Hello guys...
Hope U mzima...
:TruE stoRy:
Ilipoishia................~\
Nilipofika pale Ubungo terminal,
nilihakikisha ninaripoti sehemu husika, yeah' nilisubuli muda na muda ulipotimia, niliingia ndani ya basi uku nikijishauri....
au niludi....[ @£$ ] nikajisemea mwenyewe" huwenda wachawi wameshajua kuwa' nakwenda kuzoa mipesa huku na ndio maana nafsi inakuwa nzito!.
Sasa tuendelee..................¥
Taratibu basi lilianza kutoka kwenye lango kuu la pale Ubungo terminal, tayari kuiyanza safari ya kelekea nchini Zimbabwe.
Kwa bahati nzuri' nilipata siti iliopo dirishani nyuma ya dereva,
Hivyo' niliutazama kwa makini mji wangu wa Dar es salaam...
nikahisi kuwa huwenda nitaumisi
siku moja.
Nilivuta pumzi kubwa tu' then nikaegemea siti yangu...uku nikitafakali yatakayojili huko niendako.
Baada ya muda mchache kupita,
mji wa Dar es salaam tuliupa mgongo na hatimae tukaendelea kuchanjambuga
uku tukisikilizia changalawe zinavyogonga kwenye bodi ya gari, na wazee wa tochi A K A
dereva shuka uje unipe hela ya chai....hawakosi njiani hahaha
Tanzaniano bhana!
Masaa yaliyoyoma, na hata tukafika mahala fulani' hapo..
pana restaurant < mgahawa >
so' wengi wetu tuliteremka...
wengine walikwenda kula, na wengine walikwenda kuchimba dawa....
Mimi niliingia mule ndani ya restaurant...nikanunua chakala' baada ya hapo nikatafuta sehemu tulivu na makamuzi yalifuata.
Punde tu' alikuja jamaa mmoja na yeye ni *mtanzania* akanipa Hi' kisha akaketi pembeni yangu,
Akaniuliza*-* unaelekea wapi jamaa yangu?
Nikamjibu: naelekea kwa Madiba hapo!
Akaniuliza*-* mji gani huko kwa Madiba?
Mi sikusita' ilibidi nimchane tu...
nikamwambia brother..me nakwenda nisikokujua, pia huko' sina ndugu, rafiki wala sijui nitafikia wapi, mji gani actually
I don't know...
Akasema: dah! mimi pia nakwenda hukohuko..ispokuwa' me nakwenda mji wa Johannesburg...na ndio mara yangu ya kwanza pia!.
Akaendelea kwa kusema:
km vp...wewe usiwaze" me nitamwendea hewani B'mkubwa wangu..nimfahamishe kuwa kuna mtu nakuja nae..coZ' yeye anaishi huko South" pia hana noma...........
Dah!..kwakweli nilijihisi ni mtu mwenye bahati kiasi flani...hata stress zangu zilipungua makali.
Nilimshukulu sana aisee...
nikamuitikia' poa brother nashukulu kaka....
Haikuchukua muda" alikuja jamaa mwengine pale tulipoketi sisi wawili..akatupa Hi'...kisha akaketi pamoja nasi...nayeye ni
*mtanzania* pia.
Tukaulizana maswali mawili matatu pale...tukafahamiana kwa uchache..na hatimae muda wa mapumziko ulikwisha...hivyo'
sote tulirejea kwenye lile basi,
na safari iliendelea!
Hapa" ifahamike kuwa sisi sote wa 3...hatukuwa wenye kujuana.
Hakika safari ilikuwa ni ndefu sana....story mchanganyiko ndani ya basi kama kawa..
Na wale wakuchart....
wanaperuzi tu mwanzo mwisho!
Kasheshe kwa wenye Tigo, hahaha...lol
Kwakweli safari ilikuwa ndefu mno' na hata majuto yalianza kuingia ndani ya nafsi zetu kwa kujilaumu...kwanini tumepanda basi badala ya Fast jet *ndege*
pale tu' tulipoanza kukata tamaa
ndipo tukauwona mji wa Tunduma...sambamba kabisa na border ya Tanzania na Zambia.....
Kama sikosei, ilikuwa kwenye mishale ya saa 3~4~5 usiku tulipowasili Tunduma,
Hapo' wengi wetu tuliteremka na wengine walikuwa wameshafika makwao, wengine walichukua usafili wmingine kawa haraka zao,
Mimi na wale jamaa zangu wawili, tuliingia ndani ya bar flani ya palepale border *Tz*
Nakumbuka kulikuwa na balidi kali sana siku hiyo, baC' tulibadilishana mawazo mule ndani ya Bar...kusema kweli mimi na yule brother wangu wa kwanza..*-* ..hatukuwa walevi ispokuwa yule jamaa mwengine' yeye alisema anapasha koo+
Kwa upande wangu..nilishindwa kustahmili lile baridi..hivyo' niliingia ndani ya lile basi..punde tu' jamaa zangu nao waliingia ndani ya basi, tukaupiga usingizi wa sungura!.
Asubuhi kulipopambazuka, harakati za kugonga *Visa* zilianza chapchap, hapa ndipo
nilipoukumbuka ule msemo wa yule baalia wangu wa kitaani..
#watanzania_wakuda_sana..
Picha linaaza" pale reception, wananiambia nikabadilishe nguo, nikachukulia poa,
Hiiiii...naludi' nakuta watu wanalalamika eti zimezuiliwa passport zao...dah! nilikuwa na hasira....
Walichokifanya, ni kuweka mianya ya utoaji rushwa...yaani ili ugongewe visa, ni lazima utoe pesa kidogo...walivyo [HASHTAG]#washenzi[/HASHTAG]
Hawataki Shillings, wanataka Dollars...otherwise itakula kwako.
Kishingo upande..ilibidi nitoe visenti vyangu nikawapa...ili kuepusha maharagwe yangu yasichache bure!
Baadae..walipanda abiria wengine kutokea palepale border...wengine walikuwa wana kwenda Zambia wengine Zimbabwe...shida tupu!
Taratibu..basi lilianza kuikanyaga ardhi ya Zambia tayari kuiyanza safari.
Kwenye siti yangu nilikaa mimi na mzungu flani ambae yeye safari yake ilianzia pale border
Tz & Zm,...
Sikuacha kujishobokesha kwa yule mzungu...ingawa lugha ngongano...lkn sikusita...pia nilimwambia ukweli kuwa mimi si mtaalam wa lugha, akanielewa...so' story ziliendelea.
Kumbuka wale jamaa zangu, wapo siti za nyuma.
Masaa yalikatika...nuru ya jua nayo ilituama, kiza kikatanda, sikumbuki ilikuwa saangapi' hatimae basi lilikwenda kupaki mahali flani...hapo tayari..tulishaikalibia border ya Zambia na Zimbabwe.....
Tuliteremka, palikuwa hapaeleweki sana..sijui kuna kambi ya jeshi...sijajua!
Ilikuwa ni usiku nakumbuka...
hapo, wengine walioga, wengine walifua baadhi ya nguo zao...kisha tukaupiga usingizi wamaana aisee!
Asubuhi, kulipopambazuka..
mdogomdogo...safari ilianza' kuelekea border...
Tulitumia km lisali moja iv' kufika pale border ya Zambia & Zimbabwe...
Tulipofika, tuliteremka abiria wote na kuingia ndani ya ule mjengo...*Home affairs*...
Sasa ile wakati tunashuka, akaja jamaa mmoja ni
*mtanzania* inasadikika yeye aliachwa na basi pale kwenye kugonga Visa *Zambia*
Akatuuliza: oya' munaenda
South .A...?
Sote watatu, tukaitikia' ndio..!
Akauliza tena..ndio mara yenu ya kwanza..?
sote watatu, tukaitikia' ndio..!
Akauliza tena..je' munapesa ya kutosheleza ili mukaonyeshe pale reception..?
Yule jamaa mwengine aliyetufua pale restaurant *Tz*..
akajibu..mimi ninazo za kutosha!
Yule jamaa..akasema, twendeni ndani ya huu mjengo niwasaidie namna ya kujaza vile vipeperushi vilivyopo pale reception.....
Tukaongozana nae mule ndani..
Pia tukapokezana kuzitumia zile pesa kama *show money* pale reception.
Kuanzia pale, yule mkaka akawa ndio kama kiongozi wetu wa msafra mzima...!
Sasa tukaongezeka tukawa...
wanne!
Hakika..tulifaulu na tukatoka nje ya ule mjengo..tukapanda basi..
akiwemo na yule mkaka' kwani yeye aliwasiliana na konda wa basi lake lililomuacha, kuwa apande lile la kwetu.
Safari iliendelea...masaa yalikatika pia..hatimae jioni
basi lilitia timu katika mji wa Harare nchini Zimbabwe..
Hapo sasa basi letu lilifikia ukingoni...|||
Kilichofuata ni yule mkaka alitusaidia kubadili pesa zetu from Shillings, Dollars to Rand,
kwakweli sina hakika kama ajatuibia pale...hahaha lol!
Pia akatusaidia kukata tiketi ya kwenda South *Dizonga*...
Palepale nikamstua yule brother,
kuhusiana na B'mkubwa wake..km vp amvutie waya ili anipunguze mawenge kichwani!
akajibu: poa baalia wangu usiwaze..
Kwa bahati nzuri..tulipoingia ndani ya basi..tukapitishiwa laini za simu *sim card* for free...
Pale' nilimshauri tuweke vocha ili tuwasiliane na B'mkubwa..
Ikumbukwe kuwa...
yule mkaka tuliyekuta nae pale Zambia, ni mwenyeji huko tuendako, na wale jamaa zangu wawili, ni wageni kama mimi' ispokuwa wao, wana wenyeji wao huko South Africa...!
Hivyo' safari ilianza kueleke South .A.
Tulikaa sana njiani nakumbuka,
na hata yule brother wangu nae nilimuona akichart na B'mkubwa
wake...nilianza kupata matumaini ya huko niendako ni salama...nilihakikisha najipendekeza sana kwake ili niupate msaada wake.
Hatimae usiku uliingia, sina hakika sana ila kwenye mishale ya saa 7~8 ya usiku ndipo tulipo fika kitovu cha mwisho panaitawa *Beit bridge*
Hahaha...hapo si mchezo...
Ukifeli kidogo tu...imekula kwako %..
Kwa upande wetu, mambo yalikwenda vyema2..
wala hapakuwa na tabu yoyote
Zoezi lilimalizika asubuhi...
Kwenye saa 4~5...asubuhi taratibu basi lilianza kuyoyoma..
Masaa kadhaa tulianza kujiona tupo nje ya Africa hahaha...
Kaubaridi kanapuliza taratibu,
Jiji safi, nyumba amazing, hata kama simu yako haina flashlight
ukipiga self* kisha ukawatumia washkaji zako na kuwaambia, umeghairi kwenda South .A.
na sasa upo Europe..wataamini kwa %. hahahahah...raha tu.
Saa kumi kasoro ya jioni, basi lilitimba katika jiji la *pretolia*,
Basi letu lilipata itlafu kidogo,
so' abilia wote tulitakiwa tushuke..tuletewe basi lengine.
Sisi wanne kwakuwa tuna haraka, tukashauliana tuchukue daladala..kwa lugha ya kwetu*
kwakuwa tulishushwa stand..tulitembea atua 5 tu, tukaingia ndani ya ile hice
*daladala*..
Njiani nakumbuka yule brother nilimuona akiwasiliana B'mkubwa wake..kisha akaninyooshea dole gumba, kuashilia kuwa nisiwe na wasiwasi mambo yanakwenda level...basi hakika, tabasamu la nguvu lilionekana usoni mwangu, yaani nilikuwa kama mschana aliyeambiwa you are so beautiful...
Kama lisali moja na nusu iv' kupita,..hatimae tukawasili ndani ya Johannesburg *Dizonga*...tukateremka..
Nakumbuka kila mmoja wetu alikuwa akiwasiliana na jamaa yake ispokuwa mimi tu..
Yule jamaa ambae tulizitumia pesa zake pale Zambia...
*show money*, yeye alielekezwa aende wapi' hivyo akaondoka,
Na yule mkaka ambae tulikutana nae pale Zambia..yeye alikaa mbali kidogo na sisi wawili mimi na yule brother,
Yule brother akawasiliana na B'mkubwa..akaambiwa asubili palepale kwakuwa hakuwa mbali na pale tulipo.
Ghafla" yule brother baada ya kumuona tu B'mkubwa wake,
[HASHTAG]#alinigeuka[/HASHTAG] aisee!
Nikaona kama masihala iv'
akaonyesha msisitizo na kusema:
Oya* kama kufika umeshafika jikatae tena!!
Dah!...nikamuuliza kwa mshangao..brother uko serious..au unazingua??
Akajibu kwa ukali..
akasema: kilamtu kimpango
wake tusizoeane bhana!
Aisee' nakumbuka..burg ilinidondoka from ma hand..
nilihisi kudata, palepale nikaanza kutazama yale mazingila ya pale..iasee" ajulikani foreigner wala mzawa,
wote mateja *ngada* tupu.
Nikafikilia kurudi Tz..nikaona haiwezekani, itakuwa jau bhana!
kwanza nauli sina ya kuludia dah!..........
Wakati ule, B'mkubwa alikuwa anaona kinachofanyika pale ila hakuelewa kinachoendelea..
Ilimbidi aje pale tulipo sisi wawili
kisha akauliza:
Kinaendelea kitu gani hapa..??
Yule brother..alikuwa mkali na wala hakutaka kumpa B'mkubwa chance ya kujua kinachoendelea...zaidi' anamwambia apeleke mizigo yake ndani ya gari aliyokuja nayo B'mkuwa..watimke.
Dah!...hakika nilivulugwa sana2,
taratibu niliokota begi langu..
nikimtazama yule mkaka
tulyekuta pale nchini Zambia..,
Nikamuona kwambali anajifanya yuko busy na simu yake...nikatazama yale mazingira nikagundu kuna kamchezo kamechezeka>>
Je' Unajua nilichokifanya pale?
Je' Unahisi nini kitatokea iwapo
B'mkubwa akijua ukweli?
Je' Yule mkaka ni nani, na kwa
nini hakuondoka muda
wote ule?
Gonga likes nyingi...
Then tukutane part 3...
Tooth Brush
#$$$