David Harvey
JF-Expert Member
- Jul 17, 2014
- 2,894
- 6,020
Umeamua kayakana maneno yako sio? Wewe na wanazi wenzako humu jf kila siku mlikuwa mnaongelea ilo jambo, baada ya kupigwa 5 mnaanza kukana.Unamjaza mwenzio upepo. Amefungua link kwenye post ya kwanza akaangalia niliileta lini mada ya kuhoji hadi aseme "Baada ya kufungwa tano ndio unataka kufahamu ubora wa NBC imeingia vipi"?
Baada ya kutamka how much yalifuatiwa na maneno gani?Nawe jibu swali kwa nini Infantino aulize "how much" tena baada ya kutoka kuuliza "how many" akabadili swali? Msomali wenu alishindwa kujiongeza.
Mwambieni Rais wenu aache kuzunguka kusambaza umbea kama Mwajuma Ndala Ndefu
Hajui kiingereza vzr yule kama Robertinho baada ya kusema how mucha baadaye alijirekebisha akasema How many ?Wote tumejionea kwenye mitandao hii hii ya kijamii kuwa Motsepe na Infantino walikuwa hawajui matokeo. Uzuri video mmesambaza uto wenyewe. Ila video inaonyesha waliuliza "how much?" Kwa hiyo inawezekana walimuuliza ametoa mlungula kiasi gani kupata ushindi ule.
Huyo mbwiga hana ajualoHajui kiingereza vzr yule kama Robertinho baada ya kusema how mucha baadaye alijirekebisha akasema How many ?
Niliwahi kuhoji taarifa za mchongo kuwa eti ligi ya NBC ni ya 5 kwa ubora na wengine wamekuwa wanajitangazia tu eti derby ya Kariakoo ni moja ya derby 3 kwa ubora na ukubwa Africa, watu wakanibishia.
Kuna kaclip kanasambaa kakionyesha Rais wa Yanga akiwa South Africa akisambaza umbea kwa Rais wa CAF Patrice Motsepe na Rais wa FIFA Gianni Infantino kuwa Yanga imemtandika mtu goli 5. Infantino ambaye ni mwanachama na shabiki kindakindaki wa Simba mwenye kadi namba 45263 alionekana kupuuzia taarifa hizo, akikodolea kamera kama haamini amini hivi huo umbea huku Rais wa CAF akihoji labda inawezekana kuna wachezaji wamerubuniwa au ni fluku tu ya kimpira, Hersi alipoanza kujitetea video ikakata hapo hapo.
Tuyaache hayo, swali langu inakuwaje ligi inayosemekana ni ya tano kwa ubora Africa, ligi inayosemekana kuzizidi kwa ubora ligi za Saudi Arabia, USA na Sweden, na wakati huo huo derby ya Kariakoo inayosemekana ni top 3 Africa, lakini Rais wa CAF na FIFA hawajui hata matokeo ya hiyo derby wiki moja baada ya mechi yenyewe?
Niliwahi kuhoji taarifa za ligi ya NBC kuwa ligi ya 5 kwa ubora hapa sikupewa majibu ya kuridhisha.