Njama za kuifukuza Sahara Magharibi zinasukwa. Tanzania inahusika?

Njama za kuifukuza Sahara Magharibi zinasukwa. Tanzania inahusika?

Hao Sahrawi wanaisadia nini Tanzania?
Tabia na kauli ya kikahaba kabisa hii. Mahusiano ya kimataifa na urafiki ni vitu viwili tofauti. Ikiwa fulani hana masilahi basi tuachane na mambo yake saa hizi tungekuwa na hali mbaya kama Taifa, maana wanaotusaidia yetu si wote maslahi na sisi.
 
J
Wa Sauzi tuliwapigania,tuliwapa base na kuwapa makazi miaka mingi baadae mzulu anamuona kaburu ni bora kuliko mbongo ,hataki hata kijana wa kitanzania ajitafutie riziki Jo'burg .sasa hivi Tanzania kwanza vingine baadae
Juzi juzi walimuua lecturer moja wa kitanzania aliyekuwa akifundisha in one of the Universities Joburg! Washenzi sana wale.
 
Zitto Sahara Magharibi imetambulika de jure kuwa huru tangu mwaka 1976 but in reality haijawahi kuwa huru kwani ilichukuliwa na Morocco na licha ya Morocco kujiondoa AU (OAU), imepita miaka zaidi ya 40 hakuna tangible kilichofanyika.

It's a fact of life kuwa, Sahrawi ni mali ya Morocco, nani ataenda kuikomboa tena baada ya muda wote huo.

Sera yetu ya Mambo ya Nje imeshabadilika na sasa focus yetu ni Economic Diplomacy." Tulisaidia nchi ngapi kwa miaka 35 (1961-1994) ya mapambano yetu ya uhuru Kusini mwa Afrika? Leo hii ukiacha Msumbiji nani unayemzidi kimaendeleo? Tusijidanganye, kila kitu mwenye nguvu ndiye huwa (na ndiye anayepaswa) kushinda. Na hapa Morocco ameshinda.

Tuambie msimamo wako kwenye uhuru wa Sudan-Sudan Kusini, Ethiopia-Eritrea na Somalia-Somaliland.
 
Kuna mkakati wa kuifukuza POLISARIO nchini

Serikali ya Tanzania: POLISARIO ni Chama cha Ukombozi ambacho kilipewa hadhi ya Serikali na uanachama wa Umoja wa Afrika tangu 1982. Suala hili limeanza kuleta utata wa kisheria Katika Umoja wa Afrika na Katika duru za Kimataifa.

ACT Wazalendo: Huu ni Mkakati unaosukwa kuifukuza POLISARIO kwenye Umoja wa Afrika na tulionya hili mapema sana wa kampeni za kuirudisha Morocco AU. Serikali ya Tanzania kuweka sentensi hii kwenye Hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje Mwaka 2018 ni mkakati wa kutuandaa kisaikolojia kuifukuza POLISARIO. Msimamo wetu ni kuwa Jamhuri ya SAHRAWI ( Sahara Magharibi) ni Taifa huru lililovamiwa na Morocco. Ubalozi uliopo nchini ni ubalozi wa SAHRAWI na sio wa POLISARIO na kiti cha AU ni kiti cha Jamhuri ya SAHRAWI. Tunaitaka Serikali ya Tanzania iache ujanja ujanja kwenye suala hili na itumie nafasi yake ya urafiki na Morocco kuhakikisha Maazimio ya UN yanatekelezwa ili watu wa Sahara wawe Huru wajenge nchi yao.

Zitto Kabwe

24/5/2018

Zitto bhana, Swala la Sahara ya Magharibi limekuwepo miaka na miaka, Umoja wa Mataifa ulijaribu kuingilia kuweka makubariano baina ya Polisario Front/SADR na Morocco lakini imeshindikana, bado Russia nao wakajaribu. Mwaka 2000 Morocco waliamua kuwa hawatoendelea na maongezi au usuluhishi wanacho tambua wao kuwa Sahrawi ni sehemu ya Morocco. Lakini inasemekana kuwa waanzilishi wengi wa Polisario ni maveterani waamihaji toka Morocco. Nakuwa waliunda umoja huo ambao unawajumuisha makabila asili ya waamiaji katika Sahrawi. Maongezi yaliyokuwa yanafanyika ni kwa wananchi wa Sahrawi wao wenyewe kupiga kura waweze kukubali au kukataa kama wanataka waendelee kuwa chini ya Morocco au lah haya makubaliano ndo yalikuwa yana ungwa mkono na UN. Na hakuna muafaka uliofikiwa. Umoja wa Mataifa unaitambua Sahara ya magharibi kama taifa lisilojiongoza, na ambalo si koloni. Sasa ndugu yangu zito lawama zako kwa Tanzania, sioni mantiki yake kwani wenye nguvu kama UN, AU, USA, RUSSIA na baadhi ya nchi wameshindwa kuleta usuluhishi, wewe kazi yako kuilaumu nchi yako siko zote. Ukilala ukiamka wewe na Tanzania. Je miaka yote ulikuwa wapi kwani haijawai tokea suluhishi la mgogoro huu kufikia hitimisho. Kilichotambulika na Umoja wa Mataifa nikuwa Polisario Front/SADR ndiye mwakilishi wa SAHRAWI. Na UN inaitambua Sahara ya Magharibi kama nchi isiyojitawala bali inawaakilishi, ndo maana wakaweka mikakati ya masuluhisho. Wewe unachokisema hapa ni kana kwamba Sahara ya Magharibi nchi iliyojitawala sasa inataka kuondolewa utawala wake binafsi. Kwanini ulione leo siku zote umekuwa wapi kutetea maslahi ya SAHRAWI ambayo haijawahi kuwa na Uhuru wa kujitawala yenyewe. Nchi mbalimbali duniani zimekuwa zinabadilika kulingana na maslahi yao, mara wawe upande wa Morocco mara upande wa Sahara Magharibi.
Tanzania tulitumia nguvu zetu nyingi kupigania Mataifa mengine hasa kusini mwa jangwa la Sahara kupata Uhuru. Tulitumia raslimali zetu. Nakumbuka wakati huo mashuleni watu tuliimba nyimbo za ukombozi. "Nataka kwenda Zimbabwe" hata Roma kaimba naenda Zimbabwe huo wimbo Neno hilo lilitumika kuhamasisha watu, ndipo tukaimba nataka kwenda zimbabwe nikaokoe ndugu zangu wanakufa: Sasa ni muda wa kuangalia maslahi yetu. Nchi nyingi zilizoendelea siasa zao ni za maslahi. hawana adui wa kudumu au rafiki wa kudumu. Tanzama Marekani, Uingereza, France, Ujerumani na nyinginezo. Wao wanaangalia Maslahi kwa Taifa. Pia Mataifa yaloendelea hukuti mtu analaumu laumu nchi yake. Ni wazalendo na kamwe hawaisemi nchi yao vibaya. Zito hizo siasa zimepitwa na wakati. Kikubwa angali mtanzania anafaidika nini, Mtanzania uchumi wake unakua, Mtanzania tunakuza kipato cha raia masikini, haya ndo yakupigania, na si kulaumu bali kushauri na kutafuta mwafaka.
 
Wengi hawataelewa kabisa ila watachangia tu
Tanzania ya viwanda na Saharawi inaingilianaje
 
Sikumbuki hata ni sehemu gani.....Ngoja niutafute.
Nakumbuka niliwahi kukwambia kwamba haya yatatokea kwenye uzi fulani hivi,
Ilikuwa ndiyo siku ya kwanza mimi na wewe kuonana na tukabishana sanaa sanaaa.
Oooooh nmekumbuka huo uzi mkuu.... Dah tulibishana sana kuhusu POLISARIO, PLO na Biafra ila kwa zile nondo zako nilisalimu amri 😀😀😀 na toka hapo sikuwa na guts za kudebate lolote na wewe 😉
 
Inapaswa pia tujiulize kuwa ANC, SWAPO, na wengine kama hao wameisaidia nini Tanzania. Tulitumia miaka mingi kujitia umasikini ili kuwakomboa wengine, sasa hivi wao wanapeta kiuchumi sisi tumebaki tunashangaa.
Ndio maana Zito anataka tuwaache wapambane kivyao sio serikali yetu kutoa matamko haituhusu
 
Tabia na kauli ya kikahaba kabisa hii. Mahusiano ya kimataifa na urafiki ni vitu viwili tofauti. Ikiwa fulani hana masilahi basi tuachane na mambo yake saa hizi tungekuwa na hali mbaya kama Taifa, maana wanaotusaidia yetu si wote maslahi na sisi.
Ni kweli umetokea kwenye TUNDU baya!
 
Oooooh nmekumbuka huo uzi mkuu.... Dah tulibishana sana kuhusu POLISARIO, PLO na Biafra ila kwa zile nondo zako nilisalimu amri 😀😀😀 na toka hapo sikuwa na guts za kudebate lolote na wewe 😉
Mambo yako wazi mkuu, yaani nilishajua kabisaa ndiko tunakoenda huku kwa tabia za mtu kama Raisi Magufuli.
 
Kweli kabisa mkuu, hao wa Sahrawi na wapalestina wacha wajipiganie wenyewe, Sisi sasa hivi interest yetu ni kuboresha uchumi na maisha ya watu. Tunabadili mfumo wa mahesabu yetu sasa, Sasa hivi ni kutengeneza urafiki wenye tija tu, urafiki usio na tija kama ule tuliokuwa nao na vyama vya ukombozi kusini mwa Afrika tupa kule. Kilichobaki sasa ni siku ya kuhamishia ubalozi wetu Yerusalem.
Hapa umeongea fact ingewezekana hata Leo tuhamishie ubalozi Jerusalem tuangalie faida kama wachina migogoro tuwaachie wao
Huyo wazir aachane na mambo ya wengine ya kwake yanamshinda
 
Nilidhania Mahiga angeleta usimamizi imara wa mambo ya diplomasia ila ndo kaharibu kabisa..Kujipendekeza kwa mkoloni Morocco ni zaidi ya uzwazwa..nchi za africa ni nchi zinazoongozwa kiboya sana with no focus..
 
Aliyekwambia ACT ina exist ni nani? Usijifanye hujui km kauli ya zzk ndio kauli ya unachokiita ACT. By the way sijafanya personal attack km unavodai. Nimekuwa nikimfatilia huyu mzalendo ana hoja nzuri chokozi lkn sio msimamizi na muumini wa anachokisema. Amekuwa MTU wa kulalamika tuu na ndio mana watu wameanza kumchukulia kawaida sana.

Ulitaka akishasema achukue hatua gani?
 
Aliyekwambia ACT ina exist ni nani? Usijifanye hujui km kauli ya zzk ndio kauli ya unachokiita ACT. By the way sijafanya personal attack km unavodai. Nimekuwa nikimfatilia huyu mzalendo ana hoja nzuri chokozi lkn sio msimamizi na muumini wa anachokisema. Amekuwa MTU wa kulalamika tuu na ndio mana watu wameanza kumchukulia kawaida sana.

Unataka asimamieje? Yeye ameshatoa hoja zake na kuwafungua macho/ kuwatoa tongo tongo, kinachofuata ni nyie wengine kuendeleza.

Hapo zaidi ya andiko hili unataka afanyeje??
Kama ni kweli na government ni sensitive itachukua hatua au kutoa maelezo.

Kikubwa chama chake kimejionyesha dhahiri kuupinga huu udhalimu.
 
Wa Sauzi tuliwapigania,tuliwapa base na kuwapa makazi miaka mingi baadae mzulu anamuona kaburu ni bora kuliko mbongo ,hataki hata kijana wa kitanzania ajitafutie riziki Jo'burg .sasa hivi Tanzania kwanza vingine baadae
pic+mwanafunzi souh africa.jpg

Kama walivyomuua MWANAFUNZI wa shahada ya uzamivu (PhD), Baraka Nafari
 
Kuna mkakati wa kuifukuza POLISARIO nchini

Serikali ya Tanzania: POLISARIO ni Chama cha Ukombozi ambacho kilipewa hadhi ya Serikali na uanachama wa Umoja wa Afrika tangu 1982. Suala hili limeanza kuleta utata wa kisheria Katika Umoja wa Afrika na Katika duru za Kimataifa.

ACT Wazalendo: Huu ni Mkakati unaosukwa kuifukuza POLISARIO kwenye Umoja wa Afrika na tulionya hili mapema sana wa kampeni za kuirudisha Morocco AU. Serikali ya Tanzania kuweka sentensi hii kwenye Hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje Mwaka 2018 ni mkakati wa kutuandaa kisaikolojia kuifukuza POLISARIO. Msimamo wetu ni kuwa Jamhuri ya SAHRAWI ( Sahara Magharibi) ni Taifa huru lililovamiwa na Morocco. Ubalozi uliopo nchini ni ubalozi wa SAHRAWI na sio wa POLISARIO na kiti cha AU ni kiti cha Jamhuri ya SAHRAWI. Tunaitaka Serikali ya Tanzania iache ujanja ujanja kwenye suala hili na itumie nafasi yake ya urafiki na Morocco kuhakikisha Maazimio ya UN yanatekelezwa ili watu wa Sahara wawe Huru wajenge nchi yao.

Zitto Kabwe

24/5/2018
Mbona tulivua nguo kitambo?
 
Duh Kwahiyo ukoloni wa mwenzako ni sawa tu kisa haupati faida??? Ngoja siku mvamiwe na Idd amin mwingine alafu tusikie mnalialia AU kama wakati ule wa Nyerere ndio mtaelewa uchungu wanaoupata watu wa SAHRAWI kuona mnawakumbatia watesi wao
Tanzania tumewapigania kupata uhuru S.Africa lakini mkaburu anadhaminiwa zaidi ya Mtanzania

Sasa hivi tunatengeneza uchumia, mambo ya kusaidia kupigania ukombozi ya watu wengine umepitwa na wakati..

Hapo congo kuna wanajeshi wetu walikufa kibao hao hao wapuuzi walitoa hata salamu za pole?

TANZANIA FIRST,
 
Back
Top Bottom