Zanzibar 2020 Njama? Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Maalim Seif awekewa Pingamizi

Mkuu hapo kwenye tarehe siyo kuwa amesahau hapo ndiyo alipotengenezea kosa ili Maalim aenguliwe.
 
Kuna mambo mengine ni ya ajabu sana.. hizo sababu zinazofanya wagombea wakose sifa ni za ajabu sana.. na haziingii akilini.. na ni kwanini wanakosea wapinzani pekee? Kama tumeamua kufanya uchaguzi, yafaa tuache wananchi waamue juu ya viongozi wawatakao.. ni jambo baya sana kuwateulia wananchi kiongozi ambaye hawakumtaka..
 
Yote haya yanadhihirisha jinsi ccm ilivyoasiwa na wananchi na wao sasa wanachofanya ni kufa maji tu.
 
Haiwezakani ikawa hiyo ndio hoja toeni hiyo nakala ya pingamizi kutakuwa kuna pingamizi halisi
Kama ulisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa uchaguzi Zanzibar huwezi kumpinga mleta mada. Alisema vyama vilivyompinga ambavyo ni ADC na NLD vimehoji tofauti ya tarehe kwenye fomu ya kiapo, tarehe 7-7-2020 na 7-9-2020.
 
Wameghushi
 
Tarehe iliyokosewa iliandikwa na jaji au Hamad?
 
Ukiangalia fomu ipo sawa haijakosewa. Mkurugenzi wa tume alisema alijaza Tarehe 7/7 2020, hapa kwenye fomu inaonyesha wazi amejaza tarehe 7/09.

Tusubiri jibu la tume kuhusu hilo pingamizi. Natumaini haki itatendeka.

View attachment 1565612
Waache ujinga, wataiingiza hii nchi kwenye machafuko. Tume wanataka kutumia fomu iliyohaririwa Lumumba badala ya ile aliyowasilisha Maalim Seif Hamad. Wazanzibar usikubali ujinga huu! Polepole hii nchi utaiingiza kwenye vurugu! Mwaka huu mmekamatika hampumui!
 
Documents muhimu kama hizi hazina serial numbers (pre-numbered)!!!!! Ina maana mtu yeyote anaweza kutengeneza ya kwake akaigiza mwandiko. Serial numbers zingesaidia kuonyesha kuwa fomu aliyopewa ndiyo hiyo amerudisha; kama zingetokea fomu mbili tofauti zenye serial number moja, tunaweza kufuatilia kujua forgery imefanywa na nani
 
Rais anatakiwa kuwa makini.
 
Ukiangalia fomu ipo sawa haijakosewa. Mkurugenzi wa tume alisema alijaza Tarehe 7/7 2020, hapa kwenye fomu inaonyesha wazi amejaza tarehe 7/09.

Tusubiri jibu la tume kuhusu hilo pingamizi. Natumaini haki itatendeka.

CCM waache mambo ya Kitoto, kizazi cha leo kina kumbukumbu zote hakidanganyiki tunajua kua fomu wamefoji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…