Mkuu natamani kujua hao wanaopinga uwepo wa Mungu wanapata maslahi gani lengo lao kuu nini?
Hivi hawajajificha kwa ibilisi kweli?
Mungu ni nini?
Toa tafsiri yako ya neno Mungu?
Mbona concept ni simple tu
Define Mungu ni nini?
Lete hoja inayolenga kuthibitisha Mungu yupo
Then sisi pia tutatoa hoja za kuipinga (counter arguments)
Na wewe utatoa hoja za kupinga counter arguments zetu au uka modify hoja zako
Hivi ndivyo watu wenye busara hukosoana na kujengana kifikra
Sio comment za mtoto wa chekechea kama yako
Hivi unashindwa kujenga hoja ya namna hii
(Assume ningekua naamini Mungu)
1.Natoa tafsiri ya kipi ninaenda kuthibitisha
Mungu ni mmoja, yule mwenye nguvu kuliko chochote tunachoweza fikiria
Mwenye upendo kuliko chochote tunachoweza fikiria
Na mwenye maarifa yasio na mipaka kuliko chochote tunachoweza fikiria
Kisha, Naamini Mungu yupo (rejea tafsiri yake hapo juu)
Kwa hoja ifatayo
1.Ndege ya abiria ina mbawa zilizo chongoka kwa ustadi mkubwa ili kuruhusu hewa ipite kwa kasi zaidi juu ya mbawa kuliko chini ya mbawa
Tofauti hii ya speed ya hewa, inatengeneza mgandamizo (pressure) unao sukuma ndege kwenda juu
Mbawa za ndege ni dhahiri zilitengenezwa kwa lengo hili, na wahandisi
Kwa sababu kama zisingekua katika umbo hilo, ndege isinge paa
Na ni ajabu, tukisema upepo ulivuma na kukusanya vipande vya aluminum na steel na kwa bahati mbaya tu bila utashi wowote ukaunda mbawa za ndege na kuziweka panapo stahili
2.Kunguru,ana mbawa zinazofanya kazi namna hio hio
Kwa kua tumeona kwenye premise ya kwanza kuwa haiwezekani kwa mbawa za namna hii kutokea tu kwa bahati mbaya basi mbawa za kunguru kama tulivyoona kwa mbawa za ndege ya abiria
Ziliundwa kwa kusudi hilo,
3.Kwa kuwa hakuna muhandisi wa kibinadamu aliyeunda mbawa za kunguru (kunguru tumemkuta akiwa hivyo)
Basi yupo aliye nyuma ya huu ubunifu, huyo ni Mungu
4.Hivyo Mungu yupo
Huu ni mfano wa hoja iliyotolewa na mtu mwenye busara anayejua anachokiamini
Sio nyie, hamjui hata kujenga hoja
Mna hoja za kitoto mno
Ukijenga hoja ya mfano huo hapo juu ambayo ni logically sound
Utatupa sisi mtihani wa kuonyesha madhaifu katika premise moja wapo
Otherwise hatuna budi kukubali hitimisho lako kuwa Mungu yupo
Kwa sababu tumeshindwa kataa hata premise moja, so logically lazima tukubali conclusion
Ume WIN argument
Badala yake mna kuja na hoja za kitoto
Hiyo hoja niliyotumia kama mfano, ni variation yangu ya Teleological Arguments
Moja kati ya hoja dhaifu zaidi kwenye Philosiphy of religion
Nawashauri someni Philosophy of religion
Jifunzeni kutetea mnachokiamini kwa hoja