Shida na raha
JF-Expert Member
- Aug 8, 2014
- 3,773
- 3,471
- Thread starter
-
- #201
Unajua shida ni kwamba kila mtu hapendi mtoto wa mwenzie akifanikiwa hapo ndo penye utata. Ukiona mtu kafanikiwa basi nyuma yake kuna mengi aliyopitia na kuyakwepa kuhusiana na husda za watu. Na ndio maana mimi sitaki hata kwenda nyumbani ni mwendo kwenda kuchungulia siku tatu ya nne narudi.Pole sana.
Kwa hiyo hata kupata kazi tu ilikuwa kwa mbinde ili na watu walikuwekea vizingiti ukipata kazi pesa utakayoipata iishe bila wewe kujua umefanyia kazi gani.
Walimwengu wana mambo
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siku nilimwambia mfanyakazi mwenzangu mara nikienda Pemba naenda na usafiri wangu kusudi nisipate shida kipindi cha likizo... Akaniuliza " unaenda kukaa siku ngapi? " nilimjibu siku 4 ya 5 narudi.. Alisikitika sana na kunambia niache kabisa huo mchezo maana watu wataenda kuhisi nawaringishia wakati sio lengo langu. Na kweli yaliniingia akilini maana kukaa siku 4 halafu ukarudi na usafiri wako mara hukutupia jini ukaishia kulala kitandani, kwa ufupi watu hawana wema..
Kuna mwalim mmoja alijitolea kuweka bomba watu wafaidike maana palikua na shida ya maji.. Yule mwalim baada ya kuona watu wanafanya vurugu akaamua kuutoa, basi watu baada ya kuona vile wakaoana kana kwamba kawafanyia makusudi.. Juzi nikapewa taarifa na mdogo wangu kwamba mwalim huyo wamemlaza kitandani na kaparalaiz na pia hawezi kusema..
Sio huyo tu... Wapo wawili wanekuwa mabubu na wote nawafaham yaani kuna siku nilikwenda likizo nilitaka kutokwa na machozi kwa jinsi yule mtu walivomfanya.
Sent using Jamii Forums mobile app