Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,888
Kuna mkakati wa kuifukuza POLISARIO nchini.
Serikali ya Tanzania: POLISARIO ni Chama cha Ukombozi ambacho kilipewa hadhi ya Serikali na uanachama wa Umoja wa Afrika tangu 1982. Suala hili limeanza kuleta utata wa kisheria Katika Umoja wa Afrika na Katika duru za Kimataifa.
ACT Wazalendo: Huu ni Mkakati unaosukwa kuifukuza POLISARIO kwenye Umoja wa Afrika na tulionya hili mapema sana wa kampeni za kuirudisha Morocco AU. Serikali ya Tanzania kuweka sentensi hii kwenye Hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje Mwaka 2018 ni mkakati wa kutuandaa kisaikolojia kuifukuza POLISARIO.
Msimamo wetu ni kuwa Jamhuri ya SAHRAWI (Sahara Magharibi) ni Taifa huru lililovamiwa na Morocco. Ubalozi uliopo nchini ni ubalozi wa SAHRAWI na sio wa POLISARIO na kiti cha AU ni kiti cha Jamhuri ya SAHRAWI.
Tunaitaka Serikali ya Tanzania iache ujanja ujanja kwenye suala hili na itumie nafasi yake ya urafiki na Morocco kuhakikisha Maazimio ya UN yanatekelezwa ili watu wa Sahara wawe Huru wajenge nchi yao.
Zitto Kabwe
24/5/2018