Soma swali vizuri, hilo swali ulilosema la kitoto ni swali gumu sana
Kimsingi ni hoja nzima, argument from locality
Usijibu tu ilimradi ujibu
Hili ni tatizo la kutokuwa makini na kile ulicho kiukiza. Swali lako nimejibu tena kwa kutoa mfano nabii Isa,swali lako la kitoto na lina baki kuwa la kitoto kwa maana uliegemea kwa mtume Muhammad ukasahau kwamba njia hii imetumika kwa mitume wengine.
Kuna options mbili ambazo Mungu angetumia kuleta uislamu duniani (au dini yoyote ile)
Mola hapangiwi jambo bali anafanya kile ambacho ni bora.
Nilikwambia huko awali ya kuwa si kweli Uislamu umetangaa kwa jihadi pekee,jihadi ni ibada kama ibada nyingine,jihadi ni ibada ambayo imekuja baadae.
1.Atoe manabii kwenye kila jamii ya watu (Asia, Ulaya, Afrika etc), wote wakihubiri ujumbe usio pingana kuhusu uislamu kwa wakati mmoja
Allah anasema katika Qur'aan ya kuwa.
36. Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha. (an-Nahl :36)
Katika kila umma aliwatuma manabii maana yake hata huku kwetu walitumwa manabii japokuwa hawajatajwa kwa majina. Lakini manabii na mitume wote walikuwa dini moja.
2.Aanzishe eneo moja na kwa jamii moja, kisha isambae kadri miaka inavyozidi kwenda
Mola hapangiwi ndiyo maana kila kitu kimewekwa wazi,leo katika dini yetu kuna hukumu ya mtu ambaye aliishi hapa duniani lakini hakufikiwa na ujumbe,ili ujue ya kuwa hakuna mwanya wa kutokea katika ujumbe na Mola wetu anafanya kilicho kuwa bora.
Kwa mtu mwenye busara ni rahisi kuona njia ya kwanza ndiyo option sahihi
Hapa tunaangalia elimu na uhalisia,hizo busara nafasi sababu njia zote zimefanyiwa kazi.
Kwa Mungu mwenye ujuzi wote ange prefer zaidi option ya kwanza kuliko ya pili
Sababu, kwa option ya kwanza kungekua na dini moja tu kuu
Naoma unarudia kitu ambacho kilishafanyiwa kazi na kipo.
Kusingekua na confusion kuwa kati ya mshia au msuni yupi sahihi
Mjinga asiye soma ndiyo ataona kuna "comfusion" kati ya shia na suni,mashia wako mbali ma uislamu kwa sababu hawaufati.
Kila kitu kipo wazi,mtume wetu anasema ametuacha katika hali ambayo mchana wake ni sawa na usiku wake,hatopotea humo ila mwenye kutaka apotee. Kwahiyo hizi zako zinabaki kuwa stori tu.
Na ingewafikia watu kwa wakati. Mmoja
Hii si hoja,ndiyo maana hata wale ambao hawakufikiwa na ujumbe wana hukumu yao,bali mpaka watoto walio kufa kabla ya kunalehe wana hukumu yao. Ili ujue ya kuwa akili yako ni ndogo sana kufikiria mambo haya kwa kudhani tu walio angaliwa hapa ni watu fulani tu.
Njia ya pili ina disadvantages nyingi
Mfano watu walio zaliwa kabla ya uislamu, bila hata kuusikia watahukumiwa kwa vifungu vipi?
Kwanza kabisa Uislamu haujawahi kutokuwepo katika uso wa ardhi hii. Nakupa mfano watazame Wanafalsafa wa kale wa magharibi,hawa waliishi kipindi ambacho hapakuwa na mtume lakini mafundisho ya mitume walio pita yalikuwepo na kuna watu walikuwa wanayatumia mafundisho hayo.
Tukirudi kwa watu ambao wameishi mpaka wanakufa hawakufikiwa na ujumbe watu ambao mpaka leo hii wapo,hawa hukumu yao ipo,watapewq mtihani siku ya malipo watakao faulu watalipwa pepo na watakao feli watalipwa moto.