Njia ya gharama nafuu na uhakika ya kusafirisha mizigo kutoka Dar kuja Mwanza

Njia ya gharama nafuu na uhakika ya kusafirisha mizigo kutoka Dar kuja Mwanza

Friedrich Nietzsche

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
2,095
Reaction score
3,649
Wakuu
Nafanya biashara ya kuchukua mzigo Dar. Changamoto ni gharama za usafiri unajikuta faida inaishia kwenye nauli.

Nielekezeni njia rahisi ya kusafirisha mizigo kutoka Dar kuja Mwanza kwa bei rahisi ila uhakika.

Achana na magari vishoka, wale wa kuunganisha unganisha wezi sana.
 
Treni ulikuwa usafiri wa mizigo wa uhakika, usalama na bei rafiki japo utausubiria kidogo
Unaweza kuwacheki pia Hood wale wenye mabasi ya Hood kipindi cha nyuma walikuwa wanasafirisha kwa uhakika sana
 
Ungesema ni biashara gani mkuu

Kuna biashara ukisafirisha piece moja faida yote inaishia kwenye nauli.

Lakini pia unaweza ukafanya yafuatayo
1. Kuchukua mzigo mkubwa kupunguza gharama za nauli, usumbufu na kuongeza faida
2. Kutumia company moja tu ya uhakika then ukishazoeana nao ni rahisi kuwa na discount
3. Kujenga mazoea na madereva wa mabus ingawa ni risk kiasi chake lakini madereva wanasaidia kama unasafirisha parcel ndogo ndogo.
 
Treni ulikuwa usafiri wa mizigo wa uhakika, usalama na bei rafiki japo utausubiria kidogo
Unaweza kuwacheki pia Hood wale wenye mabasi ya Hood kipindi cha nyuma walikuwa wanasafirisha kwa uhakika sana
Usafiri wa treni siyo😂😂sasa si unaweza subir week zima
 
Ungesema ni biashara gani mkuu

Kuna biashara ukisafirisha piece moja faida yote inaishia kwenye nauli.

Lakini pia unaweza ukafanya yafuatayo
1. Kuchukua mzigo mkubwa kupunguza gharama za nauli, usumbufu na kuongeza faida
2. Kutumia company moja tu ya uhakika then ukishazoeana nao ni rahisi kuwa na discount
3. Kujenga mazoea na madereva wa mabus ingawa ni risk kiasi chake lakini madereva wanasaidia kama unasafirisha parcel ndogo ndogo.
huu ushauri umeshiba
 
TUMIA CARGO (MALORI) WANA BEI RAFIKI SANA KWA SISI WAFANYABISHARA
MIMI MWANZO NILKUA NATUMIA BASI ILA SASA NIMEHAMIA KWENYE MALORI WAKO POA SANA
 
Ni biashara gani hiyo unachukua. Nataka nikuunganishe na jamaa yangu ana piga masafa hiyo njia.
 
Back
Top Bottom