Njia nzuri ya kutimiza Malengo , unapoweka malengo yako usiyawekee deadline

Tambua.

Ukweli ni huu: Malengo yasiyo na deadline ni ndoto; malengo yenye deadline ni mipango ya mafanikio.
 
Mfano wa Kuweka Deadline

Badala ya kusema: “Nataka kuandika kitabu.”
Sema: “Nataka kumaliza kuandika sura 10 za kitabu changu kabla ya tarehe 31 Desemba.”

Badala ya kusema: “Nataka kuanza biashara.”
Sema: “Nataka kusajili biashara yangu ndani ya miezi 3.”
Faida zipo hasara zipo, ukiweka deadline unakimbizana kukamilisha, unakua na ari ya kutimiza.....bila deadline unakua upo upo tu "nitafanya" "nitaenda" "nitaweka akiba"

COMMITMENT ✌️
 

Kwa nini Deadline ni Muhimu?

1. Inaleta Haraka na Umakini
Bila deadline, malengo yanabaki hewani. Utasema “nitafanya kesho,” na kesho hiyo haitafika kamwe. Deadline inakufanya usiseme “siku moja,” bali “kufikia tarehe fulani.”

2. Inakupa Kipimo cha Mafanikio
Deadline inakusaidia kupima kama kweli unakaribia ndoto zako au bado upo mbali. Kama uliweka lengo la miezi 6, mwezi wa tatu utajua kama unachelewa au upo sawa.

3. Inazuia Uzembe na Visingizio
Watu wengi hupoteza muda kwa sababu hawana muda wa mwisho. Deadline inakata mzizi wa visingizio, inakulazimisha kutenda sasa.

4. Inajenga Nidhamu
Unapoweka muda wa mwisho, unajifunza kupanga vipaumbele. Unajua lipi lifanyike leo, kesho na wiki ijayo.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…