Niulize swali lolote kuhusiana na wapemba na Pemba yenyewe..

Niulize swali lolote kuhusiana na wapemba na Pemba yenyewe..

Huku dar
Nyumba ina mama,watoto wa kiume na kike watoto wa kiume wameoa wapo hapo hapo na ndugu wengine kibao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Utaratibu huu sio tu wapemba hata wahindi na waarabu wanao.... wenzetu wana umoja sana, wanaishi pamoja lakini wanachangishana unakuta wanachanga ili kumnunulia au kumjengea mmoja wao nyumba wakimaliza na huyu anafata mwingine hivyo hivyo kuja kutahamaki wote wana nyumba wanahamia makwao, au unakuta wao wanachanga kwa ajili ya kununua gari wanahakikisha kila mtu atapata gari....

Pesa wanapata wapi? wanavyoishi pamoja ile pesa badala ya kulipa kodi wao wanachangishana kwa ajili ya kufanya hayo maendeleo.

Pia wanafundishwa upendo, umoja na mshikamano ndio maana hawatupani, popote duniani wakikutana basi wao ni ndugu na watashirikiana na hawadhulumiani.

Sent from Jamii Forums using siemens kidole juu.
 
Zamani zao lililoshamiri sana ilikua...
Uwele, mpunga, mbaazi, kunde na mtama kwa wingi sasa hivi ni hafifu sana.. Wanalima mihogo lakini sio zao kuu..

Kwa ufupi Pemba tunaumizana wenyewe kwa wenyewe (husda).. Ukianza kuneemeka kidogo inakubidi uwe mshirikina tofauti na hapo utaishia kufa huku unajiona.
Mi binafsi naenda likizo nakaa siku tatu mpaka nne nageuza maana hawachelewi kunilaza kitandani kweupeee.
Mpemba ambae hajafanya shiriki ni yule anaeishi nje ya Pemba. Mi binafsi nina mganga wangu maalum maana misuko suko ninayoipata naijua mwenyewe.. Na kila nikienda likizo lazima nikamsalimie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Misuko suko ipi uliyopitia na kwa mini umeihusisha na ushirikina?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom