Muendelezo,,
Baada ya kuona Jamaa yangu ananiangalia nilibaki nawaza tu nikamuonyeshea ishara ya macho tutoke nje akaomba udhuru tukatoka nje, nikamuuliza nikiwa nimejawa na kiwewe
Sasa hapa tunafanyaje?
Akaniambia nilikuambia ufanyeje?
Niakamwambia sasa kweli gharama hizo kama milioni kumi mi naenda kukopa wapi?
Akaniambia nilijua tu unataka kuharibu.
Hebu nipe hiyo bahasha.
Tujaingia ndani nilipigwa butwaa kwa kile alichokifanya jamaa.
Aliongea maneno machache sana akiutetea muda wetu kuwa tuko nje ya muda hata hivyo makazini tumejiiba kwa umuhimu na ulazima wa tukio hili akakabidhi bahasha kwa baba mkwe na kusema maandalizi yetu na dhamira vimefikia hapo huvyo ikiwapendeza kwa hekima na busara watukabidhi binti kwa gharama hizo.
Akafunga mjadala na kuwaachia jukumu la kukubali au kukataa na angalizo lilikuwa kwamba kama hawataafiki basi bahasha zote zilizokwisha kutangulia itabidi zirudi na hiyo ya mahari.
Wakawa wanahesabu na kupokezana mpaka mtu wa mwisho huku wakiongea kinyaturu sisi hatuelewi.
Yakatokea mazungumzo marefu sana baina yao lakini kwa kinyaturu tusielewe wanchojadili
Mwishoni ikawekwa tiki suala likaishia pale wakadai masuala ya koti la mzee bibi sijui kikoi mama na mjomba.
Jamaa akanitoa nje tena akaomba bahasha tano kulingana na idadi ya wahusika tukawekamo 40 kila bahasha tukarudi ndani wakakabidhiwa mchezo ukaisha ikabaki tafrija ndogo iliyokuwa ineandaliwa na wenyeji wetu kwa utaratibu.
Baadae tulipata muda wa kumtembelea bibi kwa upande wa baba mkwe.
Tuliongea nae vizuri na alikuwa mcheshi pia alitufahamisha kuwa ndie amemlea mke wangu
Jamaa akaniambia baadae kuwa macho sana japo hahisi uhatari huo kwenye familia hii lakini kwa machache tuliyoyasikia aliyatumia na kuniambia kuwa mji ule mama ana nguvu sana tofauti na vile tunavyomuona amekaa kimya.
Sikuelewa
Ila baadae nilikuja kuelewa kiufasaha zaidi kutokana na stori za binti mwenyewe.
Tulirudi Daslam kuendelea na maisha mengine.
Mchumba alipewa taarifa zote na yeye akaonyesha kufurahi.
Baada ya muda tulitia maguu kambi ya wazito.
Ninaposema kwa wazito namaanisha wazito haswa maana hata binti kwao ni kuzito lakini baada ya kuingia kambini kwetu alikiri wazi hakuficha alisema mbona kwenu ni kuzito sana?
Nikamzuga tu kuwa hata sijui wala hakuna uzito wowote maana wakati huo sikuwa najua chochote ukizingatia nimekulia mujini Daslam.
Sasa siku ya kwanza tunaingia tu picha niliyomuona nayo mama haikuakisi furaha hata kidogo kama walivyokuwa wanawasiliana kwenye simu.
Maza aliweka ile sura ya kiancient Vampire juu akaweka tabasamu lakini mimi ni damu yake niliuhisi ubaya moja kwa moja uliopo ndani ya mama.
Nikanyong'onyea maana nilijua kuna mziki mzito tena mno
Mwanamke nimempenda na meno yangu yote na kucha zangu zote lakini nishaihisi hatari kubwa kuninyemelea maana kutenganishwa nae sipo tayari lakini naliona likija kabisa ila sipo tayari linikute sijui kama mnanielewa?
Mama alipopata muda aliniambia mwanangu una uhakika umempenda huyu mwanamke?
Nikamuambia ndio nimempenda mama tena sana.
Mama akashika tumbo akaniambia basi ukaishi kwa utashi wako. Nakuamini hutaniangusha.
Akanisihi pia usije ukamtesa hata siku moja maana atakonda abaki kashingo tu hiyo itakuondolea uhakika wa kupata mwanamke mwingine hata ikitokea mmeachana.
Hili neno kuachana liliuchana moyo wangu ile vibaya mno. Sikuwa tayari kulisikia kabisa.
Tukakaa siku tatu
Mama akanifuata akaniambia mwanangu nikushauri tafuta mwanamke mwingine uoe.
Nikamuuliza kwanini? Akanijibu mimi ni mama yako na wewe ni mwanangu mimi tu ndie naweza kukushauri hilo hakuna mwingine.
Akaniambia nimeoa mwanamke mzuri mno tena mno yaani wa kila kitu hivyo nitafute mzuri mwingine pengine anaemzidi au kulingana na huyu nimuoe yaani wawe wawili sio kwamba nimuache huyu.
Kwakuwa nilishakuwa brainwashed na tantalila za watu kwa udhamini wa magharibi, tulibishana na mama mpaka tukatofautiana kabisa hata kipindi tulichopanga kukaa pale kijijini hakikutimia nikabeba vilivyo vyetu tukarudi jiji la wamba.
Maisha yakaanza mke wangu akamleta mtoto wake kutoka kwao lakini mikunjo na visa vya hapa na pale
Mwishowe akafanya maamuzi ya kuwa nimrudishe mtoto Singida
Mimi huyo hadi Ubungo nikampeleka mpaka Singida.
Nikarudi jijini kuendelea na maisha.
Pale nilipokuwa naishi mke wangu akaanza kusema sio watu wa pale hawaeleweki
Nikaona nihame
Nikaenda zangu bahari beach kuke mitaa fulan ya ubaridi.
Nikaanza life kule.
Sababu ya kutokwenda na wife kwao ilikuwa ni mimba
Mke alinasa mimba ndio maana ikabidi nikimbie mapema kwenda kwao.
So baada ya kuhamia bahari beach mimba ikazidi kuwa kubwa..
Lakini kuna dosari ilikuja mapema sana yaani siku ya tatu tangu tuhamie bahari beach nikakamata text kwenye simu ya wife namba ya jirani yangu wa huku huku tulikohamia anajaribu kuweka mazingira ili ajiweke nikamuuliza wife mwamba kapataje namba kiwepesi hivyo?
Akaniambia alimuomba tu wala yeye hakuwaza kama kuna nia mbaya yoyote ile.
Nikajiwazia tu so unahisi umepata bwege umpange eti
Twende tu maana najua kama ni kuliwa utaliwa tu sijakukuta bikra so sina haja ya kuacha majukumu ya taifa nije nikuchunge wewe.
Mitaa hii ni wanajeshi tupu raia wachache sana.
Sasa hawa wanajeshi wakawa wakinicheki wanamuambia wife kuwa kuna sehemu washaniona ila hawakumbuki infact ni wapi so nimewapotea.
Wakawa wanamuuliza wife mume wako anafanya kazi gani?
Wife anawaambia huyu anafanya biashara tu ndogo ndogo wale jamaa wanambishia..
Wakawa wana uhakika kabisa mimi nazijua kazi zao hadi vyeo lakini wao hawanijui ikawa ni tatizo.
Huyu jamaa aliyekuwa anamuwinda wife akajaribu kujenga ujaribu na mimi nikaishia kumuweka pending tu
Kisha siku moja naenda kupanda piki piki jamaa akaja nyuma nyuma ananiita swahiba swahiba. Nikasimama akanisalimia huku akiniuliza unakwenda kazini?
Nikamjibu hapana nasafiri naenda kwetu mara moja tu nitarudi siku sio nyingi.
Akasema sorry nilikuwa na maongezi na wewe vipi unarudi lini?
Nikamjibu nikirudi nikakukuta nitakutaarifu kuwa nimerudi.
Akauliza labda huwa unapiga tungi? Nikamjibu hapana
Vipi labda kumoka?
Nikamjibu hapana sivuti bangi.
Akasema sawa.
Nikasepa kazini.
Usiku nikarudi nikamkuta huyo jirani yangu kafungulia mziki mkubwa sana hadi kero sasa ile nataka kuingua ndani kwangu mara akaniita akanitambulisha manzi yake mmoja hivi sikujali nikamjibu short tu nikazama ndani
Akamtuma manzi kuja kunigongea
Nikatoka akanipa maelekezo kwamba jamaa yule kule anataka mkazungumze.
Kuicheki tembea ya demu nikajua nae ni mjeshi pia.
Nikamfata jamaa tukawa tunaongea japo jamaa alitaka anitoe mazingira ya pale home ila mi sikutaka kabisa
Basi akaishia kuongelea pale pale.
Aliongea vitu vingi ikiwemo kuulizia mishe zangu nikamjibu lakini alikuwa na mashaka kidogo.
Nikamwambia je anampenda sana wife kiasi isingetokea mimi kumuoa yeye angemuoa au anataka tu aonje ladha iliyomo ndani ya ule uzuri apite hivi?
Jamaa akabaki ameduwaa huku akisema aisee broo mbona umeenda mbali sana angalia tusijetukatoleana bastola kizembe.
Nikamuambia ningekuwa hivyo angekuwa futi sita chini tayari.
Jamaa akafurahi sana pia akanisifu kuwa sikai na kinyongo hivyo ni rafiki wa kweli akaniuliza kama natumia wine nikamuuliza anamaanisha nini
Akasema anataka twende tukanywe kidogo maana hajawahi kumpata mtu genuine kama mimi
NIkamjibu sihitaji wala.
Nikarudi zangu ndani.
Baadae nilimsafirusha mwanamke kwao baada ya siku za kujifungua kukaribia.
Mwamba sasa akaona ndio chance ya kujiweka karibu na mimi
Lakini kila alipojaribu nilimzuia maana kwa hilo nina mbinu zote wala sio shida.
Akaanza kufuatilia taarifa zangu popote alipohisi kuwa anaweza kuzipata hata kwa baadhi ya watu waliokuwa wananitembelea.
Lakini hakuna alichoambulia maana hata hao marafiki hawakuwa wakinijua kihivyo sembuse majukumu yangu?
Baadae nilihama pale nikiwa na taarifa zote juu ya watu wengi wa pale
Na wonderful ni kwamba huyu jamaa yeye alikuwa ni mwanajeshi wa nyota moja lakini jambazi la mbali sana ambapo matukio alikuwa anayapiga kwa raketi za simu then yeye ndiye mshika mtutu aliyeiva
Yalipita hayo na pale Nilihama wife akiwa bado hajarudi.
To cut the story..
Kule ukweni baba mmwe aliniulizaga swali hili lini utfunga ndoa na kufanya harusi?
Nikamjibu kuwa ngoja nifanye maandalizi nikikamilisha mipango yote nitaweka tarehe rasmi.
Lakini imepita miaka na binti yake tumepata mtoto wa pili tabia ikabadilika kabisa misuguano imeanza ndani nyumba
Maneno yamekuwa mengi kumekuwa na changamoto za hapa na pale maisha yakikaza pesa ikikosekana tu binti anakuwa mwiba mara anatoroka anakwende ambako anajua kuna ndugu zake hata kama wako Dodoma anaenda anakaa hata miezi sita nikikaa vizuri kiuchumi anarudi.
Nikaona huyu nikifunga nae ndoa halafu nikawa nimejenga vijumba kadhaa si atanivuruga huyu maana atataka aondoke mazima akijua mali tunagawana?
Lakini pia suala la unyumba lilifika baadhi ya miaka likawa linasua sua kabisa yaani mfano mimi hupenda nikikaa na mwanamke nimchezee maziwa na makalio yeye kwake ni noo.
Nikaona hapa nina picha tu ya kuku rosti huwezi kumla.
Nikaanza kumkumbuka mama kwa hili.
Kuna muda anakwambia hamu ya tendo la ndoa imekata kumbe alienda kwenye uzazi wa mpango akaweka vijiti.
Sasa huu mwaka mwanzoni ndio akasepa na kusema anarudi kwao nilikuta tu mtu keshasepakarudishia tu mlango kwakuwa nina madog nayafuga usalama ulikuwepo.
Sasa baadae ukweni wananiuliza kwanini nimeishi na binti yao kihuni sana kwa muda wote huo?
Mara kwanini sikumfungulia biashara binti yao muda wote huo hadi nimefulia?
Wakaenda mbali na kusema ni kweli ulilipa mahari lakini hukufunga nae ndoa hivyo ana haki ya kurudi pale nyumbani na akapata mwanaume mwingine akamuoa na hautakuwa na haki ya kudai chochote.
Nikakaa kimya hapo nikiwa naongea na kaka mtu akaenda mbali zaidi na kusema kuwa nimemnyanyasa mdogo wao.
Mambo mengi tu na biti juu.
Nikamjibu kuwa nimepiga simu nataka mke wangu arudì tuendelee na maisha maana mimi sijamuacha bali ameondoka mwenyewe.
Kaka mtu ananiambia kuwa ukipata pesa hunsikilizi mdogo wangu lakini ukifulia unaanza kumuona mtu wa maana.
Akanichimba biti kuwa aisee akirudi kwako tena ukapata pesa ukamnyanyasa labda niwe nimekufa
Nikamuuliza mnaposema alikuwa ananyanyaswa nilikuwa naishi na nyie wote?
Akawaka nikamuwashia moto maana anataka kutengeneza mazingira ya kunitawala mara oo umfundishe mkeo biashara unazofanya.
Nikamjibu tu kuwa wewe hujaoa,, Oa kwanza tuongee lugha moja. Akapanik akatema shiti nikazikusanya mara tano nikampa akakata simu.
Nikakaa kimya nikaazimia kumpelekea mwanamke watoto wake huko huko kwao.
Watu wakanitonya kuwa hakwenda kwao bali ndugu zake walimpa pesa akaenda kupanga mitaa fulani hapa hapa Mwanza.
Nikapeleleza hadi nikafika alipo kimya kimya baada ya kuhakikisha ni yeye nikachukua watoto nikampelekea akashangaa sana
Halafu mimi huyo.
Baadae ndugu zake wanasema nimeenda nimemtelekezea watoto mara ooh kama nataka yaishe mke wangu arudi home nikusanye wazee wangu twende pale Singida tukakae kikao nikawaambia hilo halipo kwenye bajeti yangu kama ingekuwa ni kurudi nilishamuomba na kuwaomba wamshauri binti arudi kwake lakini hola mwezi wa sita huu
Na mimi nimeamua kuhama mkoa kabisa yaani hata hivi vitu vilivyobaki nishamuambia nampelekea vyote tukakubaliana
So sasa huwa naenda tu pale alipopanga kuwaona madogo then nageuka
Maana yeye hajui kama nikiondoka mkoa huu ndio itakuwa mwisho wa mimi kuongea na yeye na hao watoto.
Anadhani nitaendelea kuhudumia kama vile yuko kwangu.
Wakuu ni jibu gan lilifaa kuwapa hawa wa ukweni ambalo litaacha mwanya baada ya miaka saba nikachukue watoto wangu
Maana najua atawapeleka tu kwao yeye arudi kudanga mujini.