Njia 10 za Uchumba Salama

Namba 10 ni UTATA kwa dunia ya leo. ME na KE wanataka kujua compatibility kwenye idara hiyo kwa sababu mbali mbali. Hivyo inaweza kuwa sababu ya “uchumba” kuvunjika.

 
Hamna bro
Dhambi zote Ni sawa na zote zinasameheka.
Wote Wana Haki ya kujitunza iwe usichana upo au haupo.
Kutokuwa na usichana haimpi mtu guarantee ya kuendelea kufanya dhambi.
Mungu anasamehe na anamfanya mtu kuwa mpya..

Kovu la kuungua kwa moto na kovu la kukatwa na chupa hayawezi kuwa sawa. Ila yote ni makovu. Kusamehewa kupo na maisha kuanza upya.. ila zile roho za kukosea sio kwamba zinakufa au zinapotea, bado zinakuwa zinazunguka na wewe sema ni ile sala na imani zinazifukuzia mbali. Unapolega ile roho ya kukosea inakuvaa upya tena kwa nguvu zaidi ya mwanzo. Hivyo kubana miguu kwa mtu ambae ameshaonja ni utata. Kumbuka tunaishi na kuendeshwa na miili kwa kiasi kikuibwa kuliko roho.

Kuna changamoto kubwa sana wanapitia wasichana kwa hali hiyo ya kusema hapana kwa number 10 na mwisho wao huwa hauwi mzuri hata kidogo.

Mjadala mzuri, ila naomba niishie hapa tafadhali. Nitapenda niwe msomaji zaidi niendelee kujifunza.
 
Kwahiyo mkuu unaamini kama kuna dhambi kubwa na ndogo?
Kwanini mtu ajihukumu na wakati Mungu anasamehe na kusahau?
Kwahiyo unataka waendelee kufanya kwa sababu walishawahi kufanya mwanzo?
Hawana haki ya kukataa kwa sababu mwanzo walishafanya?
Nini maana ya msamaha??
Tunaishi katika mwili lakini tunaenenda kwa jinsi ya roho ndiyo maana Neno linasema enendeni kwa Roho wala hamtatimiza tamaa za mwili.
 
Namba 10 ni UTATA kwa dunia ya leo. ME na KE wanataka kujua compatibility kwenye idara hiyo kwa sababu mbali mbali. Hivyo inaweza kuwa sababu ya “uchumba” kuvunjika.
Kama watafanya basi wafanye ila ni kinyume na misingi tuliyowekewa.
Na hii imeleta matatizo mengi sana kwenye jamii zetu.
 
Reactions: BAK
Ni kweli kabisa kuna prons and cons na mwingine anamwambia bidada bila kupata ujauzito hakuna ndoa, mrembo anakubali na akishika mimba njemba inaingia mitini.

Kama watafanya basi wafanye ila ni kinyume na misingi tuliyowekewa.
Na hii imeleta matatizo mengi Sana kwenye jamii zetu.
 

Mkuu, msamaha unapatikana kwa yoyote atakaekiri na kukubali kosa bila kuangalia ukubwa au udogo wa dhambi, ila hiyo haimaanishi kwamba dhambi zote ni sawa. Nguvu ya msamaha ndio haichagui/haibagui dhambi. Tumeumbwa katika udhaifu wa mwili ila roho ndio inatuongoza.

Maisha yetu yanatulazimisha kuishi katika hali ya mwili zaidi kuliko roho. Ni ngumu kujitenga na vifungo na zile roho za malipizi hasa baada ya kuupokea msamaha. Roho za kukuangusha zitaendelea kukufata ili urudi katika uharibifu. Sasa msichana/mwanaume kuanza kuingia kwenye mahusiano ya uchumba huku unalikwepa tendo ni swala ambalo haliwezekani kibinadamu. Ni sawa na kuukaribia moto huku ukijipa imani huwezi kuungua.

Ndio maana kuna dhambi za kuombea au kukemea na pia kuna dhambi nyingine unatakiwa utoke nduki tu ukimbie, bila kujalisha imani yako kwa Mungu iko strong kiasi gani. Viungo vya uzazi ni silaha tuliyowekea kujiangamiza na kuangamiza nafsi zetu wenyewe. Ukisha karibisha roho chafu hapo, hata usali na kuokoka vipi lazima utakuja kuangukia hapo tu. Mifano ipo mingi jinsi watu na viongozi mashuhuri walivyoangukia hapo.
 
Ni kweli kabisa kuna prons and cons na mwingine anamwambia bidada bila kupata ujauzito hakuna ndoa, mrembo anakubali na akishika mimba njemba inaingia mitini.
Yeah
 
Reactions: BAK
👏👏
 
Kwahiyo wakubali kurudi dhambini kwa kuogopa roho ya malipizi??
Kwanini unasema kuna mambo hayawezekani wakati maandiko yanasema tunayaweza yote katika Yeye atutiaye Nguvu!?!!
Yote yanawezekana.

Naomba unijibu Hili swali, kuna dhambi kubwa na ndogo?
 
Sawa Anne ntaanza kufanyia mazoezi huu uzi nikifanikiwa ntaleta mrejesho.
 
Kwahiyo wakubali kurudi dhambini kwa kuogopa roho ya malipizi??
Kwanini unasema kuna mambo hayawezekani wakati maandiko yanasema tunayaweza yote katika Yeye atutiaye Nguvu!?!!
Yote yanawezekana.

Naomba unijibu Hili swali,kuna dhambi kubwa na ndogo?

Sijui uwasilishaji wangu ndio mbovu au namna gani sijui...

Kuumbwa katika udhaifu unafahamu maana yake? Kuishi katika ubinadamu ila uendane na roho unafahamu maana yake? Kumbuka tunaishi kibinadamu tukiwa na mwili wa nyama, hivyo mtu anaingia dhambini automaticaly kutokana na vile alivyoumbwa. Kumbuka anakuwa tayari ameshafungua milango ya uzinzi hivyo kuanguka ni dakika yoyote maana hakuna binadamu anaeweza kuishi na kuendana kwa roho muda wote.

Yes, dhambi zinatofautiana sana tu, zipo kubwa na ndogo. Ila nguvu ya msamaha inatoka kwa yoyote bila kujali aina au ukubwa wa dhambi as long as ametubu na kukiri kweli. Sijui umenipata hapo?
 
We bado mtoto ukikua utaacha. Hasahasa namba 10 imekufanya uwe mtoto zaidi, namaanisha ulimwengu bado hujaujua.
 
Ndiyo maana yupo Roho mtakatifu kutusaidia.
Bado msimamo wangu ni uleule,,wanawake wote wanapaswa kujitunza bila kujali Wana bikra au hawana.
Muache kuwalazimisha wanawake wasio nazo kufanya eti kwa sababu tu hawana.

Kuhusu dhambi ni kwamba hakuna dhambi kubwa wala ndogo,
Dhambi zote ni sawa na zinasameheka isipokuwa moja tu!
Kinachokufanya uhisi kuna dhambi kubwa na ndogo Ni madhara ya dhambi
Ila kiuhalisia hakuna dhambi kubwa wala ndogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…