Ahsante kwa majibu mazuri mkuu.

Ambapo tunarudi tena kwenye namna ya kuthibiti kisukari na presha.

Unamapendekezo yoyote ya mfumo wa maisha unaoweza kusaidia kuepukana na presha na kisukari?
 
1. Ugonjwa wa figo mara nyingi unakuja kimya kimya hadi kuja kugundulika tayari Figo zimefikia hatuna mbaya ya kushindwa kufanya kazi mara nyingi stage 4 mpaka 5
2. Figo zikifeli Tiba zake kuu ni 2 tu dialysis ambayo hii inasogeza maisha mbele na si kuponesha Figo, Tiba ya kudumu ni kupandikiza Figo nyingine yenye afya, mara nyingi ukiwa kwenye CKD stage 4 au 5 huponi zaidi ya kufanya dialysis au transplant. Kidney failure unayoweza kupona ni Ile Acute kidney Injure zinafeli kwa muda the ulifanya dialysis mara kadhaa zinarudi Tena kuendelea kufanya kazi
3. Ni wagonjwa wachache sana ambao walikua na CKD wakapona maana wengi wanahisi wamepona ila baada ya mwaka 1 au 2 hali inarudi Tena ,so kwa ufupi mgonjwa wa CKD ambaye amefika hatua ya kufanya dialysis wengi hawaponi wanaendelea na dialysis maisha yao yote. Wale wanaopona ni waliopatwa na AKI( Acute Kidney Injury)
4. Chanzo kikuu Cha kufeli kwa Figo High blood pressure isiyodhibitiwa kwa muda mrefu pamoja na kisukari. Uvutaji wa sigara unachochea uwepo wa hayo magonjwa Yani kisukari na High blood pressure so uvutaji wa sigara hausababishi kufeli kwa Figo Moja kwa moja Bali kunachochea chanzo Cha kufeli kwa Figo ambako ni BP na kisukari
5. Ukigundulika una shida ya Figo inategemea na stage uliyogunduliwa nayo maana kuna stage 1-5 ambako hii ya 1-3 ni ngumu sana kujua dalili zake labda tu kama utakua mtu wa kupenda kupima pima. Mara nyingi watu wengi wanagundulika wakiwa stage ya 4 au 5 ambazo zonaonesha dalili mbaya so hapo unachotakiwa kufanya ni kuanza dialysis na kutumia dawa either za presha au sukari maana inategemea kisababishi kikuu ni nini na suluhisho la kudumu ukigundulika na ugonjwa wa kufeli kwa Figo stage 4 au 5 ni kupandikiza Figo nyingine. Na hata ukianza dialysis Ile kazi kidogo ya Figo lliyobaki nayo inaisha kadri miaka ya kufanya dialysis inavyoendelea
Unakazana na Stage 4-5. Ongelea 1-3
 
Kama mtu ana presha ya juu tayari na huwa anasema anabanwa kifuani lakini hospitali amepewa dawa nyingi sana na kila siku anapaswa kunywa dawa zaidi ya tatu je ndo anazidisha hayo magonjwa?
Afuate ushauri wa daktari wake,kama ana swali lolote amuulize daktari wake. Asiache dawa bila ushauri wa daktari.
 
Ahsante kwa majibu mazuri mkuu.

Ambapo tunarudi tena kwenye namna ya kuthibiti kisukari na presha.

Unamapendekezo yoyote ya mfumo wa maisha unaoweza kusaidia kuepukana na presha na kisukari?
Ulaji wetu, kula vyakula vyenye mafuta na sukari kidogo,vyakula vya kusindika na vyenye mafuta mengi eg chipsi na soda visiwe utamaduni wetu. Pia kupima mara kwa mara ili kama ukigundulika una shida hatua ianze kuchukuliwa mapema bila kusahau kufanya mazoezi.
.
 
Back
Top Bottom