Njia ya Kibiti kwenda kwenye laana ya Cabo Delgado

Njia ya Kibiti kwenda kwenye laana ya Cabo Delgado

Tatizo ni kujitoa ufahamu. Ukitoa jina linalohusishwa na uislamu, hao magaidi muunganiko wa wtz, wakenya, Rwandan n wengi hao ni wamakonde. Sio waarabu. Juu ya yote, hiki kikundi kinaaminika kufadhiliwa na mabepari, sio waarabu.
Watu wenye fikra kama zako ndio wanaotumiwa kuunda hizo militia groups. Vitu vingine ni very obvious, umeshaanza kuleta mtafaruku humu ndani. Muda mungine muwe mkifikiria kama hamjafanya utafiti kabla hamjaropokwa kashfa nzitooo.
Hayana akili hayo majamaa,yaani uwexo wake wa kufikiria umefikia hapo.Haoni huko Congo mambo yalivyo magumu,kwa ufupi watu weupe wanatuumiza sana,vijana wanalipwa hela ili kuleta vurugu wao ewanufaike
 
Dunia ina matrix sana , vikundi hivyo huwezi kuvikuta saudia , Qatar ,oman...Huyu Raisi wa Iran aliyekufa ndio aliwamaliza hao mamluki wa kutumia propaganda za kidni baadae aliwanyonga ndio wakamuita ''The butcher"


Watu hawa wanapewa pesa kukamilisha malengo ya wazungu , jiulize silaha wanatoa wapi ? Mzalishaji mkubwa wa silaha ni USA...Mtandao huo sawa na madawa ya kulevya kama ingekuwa uislamu unahusika nina hakika watu wengi wangekimbia hiyo dini ..Ni dini inaypokea watu wengi baada ya watu kuelewa kila mwk , ndio dini inakuwa kwa kasi.

Wale waliokamatwa pale Urusi juzi tu walisem islamic state ndio wanahusika , Putin akasema atafuatilia ili mwisho wa siku ni uongo , watu wanakuwa recruited na kulipwa kutokana na kutka utajiri na pesa ... Hakuna muislamu anaweza kuchoma na kuua watu kwa vile hukumu yake huko nchi za kiislamu ni kuuliwa tu , sasa iweje hawa wanaua ?
Wenzetu uwezo wao wa kufikiri umefikia kikomo,Wazungu watu hatari sana,tazama DRC inavyopata tabu
 
Njoo n
Yameundwa na Waislam.
Hezbollah makao makuu ni Lebanon nchi ya kiislam
Al Qaidar makao makuu ni Qatar nchi ya kiislam
Mujahideen makao makuu ni Iraq nchi ya kiislam
Hamas makao makuu Palestina nchi ya kiislam
Muslim Brotherhood makao makuu Egypt nchi ya kiislam.
Alshabab makao makuu Somalia nchi ya kiislam.
ISIS makao makuu ni Syria na Yemen nchi za kiislam
Boko Haram makao makuu Nigeria Jimbo la Waislam.

Mbona hayapo nchi za wakrsto au unataka kusema Waislam ni wajinga sana kukubali makundi ya wàkristo yakae kwao kuchafua uislam wao?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
congo umeiyacha mkuu
 
Huko Misikitini huwa akili zenu zinafanywaje mkishainamisha vile vichwa na kunyanyua matako juu. Mbona issue rahisi kabisa kuielewa lazima muifanye iwe ngumu? nani asiyejua mafundisho ya Rogo yalikuwa ya kueneza chuki baina ya raia? Kwani ni lazima haini afikishwe mahakamani? Nini kazi ya intelejinsia kama ni watu wa hovyo lazima waende mahakamani.
Mla nguruwe minyoo inakupa hasira sana
 
Hivi inakuwaje jeshi lina kila haina ya zana lakini inashindwa kuwadhibiti hao wahuni wachache? Waombe elimu kwa Tanzania wawape mbinu.

Dawa ya hao wahuni ni kuwamaliza kama walivyomalizwa majambazi tanzania.
Tatizo sio kumalizwa,tatizo wajanja washatia mkono kinachofanyika hapo ni mkiwa kwenye mwanga mnacheka kiza kikiingia kila mtu anabadilika.

Kuna siku nilikuwa home naangalia movie(tujipoze kidogo) ile movie ni serikali ya Braziri iliomba msaada kupitia balozi ya Marekani kuomba nguvu ya kwenda kupambana na makundi ya wauwaji katika viunga vya miji.

Basi idala ya kijasusi ikatua pale Brazir kutoka Marekani kikaangia mtaani kupambana,yale mapambano yalikuw makubwa sana,lakini kila wajomba wakijitahidi hakuna unafuu.

Inabidi wakafanya uchunguzi wakaja baini maofisa wa polisi wengi wao hujihusisha na magenge hayo kwa kutoa taarifa muhimu.


"hivyo mkuu wanawashindwa kwa sababu nyuma watu wanazunguukana,wanapigana huku wanatoa siraha,kuisha ngumu kama Congo ilivyoona mbali kutaka kuvifukuza bikundi vya kulinda amani"
 
𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐠𝐚𝐢𝐝𝐢 𝐲𝐚 𝐀𝐧𝐬𝐚𝐫 𝐚𝐥-𝐬𝐮𝐧𝐧𝐚.

- 𝐍𝐣𝐢𝐚 𝐲𝐚 𝐊𝐢𝐛𝐢𝐭𝐢 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐝𝐚 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐥𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐲𝐚 𝐂𝐚𝐛𝐨 𝐃𝐞𝐥𝐠𝐚𝐝𝐨.

- 𝐖𝐚𝐭𝐮 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐨𝐤𝐨𝐭𝐚 𝐦𝐢𝐢𝐥𝐢 𝐧𝐚 𝐯𝐢𝐜𝐡𝐰𝐚 𝐯𝐲𝐚𝐤𝐞 𝐩𝐞𝐦𝐛𝐞𝐧𝐢.

𝐒𝐄𝐇𝐄𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝟬𝟭:

Tarehe 20 mwezi huu wa tano, waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Dkt. Stergomena Tax analiambia bunge kuwa hali ya usalama katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji bado haitabiriki.

View attachment 3003798

Kwa maneno machache bado hali si shwari na sababu ni uwepo wa kikundi cha kigaidi cha Ansar Al-Sunna ambacho kinafanya mashambulizi huko nchini Msumbiji, jimbo la Cabo Delgado linalopakana na mipaka ya kusini mwa Tanzania.

Hivyo ni bayana, kama kikundi hiki bado kinahema, basi hatuna uhakika wa usalama wetu huko mpakani. Waulize wakazi wa vijiji vya mpakani, Kitaya na Michenjele, huko halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara juu ya USIKU ule.

Usiku huo wa tarehe 14/10/2020, giza halikuja mpweke kwenye ardhi yao bali liliambatana na wageni wasiowatarajia.

Ikiwa ni majira ya saa moja, wanatahamaki wamo katikati ya mashambulizi ya kundi kubwa la watu wenye silaha za moto.

View attachment 3003799

Watu wanakimbia huku na kule wakipiga mayowe ya hofu. Wavamizi wanachoma nyumba, magari, zahanati na pia ofisi ya kata.

Sekeseke la zaidi ya nusu saa. Kifo ama uhai.

Hali kuja kutulia, watu wanatoka walikojificha na walikokimbilia, wanakuja kuokota miili ya wenzao waliopigwa risasi na wengine waliochinjwa kama kuku.

Lakini mbaya, wanabaini wapendwa wengine hawapo. Wamebebwa wakaongozana na 'mabwana' wale kurudi huko walikotokea. Wengi wao wakiwa mabinti wa makadirio ya miaka 14 mpaka 20.

(pichani ni mwanaume aliyepoteza mke na mtoto wake wa kwanza)

View attachment 3003801


Baada ya wiki moja kupita, siku ya Alhamis tarehe 22 Oktoba, ndo' aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Simon Nyakoro Sirro anasimama mbele ya vyombo vya habari na kusema tukio lile lilifanywa na magaidi waliovuka mpaka kutoka nchini Msumbiji.

View attachment 3003822

Magaidi hao walikuwa 300 kwa idadi na wamefanya uhalifu ikiwemo mauaji. Baadhi wakakimbia na wengine wakakamatwa wanaendelea na mahojiano. Anasema lengo ni kupata mtandao wote wa magaidi.

Mtandao ulioanzia kule MKIRU (Mkuranga, Kibiti & Rufiji).

Kwa mujibu wa kamanda Sirro, wale Ansar al-sunna waliopo Msumbiji leo hii jimbo la Cabo Delgado, ambao ndo' wanamfanya waziri Stergomena Tax kusema kuwa usalama hautabiriki mpakani mwetu na Msumbiji, mtandao wao ulianzia hapa nchini mkoa wa Pwani.

Ila ni kweli Pwani tu? Kuna mahusiano gani na kwanini tena jimbo la Cabo Delgado mpaka leo hii? Mbinu za hawa magaidi ni zipi? Jeshi la SADC na Rwanda wamefikia wapi? Hali ya sasa ipoje na Rwanda ananufaikaje na mgogoro huu?

Ikumbukwe ripoti ya hivi karibuni, tarehe 17 Aprili 2024, kutoka gazeti la serikali ya Msumbiji, 'Boletim da Republica' imetolewa orodha ya watu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kushirikiana na kikundi hiki cha ugaidi, miongoni mwao wametajwa watanzania wawili; bwana Ally Yusuf Liwangwa (47) kutoka Dar es Salaam na bi. Safina Maulana (36) kutoka Mtwara.

View attachment 3003806

Sasa turudi kwenye siku ile ya tarehe 5, Oktoba 2017. Siku ya kwanza kabisa risasi kurushwa hewani kwa jina la Ansar al-sunna.

Siku hiyo katika mji wa pwani - Mocimboa de Praia - jimbo la Cabo Delgado, mambo yanabadilika ghafla katikati ya usiku na alfajiri.

View attachment 3003807

Kuanzia saa saba ya usiku, kundi la watu wanaokadiriwa thelathini kwa idadi wakiwa na silaha za moto na baridi, wanavamia mji huu wakilenga vituo vya wanausalama.

Mpaka kufikia saa kumi alfajiri, vituo vitatu ambavyo ni Mocimboa district police, kituo kidogo eneo la Awasse na kituo cha polisi cha maliasili na mazingira vinaripoti kushambuliwa na kutokea majibizano ya risasi.

View attachment 3003808
View attachment 3003814

Msemaji wa jeshi la Polisi, kamanda Inacio Dina (pichani), anawaambia waandishi wa habari mashambulizi hayo yamepelekea vifo vya maafisa polisi wawili na wavamizi watatu lakini ripoti zinasema watu 14 walifariki na pia vituo viliripoti kupotelewa na silaha.

View attachment 3003811

Wavamizi hao walikuwa wanazungumza lugha ya Kireno, Kiswahili na Kimwani. Hiki Kimwani ni lugha ya watu wa pwani ya eneo hili.

Kamanda anasema pia wamefanikiwa kuwakamata wavamizi kadhaa na hao watasaidia kupata taarifa zaidi ya wavamizi wenzao.

Kamanda anapoulizwa kuhusu mafungamano ya wavamizi hao na waislamu wenye itikadi kali mathalani Al-shabab wa kule Somalia, anasema ni mapema sana kusema hivyo. Watu hao kutumia 'local languages' za hapa Msumbiji kunamaanisha ni watu waliokulia hapahapa.

View attachment 3003815

Na hili linatukumbusha miezi sita nyuma ambapo redio ya taifa, Radio Mozambique, iliripoti kukamatwa kwa wanaume watatu wanotuhumiwa kuwa na 'connection' na Al-shabab.

Wanaume hao walikuwa wanawakataza watu kwenda vituo vya afya vya serikali na pia kuwapeleka watoto wao shule.

View attachment 3003816

Lakini baadae walikuja kuthibitika hawana mahusiano yoyote na Al-shabab ya Somalia japo wakaazi walikuwa wanawaita jina hilo, hivyo wakaishia kushikiliwa kwasababu ya kusababisha mashaka ya usalama.

Kamanda Inacio anawaondoa hofu wananchi akisema kikosi maalum cha kupambana na ugaidi kipo kazini na hivyo hali ya usalama itakomaa hivi punde.

Lakini tofauti kabisa na anachosema, huu ndo' unakuwa mwanzo rasmi wa mfululizo wa mashambulizi na mauaji katika jimbo la Cabo Delgado mpaka kuja kuvuka mpaka wa Tanzania.

View attachment 3003818

Kabla ya mwezi Oktoba kuisha, 'mabwana' wanamjibu kamanda kwa mashambulizi mawili katika kijiji cha Maluku na karibu na kijiji cha Columbe.

Mwezi unaofuata (Novemba) tarehe 29 wanavamia vijiji vya Mitumbate na Maculo. Wanaharibu kanisa na pia wanachinja watu wawili.

View attachment 3003819

Tarehe 13 January 2018 wanaingia mji wa Palma na kumwaga risasi sokoni na kwenye ofisi ya serikali. Watu watano wanakufa.

Tarehe 12 March, wanavamia kijiji cha Chitolo na kuchoma nyumba hamsini pia wanaua wakazi. Na kwa siku tatu mfululizo 20, 21 na 22 mwezi Aprili wanavamia vijiji kadha wa kadha wakiua na kuteka watu.

View attachment 3003823

Ni mwezi unaofuata, Umoja wa Afrika (AU) unathibitisha ripoti ya gazeti la Afrika Kusini iliyosema kuna wapambanaji wa Islamic State wamekwishaingia ndani ya Msumbiji, ripoti ambayo serikali ya Msumbiji ilikuwa inapingana nayo hapo awali.
View attachment 3003826
Na kilichofuatia baada ya hapo, ndo' hali ikawa mbaya zaidi. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huo 2019, watu zaidi ya arobaini na sita wakaripotiwa kuuawa kwa risasi na kuchinjwa kama kuku ikiwemo watoto wadogo.

View attachment 3003824

Achilia mbali nyumba lukuki ziliishia kuchomwa moto, watu kujeruhiwa na wengine kutekwa.

Si polisi, si jeshi la Msumbiji (FDS) wote wako hoi.

Mabwana hawa waliwavua nguo, kila mtu akaona uchi wao. Namna walivyo duni kwenye vifaa na mafunzo, na namna walivyo 'corrupt'.

View attachment 3003828

Wananchi wanasema mara kadhaa wameshuhudia wanajeshi wakikimbia eneo lao la ulinzi muda mfupi kabla ya eneo hilo kushambuliwa na magaidi. Wengine wanaiba mitumbwi ya wananchi ili wakimbie kujinusuru.

Kwa kaliba hii, mashambulizi yanazidi kutiririka, magaidi wakiamua wachinje ama wakatekate kama kuni (dismembering).

Zoezi hilo linaenda mpaka mwishoni mwa mwaka 2019 ambako serikali ya Msumbiji inakiri kuhitaji msaada, wamezidiwa.

Kwa kupitia FDS wanawekeana mkataba na jeshi la mamluki (mercenary) Wagner Group la nchini Urusi, na kwa mara ya kwanza kabisa mapema ya mwezi Oktoba mwaka 2019, mashambulizi ya kwanza ya FDS wakishirikiana na Wagner Group yanashika hatamu na yanaleta mafanikio.

View attachment 3003830
Wanawakimbizia magaidi huko misituni na wanafanikiwa kukamata watu makumi kwa makumi walokuwa wanasafiri kutoka jimbo la Nampula kwenda kuongeza nguvu ya magaidi huko jimbo la Cabo Delgado.

Lakini nguvu hii ya soda haikuchukua hata mwezi. Magaidi wanajibu kwa mtindo wa mashambulizi ya kushtukiza (ambushing) na FDS wanapoteza wanajeshi ishirini huku Wagner wakipoteza wanajeshi saba.

Mwezi wa kumi na moja, FDS wanapoteza tena wanajeshi kadhaa huku Wagner wakipoteza wanajeshi watano.

View attachment 3003832

Kipigo hiki kinapelekea pande hizi mbili, FDS na Wagner Group, kuingia kwenye mgogoro. FDS wanailaumu Wagner kutokuwaheshimu maafisa wao na huku Wagner wanalaumu jeshi la FDS pamoja na raia kuwa 'undiscplined'.

Hivyo oparesheni inafeli.

Wagner wanaondoka zao na katika ombwe hili, mkuu wa jeshi la Polisi, kamanda Bernadino Rafael, anaona afanye jambo upesi ili kujiimarisha kiusalama.

Anawasiliana na bwana Lionel Dyck, mkurugenzi wa jeshi binafsi toka nchini Afrika Kusini, Dyck Advisory Group (DAG), ambayo inahusika na utoaji wa vifaa na wataalamu wa mapambano ya kivita.

View attachment 3003837

Wanaweka makubaliano ya kupatikana kwa helikopta sita za vita na pia msaada wa anga kuwakabili magaidi.

Kwa muda huo 2020, hapo Msumbiji kulikuwa na helikopta moja tu ya combat, Russian-built MI-8, tena waliyopewa kama msaada na Rais Putin mwaka 2017.

View attachment 3003840

DAG wanaanza oparesheni yao April, 2020, wakikatiza anga la Msumbiji kupambana pembeni ya wanausalama.

View attachment 3003855

Lakini misheni yao ikiwa imebakiwa na wiki mbili tu kumalizika, linatokea shambulizi la mji wa Palma.

Shambulizi kubwa la kigaidi kupata kutokea katika ukanda huu wa kusini mwa Afrika.

Watu takribani 1,200 - 1,400 wanauawa ndani ya siku moja. Maiti zinazagaa barabarani. Mamia ya watu, ikiwemo watoto, wanaokotwa wakiwa hawana vichwa.

View attachment 3003862

Shambulizi hizi linashtua jumuiya mataifa ya kusini mwa Afrika (SADC), na sasa linaazimia kufanya kitu upesi kabla hatujaipoteza nchi ya Msumbiji mazima.

View attachment 3003933

Na Rwanda naye habaki nyuma. Anaingiza miguu yake eneo hili akidai kuisaidia Msumbiji kupambana na ugaidi ni njia mojawapo ya kujihakikishia usalama wake kama nchi.

View attachment 3003866

Lakini hana interests zingine hapa?

Kama hapana, je vile vikao vyake na raisi wa Msumbiji, Felipe Nyusi, pembeni ya mkurugenzi wa TotalEnergies, bwana Patrick Pouyanné, vinatoa ujumbe gani?


Ikumbukwe shambulizi hili la mji Palma lilitokea karibu na mradi mkubwa wa dola 'mabilioni' ulio chini ya kampuni ya kifaransa ya TotalEnergies na kupelekea kampuni hiyo kufunga shughuli zake kwa muda usiojulikana.

View attachment 3003938

Lakini yote kwa yote, Msumbiji imefikaje hapa? Intelijensia yake ililala wapi? Hawa magaidi ni kina nani na wanataka nini hapa Cabo Delgado?

Kuna mahusiano gani na mambo ya MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji)?

Habari inaanzia kule Mombasa, Kenya, miaka 12 ilopita...

𝐓𝐔𝐍𝐆𝐎𝐉𝐄 𝐒𝐄𝐇𝐄𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝟬𝟮:
Nasubiri muendelezo...
 
Acha kuwa mpumbavu tangu lini serikali inashambulia watu ? serikali ilikuwa na uwezo wa kumfikisha mahakamai wakati Rogo kashambuliwa .


View: https://youtu.be/go3z4EPz_Bc?si=6ybIdWvlRRSZqaVT

Minyoo ya Nguruwe inakuharibu kichwani hata kufikiria hujui.

Bila ya mchongo wa vyeti fake hauna jipya , kumbe hata hujui unaongela , basi kashambuliwa kama Tundu Lissu .

Mara vyeti feki,mara minyoo ya nguruwe,mara Tundu Lisu.

Mbona hauko consistent kwenye mada? Hapa wanaongelewa magaidi wa msumbiji,ila mlikuwa mmeficha matako yenu kwenye mashimo mkisubiri kuanza mashambulizi.

Wapi mleta mada ametaja uislamu? Nimekujibu wewe na mwenzio kwa sababu mnajihami sana.
 
Hayo mauawaji hayauhusu Uislam, hivyo ni vikundi vya kijambazi vinavyopachiwa majina ya Kiislam ili ionekane ni Waislam. Si kila Omari ni Muislam.

Uislam ni amani.

Kumbuka hayo.
Mbona yanajitokeza katika jamii za Kiislamu tu.
Tanga, Kibiti, Rufiji, Mkuranga, Zanzibar. Nk.
Wanafalsafa wanasema hayo makundi yanalelewa na Waislamu.
Mbona hayazaliwi Rolya, au Njombe, yaani kwenye Jamii za Kikristo ?
Mkubali mnawalea nyinyi Waislamu.
Sasa mnawaleaje maadui zenu.
Majina yao yote ni majina ya Kiislamu.
Waislamu mujitafakari.
Bila kujua udhaifu wako huwezi kujitathmini
Mna tatizo na bado mnajifanya ni watu wakweli sana.
Kama Waislamu musinge kuwepo Tanzania hayo Makundi ya Kigaidi yasingekuwepo kabisa.
Jitafakarini badala ya kukanusha kanusha tu.
Au ninyi ni watakatifu sana na hamkosei ?
Msalimie Gaidi mwenzako Ritz
 
Majeshi mengi ya afrika ni kulinda maslahi ya vyama tawala na watawala tu.

Hao magaidi wanaua wananchi miaka nenda miaka rudi, wakigusa ikulu zao ndio utaona kazi halisi.

Jambo lingine linalotia shaka ni kwa nini wewe mwandishi na waandishi wenzako mnatoa hizi habari za kutisha kila inapokaribia Uchaguzi?

Vita kuu ya kuuchafua Uislamu duniani ni DISINFORMATION.

Mwandishi wa makala hii analipa huu upupu alioumwaga. Hajaanza leo. Na analipwa na watendaji wa wasio waaminifu, wavuta bangi.

Ndio maana nimeuuliza mwanzoni tu.

Huu ujumbe wa makala unaolenga kuufungamanisha uislam na ugaidi.

Je, HIVI MAGAIDI WENYEWE NDIO WANAOJIFUNGAMANISHA NA UISLAM au WAANDISHI NDIO WANAOFUNGAMANISHA UGAIDI NA UISLAM?

Tuseme nchi hii kuna ugaidi wa kutengenezwa. False Flag Terror.

Tatizo la nchi la nchi yetu ni ubaguzi wa kidini tu hakuna cha ugaidi wa Waislam na Uislam.

......ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya.


Nitaweka threat inayojitegemea waraka wa waislam kwa serikali ukiitahadharisha serikali iache kuwalea waandishi wote wa kikundi hichi kinachofadhiliwa kuuchafua uislam.

Kama serikali haina mkono wake tunahitaji wamtafute azori ili atueleze ukweli wa mambo
Ngumu sana kuutenganisha uislamu na ugaidi,mbona duniani dini nyingi tu ila hazisemwi bali ni uislamu tu.
 
Upo page namba ngapi mkuu
 
Ngumu sana kuutenganisha uislamu na ugaidi,mbona duniani dini nyingi tu ila hazisemwi bali ni uislamu tu.
Nimekuelewa. Labda niulize tena ukristo una usafi gn au utakatifu gani hadi imani nyingine zipambane kuuchafua wakati kwa sasa wenyewe umejipamba na sifa mbaya kuchafuka
 

Attachments

  • IMG_20240415_155338.jpg
    IMG_20240415_155338.jpg
    171.9 KB · Views: 14
  • IMG_-anhwz8.jpg
    IMG_-anhwz8.jpg
    283.1 KB · Views: 14
  • 1717180998152.jpg
    1717180998152.jpg
    21.8 KB · Views: 13
Lakini hawa magaidi, madai yao huwa ni nini? Au malengo yao nini? Je, hawapo tayari kwa mazungumzo kama kweli yapo madai?
 
Back
Top Bottom