Njaa mbaya sana; Ni jambo gani la hatari uliwahi fanya ulipokumbwa na njaa?

Njaa mbaya sana; Ni jambo gani la hatari uliwahi fanya ulipokumbwa na njaa?

Kipindi nasoma chuo UDSM first year nakaa hostel lakini nilikuwa nimepanga Sinza Vatican huko naenda weekend tuu. Siku hiyo nimetoka chuo nikawaza hapa nitatoa hela ATM ya sinza kijiweni basi nimeshuka pale kufika ATM hakuna hela. Ikabidi nikanyage mpaka vatican sio mbali. Mfukoni mimebaki na 1000 tuu nikalala bila kula sikuwa na shida.

Kesho yake mchana nimeamka nikaprint tena hadi ATM Kijiweni kuangalia hela hakuna ikabidi nipande daladala 400 hadi Africasana kuna ATM pale nikawa nimebaki na 600 kufika pale pia hakuna hela pia. Nikarudi tena mpaka vatican kwa daladala mfukoni nimebaki na 200 tuu. Usiku njaa ilikamata ndani nina mchele tuu ikabidi niuloweke na maji nile mchele mbichi kupunguza njaa.

Kipindi hicho mawakala wa CRDB hawakuwepo wengi kama sasa hivi. Inshort niliomba nauli kwa huyo mama nilikutana nae ATM siku ya 3 yake naye alikuja kutoa hela akakosa akanipa 1000 iliyonifikisha chuo ndio nikaenda kutoa hela. Nikajifunza hata kama nyumbani naenda weekend tuu bora kuwa na kila kitu gas,mafuta etc.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji24][emoji24][emoji24] Nilipokuwa chuo UD, ilikuwa nikikosa hela, lazima nionekane tu, yaani nakuwa na mawazo, nakonda, nywele zinapauka, yaani hata uvaaji unabadilika

Nilivyokuwa first year sasa, mida ya saa tatu usiku nawasha miguu yangu, ni safari ya kutoka chuo kwenda Mabibo Hostel, muda huo utumbo unaruka ruka. Nilikuwa na sukari ya dharura, nikifika nachukua Limau ya unga naweka kwenye kichupa cha maji nakorogea na sukari, maisha yanakwenda[emoji24][emoji24]

Kwa hizi situations, sintomsahau binti Rose, aliniokoa na maisha haya kwa kiwango kikubwa hapo chuoni, sasa hivi ashaolewa maskini
 
Da kuna mapito nilipita mwaka 2018 sitasaha hapo ndio najua rafiki wa kweli mi yupi na mpenzi wa kweli nilipata kesi kazini nikatumia hela yot kusolve kimbembe sasa ni mama yangu mzazi ni mgonjwa kapooza nusu upande ...ili bidi nijifunze kupika maandazi tulawa tunashindia hayo hadi nilipopata muujiza kuna mtu alikosa kutuma hela akatuma kwenye mpesa yangu 280 k faster nikaitoa nikanunua mhitaji ...nikamuahidi kumlipa mwiaho wamwezi mshahara ulivyotoka nikamlipa nusu
Aisee. Mwamba alikuwa muungwana. Hakuwa na makasiriko. Usawa huu 280,000/= kwenda kwenye matumizi ambayo haujapanga sio kitu rahisi.
 
[emoji24][emoji24][emoji24] Nilipokuwa chuo UD, ilikuwa nikikosa hela, lazima nionekane tu, yaani nakuwa na mawazo, nakonda, nywele zinapauka, yaani hata uvaaji unabadilika

Nilivyokuwa first year sasa, mida ya saa tatu usiku nawasha miguu yangu, ni safari ya kutoka chuo kwenda Mabibo Hostel, muda huo utumbo unaruka ruka. Nilikuwa na sukari ya dharura, nikifika nachukua Limau ya unga naweka kwenye kichupa cha maji nakorogea na sukari, maisha yanakwenda[emoji24][emoji24]

Kwa hizi situations, sintomsahau binti Rose, aliniokoa na maisha haya kwa kiwango kikubwa hapo chuoni, sasa hivi ashaolewa maskini
Sema mabinti wa chuo wanawasevu sana wanaume wakiwa hawana hela. Sasa hivi kuna binti pia kajitolea kumsave jamaa fulani ndio kwanza wapo first yia, anampikia, kumnunulia msosi hadi kumpa hela ya ziada ingawa jamaa sio kwamba hana hela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ex wako mtu sana. Inaonekana hamkuachana kwa kinyongo. Ninashawishika kukushauri umuweke kwenye mipango yako ya muda mrefu.
Tuna urafiki na suala la mapenzi halipo kabisa hakuna anayelifikiria. Kila mtu yuko busy na mambo yake ila tukipata muda tunaongea sana. Kuachana tulikubaliana, lifestyle yake na yangu tofauti hatungefika mbali
 
Njaa inaweza kumfanya mtu afanye jambo la ajabu sana!

Naomba tuelezane hapa, nikituko gani au jambo gani la hatari uliwahifanya ulipopatwa na njaa wakati huna kitu mfukoni?
Mie nilivyokuwa mdogo nilishikwa na njaa kali wakati sina kitu mfukoni mama akanisongea ugali na mboga ya mnafu. Nilipomwita kumuuliza nianze ugali au mboga ikawa hatari kweli, akanipiga na mwiko aliosongea ugali bila kosa lolote.
 
Njaa balaa lake halikuwahi la kitoto aisee.

Hadi unaanza kutamani kile chakula ulichokitupa enzi hizo kingekuwepo ukifakamie😂
 
Back
Top Bottom