uchawi unausema hauna ukweli wowote?
Hapo ndio ulipo anzia kupotea, elimu ya uchawi ipo nje na sayansi na hivyo ni ngumu kuitambua na wala haihusishi sayansi kabisa katika kuitambua, sasa nitakushangaa kutumia sayansi kupima mambo mengine yasiyo hitaji sayansi. Sayansi sio kila kitu kwenye maisha .kila jambo na sehemu yake.
Mambo haya ni magumu sana ,mtaparuana bure tu pasipo kupata muafaka. Mnazungumzia elimu mbili tofauti kabisa na hivyo kuelewana ni vigumu mno. Mambo ya kiimani ni magumu na nitofauti na elimu ya kisayansi ilivyo,na hayahitaji elimu kubwa kuyaelewa.Yanahitaji imani tu, yaani kuamini kwanza ndo yanajizihirisha uwepo wake.
Scars hauamini na hata haujui uchawi utaaminije vitu vingine ambavyo huwezi hata kuvihisi kwa kutumia hiyo sayansi uliyonayo? Amin katika hicho unachoamin ia pia tambua kuna mengi yanayoendelea nje ya kile unachokiamini ww, ndio dunia inavyoenda, sio kila jambo utalifahamu, ukibahatika kujua jamabo moja tambua kuna moja lipo ambalo bado hujalijua.