Niulize kuhusu ugonjwa sugu wa Figo(CKD) na dialysis

Una ushauri gani unaosaidia figo kuendelea kuwa kwenye hali nzuri na kuepusha uwezekano wa kupunguza ufanisi wake na mwisho kushindwa kabisa kufanya kazi?
1. Dhibiti presha na kisukari maana ndo vinaongoza kwa kuua figo.
2. Cheki afya ya figo kila mwaka ili kama zina shida igunduliwe mapema kabla ya kufikia stage mbaya. Figo huwa zinapata shida polepole huku mtu hajijui,siku akianza kuonesha dalili tayari hali ishakuwa mbaya.
3. Usitumie dawa hovyo hovyo haijalishi ni za hospital au za kienyeji.
 

Mimi huwa napima magonjwa madogo madogo tu, itabidi kweli nianzishe huo utamaduni
 
Mtindo wa maisha, ulaji na ufanyaji mazoezi. Linganisha walivyokuwa wanakula kizazi cha 80 kurudi nyuma na sisi tunavyokula sasahivi utaelewa kwanini presha na kisukari vimekuwa majanga kwetu.

Kama mtu ana presha ya juu tayari na huwa anasema anabanwa kifuani lakini hospitali amepewa dawa nyingi sana na kila siku anapaswa kunywa dawa zaidi ya tatu je ndo anazidisha hayo magonjwa?
 
Ahsante kwa majibu mazuri mkuu.

Ambapo tunarudi tena kwenye namna ya kuthibiti kisukari na presha.

Unamapendekezo yoyote ya mfumo wa maisha unaoweza kusaidia kuepukana na presha na kisukari?
 
Unakazana na Stage 4-5. Ongelea 1-3
 
Kama mtu ana presha ya juu tayari na huwa anasema anabanwa kifuani lakini hospitali amepewa dawa nyingi sana na kila siku anapaswa kunywa dawa zaidi ya tatu je ndo anazidisha hayo magonjwa?
Afuate ushauri wa daktari wake,kama ana swali lolote amuulize daktari wake. Asiache dawa bila ushauri wa daktari.
 
Ahsante kwa majibu mazuri mkuu.

Ambapo tunarudi tena kwenye namna ya kuthibiti kisukari na presha.

Unamapendekezo yoyote ya mfumo wa maisha unaoweza kusaidia kuepukana na presha na kisukari?
Ulaji wetu, kula vyakula vyenye mafuta na sukari kidogo,vyakula vya kusindika na vyenye mafuta mengi eg chipsi na soda visiwe utamaduni wetu. Pia kupima mara kwa mara ili kama ukigundulika una shida hatua ianze kuchukuliwa mapema bila kusahau kufanya mazoezi.
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…