Kama ilivyo kwa makampuni binafsi, mashirika, na taasisi, pamoja na watu binafsi, wanaweza kuwa katika hatari ya udanganyifu wakati wa kununua bidhaa kutoka nje ya nchi (mtandaoni). Hali kadhalika, kwa wafanyabiashara waendao China, wanapokagua mizigo vizuri wakati wa kupakia kwenye kontena, wanaweza kubadilishiwa bidhaa au kukumbwa na udanganyifu wakati wa malipo mtandaoni. Kabla ya kupokea email kutoka kwa real manufature, then unapokea a same spam email kutoka kwa (hacker)mwizi, na hivyo kusababisha malipo kufanyika kwa taasisi isiyo sahihi. Je, hali hii inaweza kutokea pia serikali, kwa mfano, katika manunuzi ya ndege au SGR, au tenda, au bidhaa nyingine, na kusababisha hasara kutokana na tamaa ya kupata unafuu fulani? Na kama kuna mifano halisi, tafadhali nipe.