Njaa inanukia, mvua zimegoma. Serikali zuieni kuuza chakula nje ya Nchi

Mbaya zaidi hii mbinu yao ya kiprimitive badala ya kuondoa tatizo la njaa inaleta njaa.
 
mwachieni mbowe mvua zitanyesha za kutosha au endeleeni kumshikilia mpate ukame
 
Vitoto vya mjini hivi, vikikosa maji ya kuoga siku 2 tu vinalia dunia nzima
 
Kwa sisi wakulima kwetu ni sherehe, mvua ivute vute ianze January.

Unadhani hizo bei za mbolea tutaziweza mazao yasipopanda bei? Tumeshapata hasara sana....Mvua ikaze hivyo hivyo.
Na sisi Serikalini hatutakubali gunia livuke 65,000 ..

Kwanza hakuna mkulima humu ndani ni wafanyabiashara wamejaza magunia kwenye store wanajifanya wakulima.
 
Hii nchi kila mtu anasubiria serikali, kweli kuongeza Tzn ni ngumu Sana
 
Jaribu kuingia kwenye kilimo japo kwa msimu mmoja tu afu utakuja ufute huu uhalo wako hujui ulisemalo kwani kuna mtu anapenda hasara?
 
Na sisi Serikalini hatutakubali gunia livuke 65,000 ..

Kwanza hakuna mkulima humu ndani ni wafanyabiashara wamejaza magunia kwenye store wanajifanya wakulima.
Mnaweza msikubali nyie na wanunuzi mitaani wakakubali.

Kwa hiyo wakulima hadhi yao ni ya chini kwamba hawawezi kumiliki smartphone au kwamba hawajui kama kuna kitu kinaitwa Jamii forum?

Mvua ikaze hivi hivi msiponunua serikali tutawauzia wafanyabiashara wa unga. Kwanza sisi hatutakagi kufanya biashara na serikali mahindi utoe leo pesa upewe mwaka umeisha.
 

Achana na hao wahuni mkuu. Huu uhuni ndio umechangia mimi kuweka signature ya hivi.
 
Reactions: Luv
Unataka wananchi mazao yao yawadodee si ndiyo.Wamelima kwa gharama kubwa nani atawarudishia gharama zao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…