Pole sana brother. Allah akufanyie wepesi utatoka kwenye tabu unazopitiaMimi mpka sasahivi ndo hali napitia unapigwa na njaa halafu huku mwenye nyumba anataka kodi.Wiki iliyoisha nilikaa kama siku nne hivi sijala kitu bhana halafu nikiangaza kitu cha thamani nilicho nacho gheto ni jiko na masufuria nkaona hivi havina msaada kama hata msosi kupata ni shida ilikuwa mida ya saa tatu nikachukua kajiko kadogo ka mkaa nikamwaga majivu nikalitia kwenye begi nkaweka kisu masufuria nikayaweka kwenye mfuko nikashuka zangu kwa mam ntilie yule bi mkubwa aliona na shida akaamua kunilalia kabisa nikauza vitu vyangu kwa elfu 10 akanipa na sahani ya wali nkalala nkarudi kulala shida haziishi wazee hapa nawaza nauza nini nilipe kodi kitu cha thamani nilicho nacho ni pc kama ingekuwa yangu ningekuwa nishapiga bei sema nathamini vitu vya kupewa.
Sent from my SM-M515F using JamiiForums mobile app