Njia gani nzuri ya kutatua changamoto kama hii kazini kwangu?

Njia gani nzuri ya kutatua changamoto kama hii kazini kwangu?

Zongh

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2023
Posts
463
Reaction score
492
1. Bosi wangu ananifokea Sana kwamba sijui kazi ilihali ni kitu nilichosomea na najitahidi kuonesha juhudi

2. Bosi wangu ananifokea Sana hata kwa makosa ambayo kayafanya yeye mwenyewe kwa uzembe

3. Natumia kila njia ili niwe mfanyakazi mzuri na kumfurahisha bosi wangu lakini Bado anakuwa mkali kwangu

NB: Leo boss wangu kanifokea ilikuwa kidogo tuu niombe kuacha kazi na ilikuwa mbele za watu hadharani.
Ni taasisi binafsi

Je nifanyaje kwenye Hali Kama hii?
 
Me pia Boss wangu ni kama freemason, ananikosesha Amani daily. Anapenda sana dharau za kifala. Mara aseme Wamasai ni sawa na tumbili..

Wiki iliyopita alinifokea bila sababu ya msingi nikamuambia akiendelea nitamuua. Hatusalimiani tangu Alhamisi. Supervisor siyo Mungu.
 
Me pia Boss wangu ni kama freemason, ananikosesha Amani daily. Anapenda sana dharau. Wiki iliyopita alinifokea bila sababu ya msingi nikamuambia akiendelea nitamuua. Hatusalimiana tangu alhamis
Inasikitisha sana aisee,,inapelekea mpka mtu unashindwa kufanya kazi kwa amani na inaondoa utulivu wa akili kazini
 
1. Bosi wangu ananifokea Sana kwamba sijui kazi ilihali ni kitu nilichosomea na najitahidi kuonesha juhudi

2. Bosi wangu ananifokea Sana hata kwa makosa ambayo kayafanya yeye mwenyewe kwa uzembe

3. Natumia kila njia ili niwe mfanyakazi mzuri na kumfurahisha bosi wangu lakini Bado anakuwa mkali kwangu

NB: Leo boss wangu kanifokea ilikuwa kidogo tuu niombe kuacha kazi na ilikuwa mbele za watu hadharani.

Je nifanyaje kwenye Hali Kama hii?
Wee ke au me? Bosi wako ke au me?
 
1. Cha kufanya zile kazi anazo kupa ambazo hazikuhusu , siku akikupa ifanye alafu kesho yake asubuhi kabla kazi hazijaanza mwambie kuna kazi ambazo nafanya naona hizi kuna ambaye anastahili lakini Mimi nazifanya

2.Kingine hakikisha unakuwa unaenda na muda wa kazi uondoke muda ukiisha ili kazi zitakazotokea zipo nje ya muda asije kukupa na usijitie unajua vitu sana kuwa normal maana ukionesha unajua kazi zote utapewa wewe

3. Usiwe na mazoea naye siku ambazo hakuna sababu ya kukutana msionane ili kutokujenga kuzoeana

4.Sikiliza hii video
 
Attachments

  • VID-20250127-WA0000.mp4
    10.1 MB
Nipo taasisi binafsi
Binafsi Kaza tu, Ongea naye kwa Upole, weka kikao ambacho mtakua walau na myu mmoja au wawili wenye busara kulizungumzia hilo.

Kama Hakuna suluhisho na Fani yako ni marketable tafuta kazi ofisi nyingine upige chini hapo. Amani ya Moyo ni kitu muhimu sana hasa sehemu unayoshinda almost robo tatu ya siku yako.
 
Back
Top Bottom