Njaa mbaya sana; Ni jambo gani la hatari uliwahi fanya ulipokumbwa na njaa?

[emoji24][emoji24][emoji24] Nilipokuwa chuo UD, ilikuwa nikikosa hela, lazima nionekane tu, yaani nakuwa na mawazo, nakonda, nywele zinapauka, yaani hata uvaaji unabadilika

Nilivyokuwa first year sasa, mida ya saa tatu usiku nawasha miguu yangu, ni safari ya kutoka chuo kwenda Mabibo Hostel, muda huo utumbo unaruka ruka. Nilikuwa na sukari ya dharura, nikifika nachukua Limau ya unga naweka kwenye kichupa cha maji nakorogea na sukari, maisha yanakwenda[emoji24][emoji24]

Kwa hizi situations, sintomsahau binti Rose, aliniokoa na maisha haya kwa kiwango kikubwa hapo chuoni, sasa hivi ashaolewa maskini
 
Aisee. Mwamba alikuwa muungwana. Hakuwa na makasiriko. Usawa huu 280,000/= kwenda kwenye matumizi ambayo haujapanga sio kitu rahisi.
 
Sema mabinti wa chuo wanawasevu sana wanaume wakiwa hawana hela. Sasa hivi kuna binti pia kajitolea kumsave jamaa fulani ndio kwanza wapo first yia, anampikia, kumnunulia msosi hadi kumpa hela ya ziada ingawa jamaa sio kwamba hana hela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ex wako mtu sana. Inaonekana hamkuachana kwa kinyongo. Ninashawishika kukushauri umuweke kwenye mipango yako ya muda mrefu.
Tuna urafiki na suala la mapenzi halipo kabisa hakuna anayelifikiria. Kila mtu yuko busy na mambo yake ila tukipata muda tunaongea sana. Kuachana tulikubaliana, lifestyle yake na yangu tofauti hatungefika mbali
 
Njaa inaweza kumfanya mtu afanye jambo la ajabu sana!

Naomba tuelezane hapa, nikituko gani au jambo gani la hatari uliwahifanya ulipopatwa na njaa wakati huna kitu mfukoni?
Mie nilivyokuwa mdogo nilishikwa na njaa kali wakati sina kitu mfukoni mama akanisongea ugali na mboga ya mnafu. Nilipomwita kumuuliza nianze ugali au mboga ikawa hatari kweli, akanipiga na mwiko aliosongea ugali bila kosa lolote.
 
Njaa balaa lake halikuwahi la kitoto aisee.

Hadi unaanza kutamani kile chakula ulichokitupa enzi hizo kingekuwepo ukifakamie😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…