Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
[emoji24][emoji24][emoji24] Nilipokuwa chuo UD, ilikuwa nikikosa hela, lazima nionekane tu, yaani nakuwa na mawazo, nakonda, nywele zinapauka, yaani hata uvaaji unabadilikaKipindi nasoma chuo UDSM first year nakaa hostel lakini nilikuwa nimepanga Sinza Vatican huko naenda weekend tuu. Siku hiyo nimetoka chuo nikawaza hapa nitatoa hela ATM ya sinza kijiweni basi nimeshuka pale kufika ATM hakuna hela. Ikabidi nikanyage mpaka vatican sio mbali. Mfukoni mimebaki na 1000 tuu nikalala bila kula sikuwa na shida.
Kesho yake mchana nimeamka nikaprint tena hadi ATM Kijiweni kuangalia hela hakuna ikabidi nipande daladala 400 hadi Africasana kuna ATM pale nikawa nimebaki na 600 kufika pale pia hakuna hela pia. Nikarudi tena mpaka vatican kwa daladala mfukoni nimebaki na 200 tuu. Usiku njaa ilikamata ndani nina mchele tuu ikabidi niuloweke na maji nile mchele mbichi kupunguza njaa.
Kipindi hicho mawakala wa CRDB hawakuwepo wengi kama sasa hivi. Inshort niliomba nauli kwa huyo mama nilikutana nae ATM siku ya 3 yake naye alikuja kutoa hela akakosa akanipa 1000 iliyonifikisha chuo ndio nikaenda kutoa hela. Nikajifunza hata kama nyumbani naenda weekend tuu bora kuwa na kila kitu gas,mafuta etc.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nilivyokuwa first year sasa, mida ya saa tatu usiku nawasha miguu yangu, ni safari ya kutoka chuo kwenda Mabibo Hostel, muda huo utumbo unaruka ruka. Nilikuwa na sukari ya dharura, nikifika nachukua Limau ya unga naweka kwenye kichupa cha maji nakorogea na sukari, maisha yanakwenda[emoji24][emoji24]
Kwa hizi situations, sintomsahau binti Rose, aliniokoa na maisha haya kwa kiwango kikubwa hapo chuoni, sasa hivi ashaolewa maskini